Mnataka Da Jenny alione bunge lijalo katika tiviii siyo?
baada ya kikao kuahirishwa siku ile nilicheka sana ...kuna picha ilitoka ..mbunge suleiman kumchaya[ambaye amepata kuwa msaidizi wa mkapa siasa]..na moja wa wabunge wa lindi anakotoka ghasia...akiwa amemkumshika mkono anamkokota ..mama ghasia ...huku mama wa watu wazi akionekana na majozi ya kulia...na hasira ...kutokana na mabomu aliyorushiwa na jenista...inaonekana bifu lao litakuwa kali sana hawa!!..
kuna aliyeuliza marriage status ya maama ghasia ...ameolewa na mtaalamu abdulrahman ghasia ambaye ni mwenyekiti wa TFF wilaya huko lindi...[sidhani kama ameshastaafu TFF]
BUNGE LA TANZANIA
MAJADILIANO YA BUNGE
MKUTANO WA KUMI NA MBILI
Kikao cha Kumi na Tano Tarehe 1 Julai, 2008
………Mheshimiwa Spika, mwisho lakini sio kwa umuhimu, napenda kuwashukuru wazazi wangu, baba yangu, Mzee Abdulrahman Mohammed Ghasia na Mama yangu – Kashi Balozi kwa malezi yao na pia napenda kumshukuru mume wangu Mr Yahya Mhata na wanangu kwa kunitia moyo na pia kwa kunivumilia pale ninapotea muda wao katika kutimiza majukumu yangu ( Makofi )
Gobole = DCM Mbagala - Kariakoo au Gongo la Mboto - Kariakoo
Aksante kwa kujaribu kunifafanulia Masatu but ndo umenipoteza kabisaaaa. Asa DCM la Mbagala na Mh. Mhagama ndo vinahusianaje? Anaishi mbagala au?
Rwabugiri,
Maneni mazito sana Mkuu.
Mie sijali kama huyu Mhagama ana sifa gani na kafanya nini huko nyuma. Hawa viongozi wetu wamejiachia sana. Wakiwa wanatunguliwa namna hii walau wataanza kuwa makini. Si mnaona hata Masha sasa hatumsikii? Nafikiri kashashika adabu yake. Sidhani kama bado anakunywa ovyo Rose garden na kuropoka (iliandikwa humu JF). Viongozi wetu walijiachia/wamejiachia sana sana utafikiri akina dada wakishaolewa, kutunza miili yao inakuwa historia. Siku anaolewa mwembamba, hapo ongeza sasa azae, atajaa utafikiri anaenda kucheza Sumo (akina dada don't take it personal na hii si akina dada wote na nafahamu wengine huwa ni matatizo ya hormons).
Mama Mhagama, shambulia hawa wote. Na maadamu imeandikwa "achezae na upanga basi hufa na upanga", wapinzani wa Mhagama wameshapewa mfano wa jinsi ya kumkoma nyani. Kwani alikuwa wapi miaka yote nyuma? Na yeye atakomwa (na naombea akomwe) wakati wa uchaguzi. Hili joto likiwa kali, litatusaidia kujenga miiko ya viongozi kwani mtu ukimess up, wanakuondoa kwani utawapakazia wote.
Hongera CHADEMA na hasa Dr. Slaa na Zitto kwa kuleta huu mchezo wa Mabomu ingawa muasisi wa mabomu ndugu Mzindakaya ALIRUBUNIWA ki-siasa na Mkapa na akapata kitu kidogo na sasa mabomu yake kayafiata kabisaaa. Shame on you Mzindakaya na Mafisadi wote waliokuingiza kwenye Mduara wao.
Pheeww. Hii haijakaa sawa.
Edit hapo na kuandika ALIRUBUNIWA. Original imeshabadilishwa.
Mnataka Da Jenny alione bunge lijalo katika tiviii siyo?
Kwa kifupi ngalangala au mbofu mbofu bure ya ghali!
Still dont get it?
Thanks. Turudi kwenye mada sasa. Kwa kupima inaonyesha kuna tofauti kubwa kati ya issues za wabunge wa upinzani na baadhi ya issues za wabunge wa CCM.
Hile ni National Assembly, na matatizo yake ni lazima yakae kitaifa-taifa. Mama Mhagama inaonyesha ana upungufu fulani. Na huu upungufu unawakabili wabunge wengi na ndio maana bunge letu ni muhuri wa serikali.
Wabunge wengi hawaelewi ni sehemu gani za kupeleka matatizo. Pamoja na kuwa Mama Mhagama alitaka kulipua mabomu lakini sio waziri anayeshugulia waalimu hasa wa shule za msingi.
Inanipa wasiwasi kuona hata baadhi ya wanaJF mnafikiri alichofanya Mhagama ni sawa.
Matatizo yanayowapata waalimu kati majimbo ya Zitto, Slaa, Mhagama ni sawa. Lakini Zitto na Slaa hawajandika listi ya matatizo ya waalimu na kumpelekea waziri Ghasia.
Mkuu angalia hizo fact zako mkuu, Kama Hawa Ghasia yeye ndo waziri anaye husika na utumishi, sasa ulitaka apeleke wapi? ili hali ni madai ya watu kuajiliwa/kuwa watumishi?
Si hilo pia mkuu, ok, tuseme alikosea akapeleka kusiko, kwanini asijibiwe kwamba apeleke sehemu fulani ndiko kunako husika? Kumbuka haya madai ni ya myaka mitatu mkuu!
Yaani kama ni Kumkoma nyani, Mhagama did it!, Dada Hawa anachopaswa fanya ni kukubali yaishe ashughulikie hayo matatizo na liwe ni fundisho kwake.
Hizi bla bla za kutafuta eti tumchafue Mhagama kwa vile kasema kweli zilaaniwe kwa nguvu zote, Tunahitaji watu kama Mhagama wanao timiza wajibu wao wa kuiwajibisha serikali.
Alikosea niambie hao waalimu wanafundisha shule gani? Sekondari au za msingi?
Je hao walimu walikuwa na mikataba gani ya kazi na katika mikataba hiyo ya kazi ni nani mwajiri wao? Unataka kusema ni wizara ya utumishi?
Sipo hapa kutetea serikali. Lakini masuala ya kuuliza ukosefu wa chumvi bungeni sio kumkoma nyani.
Mkuu kama shida ya wananchi ni chumvi, na anaye paswa kuwapa chumvi kajibweteka hatimizi wajibu wake, ukimkumbusha alete hiyo chumvi si ndo wajibu wako? si ndo umemkoma kwani hujataka enda mmalizane pembeni?
Sasa yeye kama alijua hilo swala lina husu wizara nyingine kwanini asingetoa majibu elekezi kwamba hilo swala lipelekwe sehemu fulani?
Mkuu katika yote, ni kwamba Hawa hakutimiza sehemu yake, ama la kutatua tatizo, ama kutoa majibu elekezi.
Hata hivo hii kwamba si wizara ya Hawa inayo husika unaiibua wewe hapa, mbona Hakujibu hivo bungeni akaishia kutoa majibu rahisi kwamba ni darasa la saba hawastahili kuajiriwa?
Bado nasimama upande wa Mhagama na nampongeza sana kwa kutimiza wajibu wake!