Jenista Mhagama na gharama za kuhamia Dodoma

Jenista Mhagama na gharama za kuhamia Dodoma

Kweli huyu naye ni wa kumjadili? Ni kat ya viongozi ambao hufikiri kidogo sana, yaan ubongo wao mpya kabisa!!
 
Hapo ndio mwisho wa kufikiria kwa Waziri Mzigo Mhagama! Sio kosa lake upeo wake na ka shule hafifu!!
 
Msilalamike sana, unajua vetting ya kuwa waziri ni tofauti kabisa na ya kupata kazi za UN au zile za KPMG.
Kwa maana hiyo mnakuwa mnakosea kumlazimisha mwenzenu kufikiri nje ya mipaka ya uwezo wake!
cc: BAK
 
daaah hii nchi kila iitwapo leo haiishiwi comedy. funny enough komedi inaletwa na watawala
 
kufikiria ni kazi ngumu sana ndio maana ni wachache sana wanajihusisha nayo. by Albert Einstein
 
Hii Nchi Ingeshikwa tu Na Wachaga Mana Wanajua Kubana Matumizi ...

Tunaweza Amia Dodoma kwa Mabasi ya Mikoani Tu

Na ikagharimu Millioni kadhaa Tu
 
  • Thanks
Reactions: Ame
Watu hawakubali kila kitu kama wewe wanachunguza kwanza sio kila kitu ukiambiwa unapiga makofi bila kufikiria.

Na dhani wewe umechunguza na kama ndivyo

"Mhagama amesema suala la bajeti wanalijua wenyewe serikalini."

"Bajeti tulizopanga, hasa ya 2016/17 sisi tunajua tulipanga nini, tunafahamu mapato yaliyopitishwa na Bunge yakoje. Kwa mfano mimi Jenista (waziri) kwa mwaka huu mzima wa fedha nina mikutano minne Dodoma"

Haya pia uliyachunguza na kuoanisha na anachoki report mtoa maada siyo....

Hongera sana kwakutokumpogia makofi bila kuchunguza maandishi yake.

Ajionavyo mtu ndivyo alivyo...you reflect what you said!
 
Nyie mnaokosoa kana kwamba mmechiimba izo gharama , mmezikeshea na kuja na izo 1.5T ya ninin ? How do u know it comes to a t not b's

Serikali hii hazizitaki hizo esabu zenu , zinataka za mikanda iliyobanwa ...,
Suala la kuamia dodoma linawezekana by this government's way and never ever your way....

Na hili nalo hamlijui?
Sio kwanamna yenu, namna mnavotaka...! No way

Wanaishi jana yao leo hii....statusquo zao hawataki kuzivua....serikali yangu siyo serikali ya michakato, tunaendelea kulitazama....they still are in pono sleep!
 
Msilalamike sana, unajua vetting ya kuwa waziri ni tofauti kabisa na ya kupata kazi za UN au zile za KPMG.
Kwa maana hiyo mnakuwa mnakosea kumlazimisha mwenzenu kufikiri nje ya mipaka ya uwezo wake!
cc: BAK

What you dont know you give it a name.....haya hao waliofanyiwa vetting kambambe Tz hii wanaishi wapi mpaka watuache ss muda wote huo Dar hata baada ya kuamua kuhamia Dodona miaka 30 iliyopita?

Duuh ndiyo maana taarab asili yake ni Tz maana tu wasanii wazuri sana wa maneno!
 
My Take: Mhe.Mama Prof. Ndalichako ninarudia tena na tena, kuwa suala lako la Ukaguzi wa Vyeti ili uonyeshe unauchungu na nchi yako na unataka kutukomboa na tuondokane na ujinga,umasikini,maradhi,ufisadi n.k. fanya yafuatayo;
1. Tuodolee shaka kwa kuthibitisha vyeti vyako wewe binafsi kuwa mfano,na wazungu huwa wanasema a "Leader must set an example so others can follow" tujue wewe siyo K.i.l.a.z.a kwanza, na tupate kukuamini uyasemayo kuwa ni ya kweli na khalali uyafanyayo.
2. Ukaguzi na uthibitisho wa Pili uje kwa Vingozi wakuu WOTE, tukianza na MKuu wa Nchi,Makamu wa Rais,Waziri Mkuu, Mawaziri, manaibu wakuu, watendaji wakuu wa wizara na sekta zote za Kila wizara na Watumishi wake kwa kufuata itifaki (Protocal) na asiachwe hata mmoja kwa kisingizio chochote kile.
3. Taasisi zote za umma kwa kufuata pia itifaki (Protocal) kuanzia kiongozi wa Juu kabisa katika Taasisi husika hadi wa mwisho kabisaa.
3. Private Sectors zote bila pia kujali wala kubagua, na mwisho wote kabisaa asibakia Mwana wa Adam ambaye yuko juu ya ardhi hii hakukaguliwa na kuthibitisha,hapa ndiyo tutaheshimiana.
YOTE HII NI KWASABABU YA MATAMKO NA UWEZO WA VIONGOZI PAMOJA NA WANACHI WALIO WENGI WANA UWEZO MDOGO SANA WA KUCHAMBUA MASUALA MBALIMBALI YANAYOHUSU UCHUMI,SIASA,JAMII,UTAMADUNI NA KILA NYANJA.Na hivyo tunashindwa kujinasua katika matatizo mbali mbali na kujiletea maendeleo ya nyanja zote.

MY Take kwa Mtukufu Rais JPM: Ninakuomba Mtukufu ili kizazi chetu na kijacho kikukumbuke zaidi na jina lako liwe katika Historia na Kukumbukwa kwa vizazi na vizazi, binafsi ninarudia tena na tena kukuomba kuwa MCHAKATO WA KATIBA YA WANANCHI CHINI YA TUME YA JAJI WARIOBA UENDELEA KUANZIA PALE ULIPOKWAMIA NA KUIBORESHA HIYO KATIBA PENDEKEZI KWA KUIPA MENO MAKALI ZAIDI IKIWEMO YAFUATAYO;
1. Kuondolewa kwa Kinga ya Rais ilikuhojiwa na mahakama pale inapo hitajika au kuwa na sababu zitakazo onekana ni za msingi endapo amekiuka Katiba au kusababishia Taifa matatizo yasiyo kuwa ni ya lazima.
2. Mamlaka ya Rais kupunguzwa kama vile kuwateua Majaji Wakuu,Tume ya Uchaguzi,n.k
3.Kuundwa kwa Tume huru ya Uchaguzi.
4. Kuhojiwa matokeo ya Rais Mahakamani endapo kutakuwa na kutokuridhika au malalamiko ya matokeo yatakapooneka kuwa yana msingi.
5.Kuwa na Kikomo cha uongozi au kugombea uongozi na kuendoa mfumo wa everlasting kugombea au hadi wengine kufia madarakani hasa nafasi za ubunge ziwe ni awamu 2 TU kugombea.
6.Kufutilia mbali nafasi za uongozi hasa zile zinazo onekana kuwa hazina Tija kwa Taifa na wananchi wake kama vile uDC ambayo ni UKADA wa chama,kutafuta mfumo mbadala wa viongozi kama ma RC n.k
7. Mbunge kupigiwa kura ya kumwondoa madarakani endapo kwa mfano hatoonekan katika Jimbo lake husika zaidi ya miezi 6 pasipo sababu za Msingi zilizo mfanya asionekana kwa wananchi wake.
8. Muundo wa Muungano ninapendekeza kuwa na Serikali TATU, yaani Serikali ya Jamuhuru ya Muungano wa Tz., Serikali ya Tanzania na Serikali ya Zanzibar.
9.Haki za binadamu zitambulike kikatiba na kuwa wazi.
Na kadha wa kadha....
Hayo kwa pande zote ndiyo maoni yangu, kwa Waheshimiwa Viongozi,na ninayo yaona endapo yatatekelezeka huenda tukaagana na matatizo ya mara kwa mara na mbali mbali yanayojitokeza katika Taifa letu, na pia huenda umasikini,ujinga,maradhi,ufisadi n.k. yakawa kikomo.
 
Afu TBC bhana...
kabla ya kipindi wameweka hotuba ya baba wa Taifa...
Ina kama kijembe hivi...
Inasema 'ukiona watu wanapinga kuhamia kwenye vijiji vya ujamaa si kwamba hawataki; wameshajenga nyumba zao, wana mifugo nakadhalika...hawawezi kuhamia wasiko kujua na utegemee kukuunga mkono'


Nikasema huyu kamaliza yote...kwa mfanyakazi mpya hiyo decision ni rahisi kufanya...kwa wenye familia na wamesha settle wengi wamekumbwa na msogo wa mawazo...maana wamekuwa forced kuishi ki bachelor na umri umeshaenda...

wamelazimishwa kuhudumia familia mbili...Dodoma na Dar...

Si kwamba watu wanapinga sababu hawataki...wanapinga sababu wamechanganyikiwa...
 
Tukisema uamuzi wa serikali kuhamia dodoma ulikuwa wa kukurupuka watu wengi walipinga.
 
Viunzi 6 Magufuli kuhamia Dodoma

Hapo kwenye rangi, msome Mkurugenzi Mkuu wa CDA kwenye hiyo link hapo juu. Huwa hatukurupuki.

Nyie mnaokosoa kana kwamba mmechiimba izo gharama , mmezikeshea na kuja na izo 1.5T ya ninin ? How do u know it comes to a t not b's

Serikali hii hazizitaki hizo esabu zenu , zinataka za mikanda iliyobanwa ...,
Suala la kuamia dodoma linawezekana by this government's way and never ever your way....

Na hili nalo hamlijui?
Sio kwanamna yenu, namna mnavotaka...! No way
 
Huyu Jenista Mhagama anadhani hizo posho za Mawaziri za miezi mitano ndiyo zitatosha kugharamia Serikali kuhamia Dodoma? Duh!

Gharama za kuhamia Dodoma ni kati ya 1.5 trillion mpaka 2 Trillioni halafu yeye anakuja na posho za miezi mitano za Mawaziri na anashindwa kuweka wazi hata hizo posho zake anazostahili kupata kwa hiyo miezi mitano.

========

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Uratibu wa Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Walemavu, Junket's Mhagama amesema suala la bajeti ya kuhamishia makao makuu ya Serikali kutoka Dar es Salaam litatatuliwa kwa kutumia posho za safari za mawaziri.

Akizungumza katika kipindi cha Safari ya Dodoma kinachorushwa na kituo cha televisheni cha Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC), Mhagama amesema suala la bajeti wanalijua wenyewe serikalini.

“Bajeti tulizopanga, Hausa ya 2016/17 sisi tunajua tulipanga nini, tunafahamu mapato yaliyopitishwa na Runge yakoje. Kwa mfano mimi Jenista (waziri) kwa mwaka huu mzima wa fedha nina mikutano minne Dodoma. Kwenye ile mikutano yote natakiwa kulipwa posho, maana yake ni kuwa napaswa nipate posho ya miezi mitano, sasa fedha hiyo ndiyo itakayoingizwa kwenye gharama za kuihamishia Serikali Dodoma,” amesema.


Chanzo: Mwananchi
Mleta uzi nadhani hukumuelewa Jenista vizuri.Nadhani alikuwa anaongelea budget components.Ndio akataja hiyo component ya posho.Siamini kwamba alikuwa na maana kwamba posho ndio the only source of money ya kuweza kuihamisha serikali Dodoma.Kwanza hela ya posho ni hela binafsi ya mtumishi ya kujikimu!
 
nilimsikia na mimi kwenye Interview ya TBC kipindi cha Safari ya Dodoma anadai maandalizi ya ofisi za serikali dodoma yamekamili kwa asilimia 75 na makazi kwa watumishi asilimia 70 hivyo wanaweza kuhamia kwa awamu awamu ikabidi nizime TV nikalale
ya chogo/kibiyondo au flat?
 
Ni nasubiri nisikie tu wapo Dodoma, nishachoka kusikia mipango.
 
Back
Top Bottom