Jerry muro akoswa risasi?

Jerry muro akoswa risasi?

Sumbalawinyo

JF-Expert Member
Joined
Sep 22, 2009
Posts
1,282
Reaction score
249
jerry muro akoswa risasi

pix.gif
habari ambazo gazeti hili ilizipata kutoka kwa chanzo chake cha kuaminika zilisema jerry ambaye alikuwa mahakamani hapo katika kesi yake anayotuhimiwa kuomba rushwa na watuhimiwa wengine wawili, alinusurika kupigwa na kitu hicho kinachoaminika kuwa ni risasi na badala yake ikampata mtu aliyekuwa naye mahakamani hapo.

Mtu huyo alifahamika kwa jina la dk. Paul andrew ambaye ni mtaalamu wa tiba za binadamu na ilielezwa kuwa alikuwa amekuja mahakamani hapo kumsindikiza jerry kwa maelezo kwamba ni ndugu yake.

"sisi tunaamini aliyekusudiwa ni jerry muro kwa sababu dk. Paul alikuja kwa bahati mbaya tu na hatufikirii kama waliorusha risasi walikuwa wakijua kuwa mtu huyo atakuja mahakamani lakini tunaamini waliofanya kitendo kile walijua kuwa muro atakuwepo kortini na inawezekana walikuwa wakimngoja nje ndipo akapigwa mtu wake mguuni." kilisema chanzo hicho.

Habari zinasema, dk. Paul baada ya kujeruhiwa akitokwa na damu nyingi, kitu kilichowashitua watu wengi walioshuhudia tukio hilo.

Mtoa habari huyo aliongeza kuwa walishuhudia gari moja dogo lenye ‘tinted' ambalo hawakuweza kujua namba zake likitoka eneo hilo kwa kasi, kitu kilichowafanya waamini kwamba watu waliotenda kitendo hicho cha kurusha kitu kilichomjeruhi daktari huyo, walikuwa humo.

Chanzo hicho kilizidi kupasha kuwa baada ya watu, akiwemo jerry kuona daktari huyo akivuja damu kupita kiasi mguuni huku akiwa ameanguka chini, waliamua kumkimbiza hospitali ya marie stopes mwenge ambako anafanyia kazi.
Habari zinasema alipofikishwa hospitalini hapo aliingizwa moja kwa moja chumba cha upasuaji ambako jeraha hilo lilishonwa.

Mwandishi wetu alimpigia simu juzi jumapili jerry na kumuuliza tukio la kurushiwa risasi iliyompata dk. Paul lakini awali alikataa kusema chochote, hata hivyo, baada ya kubanwa sana akathibitisha kutokea tukio hilo.
"ni kweli dk. Paul nilikuwa naye mahakamani alinisindikiza na alijeruhiwa vibaya mguuni na watu wasiojulikana na akakimbizwa hospitali ya marie stopes, lakini sitaeleza chochote zaidi ya hayo. Mtafuteni yeye awaelezee zaidi," alisema jerry.

Dk. Paul alipopigiwa simu alithibitisha kuumizwa mguuni na kitu anachoamini kuwa ni risasi na watu ambao hawajui.
Akisimulia mkasa huo, dk. Paul alisema alikwenda katika mahakama ya hakimu mkazi kisutu kumsindikiza jerry anayekabiliwa na kesi ya kuomba rushwa na mara baada ya shauri kuahirishwa walitoka nje ya mahakama.
"tulitoka nje ya mahakama na nikiwa karibu na barabara ya lami gari moja lenye tinted rangi ya silver (fedha) lilipita kwa kasi na nikashitukia mlio wa chini pyuu, nikasikia mguu una ganzi na nilipoangalia nikakuta unavuja damu," alisema dk. Paul.

Alisema anaamini kitu hicho kilichomuumiza ni risasi kwa sababu kilitoboa hadi kiatu chake na kumjeruhi vibaya mguu wake, hali iliyosababisha avuje damu nyingi.
"nilipata mshituko mkubwa ndipo ndugu na jamaa zangu wakanisaidia kunikimbiza hospitali ya marie stopes ambako nilishonwa jeraha," alisema dk. Paul.

Hata hivyo, alipodadisiwa zaidi alisema ana mashaka na baadhi ya wafanyakazi wa taasisi moja (jina tunahifadhi) kuhusika na njama hiyo ya kutaka kummaliza kutokana na kuhitilafiana, japokuwa inawezekana pia jerry ikawa alikusudiwa.

Alisema tukio hilo alikuwa hajaliripoti polisi kutokana na hofu kubwa aliyoipata iliyomfanya achanganyikiwe lakini akasema alikuwa akimsubiri jerry ili washauriane.

Gazeti hili katika matoleo yake ya nyuma liliwahi kutoa habari za kutishiwa maisha jerry na kuibiwa laptop yake yenye habari nyeti ambapo aliripo matukio hayo katika kituo cha polisi oysterbay akafunguliwa jalada namba ob/rb/18555/2009 na kituo kikuu cha polisi akapewa jalada namba cd/rb/15133/2009 na cd/ir/148171/2009 shambulio.


source: Uwazi
 
Kuna jambo hapa!
Kwahiyo sasa mission ni kumuua kabisa...God save this soul!
 
what is happening now....??!!
kwa hiyo ndo wanataka kutudhihirishia mchezo mchafu sio........
 
Jamani mbona hii habari ingehit magazeti? lakini sijaona kabisa kulikoni
 
mh kweli nchi hii kiboko so wataua wakweli hadi lini wataziba midomo wakweli hadi lini jamani
 
Duu! Sasa naona wala rushwa wanataka kummaliza kabisa kijana ili walale usingizi mnono.
 
Wakimua Jerry serikari itakuwa imehusika maana haya yote yanatokea hawachukui hatua. kwa mtazamo wangu Taaruma ya habari itakuwa imekufa. UWAZI NA UKWELI HAUTAKUPO TENAAAAAAAAAAAAAAAA katika taaruma hii mhimu.
 
Duh swala hapa sio source kama habari ina ukweli haijalishi imetoka uwazi ,kiu ,majira au mzalendo..Raia Mwema habari ni habari tu
hii ni hatari sana
 
Duh swala hapa sio source kama habari ina ukweli haijalishi imetoka uwazi ,kiu ,majira au mzalendo..Raia Mwema habari ni habari tu
hii ni hatari sana

Hii habari haijatulia hata kidogo.
Mtu unahisi umepigwa risasi halafu huendi kutoa ripoti polisi!!!
Kama kweli alipigwa risasi alitibiwaje bila ya PF3 ya poisi?
Tukio kubwa Kama hili linatokea hadharani ikimuhusisha Jerry ambae habari zake ni hot cake halafu lisiripotiwe na vyombo vingine vya habari isipokuwa "UWAZI"???
 
walimwengu wana mambo...............
ni unyama unyama tu....
 
Hii habari haijatulia hata kidogo.
Mtu unahisi umepigwa risasi halafu huendi kutoa ripoti polisi!!!
Kama kweli alipigwa risasi alitibiwaje bila ya PF3 ya poisi?
Tukio kubwa Kama hili linatokea hadharani ikimuhusisha Jerry ambae habari zake ni hot cake halafu lisiripotiwe na vyombo vingine vya habari isipokuwa "UWAZI"???
Nilikuwa karibu na eneo hilo sla mahakama ya Kisutu iku ya kesi ya Jerry (hasa wakati walipokuwa wanatoka mahakamani baada ya wale waumini wenzake kuangusha sala nzito), unfortunately, sikushuhudia tukio hili, nashangaa lilinipitaje
 
Hii habari haijatulia hata kidogo.
Mtu unahisi umepigwa risasi halafu huendi kutoa ripoti polisi!!!
Kama kweli alipigwa risasi alitibiwaje bila ya PF3 ya poisi?
Tukio kubwa Kama hili linatokea hadharani ikimuhusisha Jerry ambae habari zake ni hot cake halafu lisiripotiwe na vyombo vingine vya habari isipokuwa "UWAZI"???

hapo ndo pa kujiuliza swali
 
Hii habari haijatulia hata kidogo.
Mtu unahisi umepigwa risasi halafu huendi kutoa ripoti polisi!!!
Kama kweli alipigwa risasi alitibiwaje bila ya PF3 ya poisi?
Tukio kubwa Kama hili linatokea hadharani ikimuhusisha Jerry ambae habari zake ni hot cake halafu lisiripotiwe na vyombo vingine vya habari isipokuwa "UWAZI"???
Kwani PF3 ina lolote.......... watu wana vijihospitali vyao majumbani.......... hivi unadhani wale majambazi wanaojeruhiwa katika mapambano na polisi huwa wanatibiwa wapi...???
 
Kama nikweli alipigwa na kitu kichotoboa hadi kiatu na akavuja damu nyingi:-
1. Hospitali ya karibu wa mjini ni Hindumadal, Burhani, Dr,Khan, Aga Khan nyingine ni Tumain Muhimbili walishindwa kumwaisha ktk hizo maana alikuwa anavuja damu nyingi ss kutoka mjini hadi mwenge hapo pana nishangaza
2. Na je Hospital gani huwa inapokea majerui anaye vuja damu nyingi bila PF3 ya polisi.

Hii habari ina ulakini ndani yake??
 
Shakazulu, Mpitanjia na Borntown nakubaliana na nyinyi iweje tukio la risasi litokee mahakamani halafu watu wengine wasihisi kwamba kumetokea kitu cho chote? hata ikiwa hao wataalamu wametumia silencer lakini harakati zisingekuwa ndogo.

Na kweli kuna kihospitali au kidispensary kinachotibu bila ya PF3 hasa kwa issue kubwa kama hiyo, huyo mwenye kitegauchumi chake amechoka nacho? Akisakaziwa kuwa anashirikiana na majambazi atajitetea vipi?

Kwa maoni yangu hii ni ya kuuzia magazeti labda circulation imepungua sana.
 
mhhh nahisi hii ni trailer ya Movie. based on true story or not ???????????? Inawezekana tukio limetokea jumamosi au j2 siku mahakama zinakuwa wazi ila hakuna watu ???? Muhandishi , Jerry Muro na Dk ndio sterlings wa hii movie.

Tunasubiri full picha
 
Back
Top Bottom