Jerry muro akoswa risasi?

Jerry muro akoswa risasi?

Chanzo hicho kilizidi kupasha kuwa baada ya watu, akiwemo jerry kuona daktari huyo akivuja damu kupita kiasi mguuni huku akiwa ameanguka chini, waliamua kumkimbiza hospitali ya marie stopes mwenge ambako anafanyia kazi.Habari zinasema alipofikishwa hospitalini hapo aliingizwa moja kwa moja chumba cha upasuaji ambako jeraha hilo lilishonwa.

Kuna haja ya PF3 hapa?
 
Muro aache kutumia magazeti ya shigongo, yatammaliza kabisa!! its unbelievable such an incident isipate media coverage zaidi ya gazeti la huyu hayawani wa kuharibu image za watu!!
 
hapa hakuna ukweli wowote hii ni bleh bleh tu.kama vile daraja la manyoya nakadhalika wa kadha.teh teh
 
Habari kanyaboya ndizo hizi tukio kubwa kama hilo litokee wiki nzima lisijulikane wakati mwandishi amesema kulikuwa na watu wengi hakuna kitu kama hicho hata kama alipigwa risasi kwa nini ihusishwe na Muro upigwe risasi Posta ukimbizwe Mwenge haiji kichwani habari za Uwazi zinajulikana ni za uzandiki ili wauze gazeti
 
Bora iwe si kweli manake vinginevyo itakua ni hatari. Somalia, Rwanda, Burundi Afghhanista n.k vilianza hivihivi.
 
Ee bwana inaonekana sasa Kova na timu yake wanataka kumteketeza Muro kwa kuwaanika? Those are minner people wakimuua tutaandamana na tutaona mwisho wao.
 
Haiwezekani habari ikafanyika eneo lile la wazi na kisha ikaonwa na uwazi peke yake....Msitufanye wajinga ebo!
Muro kiama chake kimefika lazima avune alichopanda( yaani kupenda rushwa then aishie jela).....hata hiyo risasi ingekuwepo kweli, ingekuwa niyeye alie suka mpango ili watu wamuonee huruma.
Muro ni kielelezo cha jinsi waandishi wetu wanavyopenda rushwa....kiasi kwamba hata JK kalitambua hilo na kulisema wazi wazi kisha wao waandishi wakanywea kama ishara ya kukubali kupenda kutafuna rushwa.
 
Hivi huyu bwana ana siri gani nzito hato hadi roho yake iandamwe na israeli kiasi kikubwa namna hii?
 
Muro aache kutumia magazeti ya shigongo, yatammaliza kabisa!! its unbelievable such an incident isipate media coverage zaidi ya gazeti la huyu hayawani wa kuharibu image za watu!!
Dah Comrade umeandika kwa uchungu sana vp alishakuharibia nn?
 
masikini Jerry wetu watamwacha hai kweli? Jamani wapinga ufisadi tushirikiane kufunga na kumwombea huyu ndugu yetu manake kwa hali hii hachelewi kukolimbiwa!
 
Hiyo source ya Uwazi hata mimi inanitia mashaka! Manake kwenye habari wanadai "Kitu kinachodhaniwa ni risasi" Ina maana ili kuprove kuwa ilikuwa ni risasi mpaka ipelekwe kwa mkemia kuu? Ok hata huyo layepigwa hiyo risasi naye anadai anahisi Jerry Mulo alikuwa sio mlengwa, Mlengwa alikuwa yeye!!
Habari imekaakaa ki udaku udaku sana! Ndio maaana haya magazeti siyaamini too much hyping!
 
Back
Top Bottom