Jenista Joakim Mhagama | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Jenista Joakim Mhagama

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Tina, Jun 29, 2009.

 1. Tina

  Tina JF-Expert Member

  #1
  Jun 29, 2009
  Joined: Jul 9, 2007
  Messages: 571
  Likes Received: 73
  Trophy Points: 45
  Ni nani huyo Jenista Joakim Mhagama?

  Mbunge wa Peramiho kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM)?

  Je, ni yule yule aliyekuwa Mbunge wa Viti Maalumu katika kipindi cha mwaka 2000-2005?

  Akiwa karibu sana na viongozi wa serikali iliyopita hususan Frederick Sumaye na wenzake?

  Nani anamjua vizuri huyu? Hususan katika sherehe nyingi za pale Dodoma? Nani anamjua vizuri huyu ambaye juzi alionekana kama mtetezi wa walimu wenzake wa zamani? Kwanini hasa amemsaliti mwanamke mwenzetu Hawa Ghasia?

  Kuna siri gani? Waziri huwa hafanyi kazi mikoani na alipompa orodha ya walimu wenye matatizo, alijibiwa, "nimepokea siwezi kuwa na majibu hapa, ngoja niagize huko mikoani wanipe maelezo nitakupatia, sasa subiri baada ya kumaliza bajeti nitakuwa na majibu" yeye akasema, "sitasubiri, leo leo nitakulipua".... sasa alikuwa na haraka gani?

  Je, lengo ni kulipua, ama kupata ufumbuzi wa tatizo? Je, huo ndio utaratibu wa zimamoto? kama yeye alikaa na hayo majina kwa miezi mitatu bila kupata majibu, imekuaje amtake mwenzake awe na majibu ya vijiji vya Songea papo kwa papo?

  Kwa maoni yangu, huu sasa ni mchezo wa kukata tamaa na kutafuta wachawi kwa matatizo ya wabunge wetu ambao wameshindwa kazi majimboni. Baadhi watatumia kiini macho cha kufuatwa fuatwa na maadui zao, wako watakaosingizia wanaotaka ubunge 'wao' lakini je, kuna mwenye HAKI MILKI YA UBUNGE? Kama wameshindwa waache wenye uwezo waingie jimboni na kama mtu ulishindwa kwa miaka minne kufanya kazi jimboni, huwezi kupiga kelele bungeni kipindi kilichobaki ukafanikiwa. Waende majimboni kufanya kazi na wananchi na si kupiga kelele
   
 2. T

  TwendeSasa Senior Member

  #2
  Jun 29, 2009
  Joined: May 24, 2008
  Messages: 128
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  mmh mie yangu masikio
  Ila alitoa changamoto
   
 3. Ng'wanza Madaso

  Ng'wanza Madaso JF-Expert Member

  #3
  Jun 29, 2009
  Joined: Oct 21, 2008
  Messages: 2,278
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  Alishampa siku nyingi hayo majina na hakuyafanyia kazi sasa anampa siku tatu kama huyo waziri alishindwa kwa muda ule wote je angeweza kwa zile siku tatu?, au alitaka kumfumba mdomo? ili bajeti yake ipite kiulaini?
   
 4. Halisi

  Halisi JF-Expert Member

  #4
  Jun 29, 2009
  Joined: Jan 16, 2007
  Messages: 2,810
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  Ahaa!!! mwacheni mwenzenu atumie nafasi aliyonayo na vipaji vyake kufikia malengo yake!! (joke)

  hata mm nitashangaa sana kama huyu mama hatokuwa na mambo ya kinyume kinyume. Nakumbuka nikiwa namsaidia kazi yake muhimu pale Dodoma, alinisaliti kwa kunidanganya, lakini baadaye akaona aibu baada ya uongo wake kubainika. Aliniambia yuko njiani kwenda dar, lakini nilipofika mahala fulani pale pale Dodoma, nikiwa sijakaa sawa akaingia na kutahayari, akisema, "kaka samahani, nitakutafuta baadaye" na hakunitafuta tena, nikamsamehe na kuendelea kumsaidia bila ushirikiano wake. Nikaifanya kazi yake kwa msaada wa watu wengine na yeye baadaye akanipigia simu, "nashukuru sana, imenisaidia sana." nikamwambia asijali, tuko kulitumikia taifa. Kwa ufupi si mwadilifu hata kidogo
   
 5. M

  Masatu JF-Expert Member

  #5
  Jun 29, 2009
  Joined: Jan 29, 2007
  Messages: 3,285
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Sera za kulipua mabomu zinalipa hususan kipindi hiki kuelekea uchaguzi mkuu mwakani. Walianza kambi ya ushindani na lipu lipu zao na wana CCM wameona kumbe ina draw attention hasa kwenye media, kwa maana ina make headlines kama waziri atolewa jasho, mbunge ... amlipua waziri, mbunge asema mawaziri wana roho mbaya na walaaniwe, majibu ya waziri ni ovyo ovyo nk.

  Hiyo issue ya walimu ingweza kabisa kumaliza ka kutumia busara ndogo tu lakini yatari mbunge alikuwa anataka kuwaonyesha wapiga kura wake kuwa yupo.

  Kumbuka uchaguzi mkuu upo mwakani kila mtu anataka kurudi jimboni aweze kusema si mlinisikia nilivyo mbwatuakia waziri?
   
 6. Halisi

  Halisi JF-Expert Member

  #6
  Jun 29, 2009
  Joined: Jan 16, 2007
  Messages: 2,810
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  hayo majina aliyopewa siku nyingi yalifanyiwa kazi na majibu ndio yale, sasa akawa na follow up, ambayo ndiyo akapewa muda. Angaalao kwa sisi hapa Dodoma ndio tumeona hivyo. Lakini huyo dada si mwadilifu na si muungwana.
   
 7. Limbani

  Limbani JF-Expert Member

  #7
  Jun 29, 2009
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 1,441
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 145
  Kwani kaolewa huyu mama?
   
 8. Chakaza

  Chakaza JF-Expert Member

  #8
  Jun 29, 2009
  Joined: Mar 10, 2007
  Messages: 23,668
  Likes Received: 21,901
  Trophy Points: 280
  Limbani! Wataka kuoa yakhe!
   
 9. M

  Masatu JF-Expert Member

  #9
  Jun 29, 2009
  Joined: Jan 29, 2007
  Messages: 3,285
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Unataka kutia timu?
   
 10. G

  Game Theory JF-Expert Member

  #10
  Jun 29, 2009
  Joined: Sep 5, 2006
  Messages: 8,571
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 0
  Gobole lile
   
 11. Limbani

  Limbani JF-Expert Member

  #11
  Jun 29, 2009
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 1,441
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 145
  Hapana ndugu yangu! Nasikia sifa zake huyu mama kwamba nae Alhamdulilah...!
   
 12. Bishanga

  Bishanga JF-Expert Member

  #12
  Jun 29, 2009
  Joined: Jun 29, 2008
  Messages: 15,347
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 0
  Alhamdulillah? exactly what do you mean? nitoe ushamba ndugu yangu!
   
 13. MwanajamiiOne

  MwanajamiiOne Platinum Member

  #13
  Jun 29, 2009
  Joined: Jul 24, 2008
  Messages: 10,478
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  GT Gobole maana yake ni nini? Hebu tuwe na heshima kwa binadamu wenzetu!
   
 14. d

  dmatemu JF-Expert Member

  #14
  Jun 29, 2009
  Joined: Mar 14, 2008
  Messages: 591
  Likes Received: 140
  Trophy Points: 60
  ndo mwanzo wa kampani za ubunge mwakani hakuna kitu hapo, huo ni mchezo wa kuigiza tu. kwani Jenista si alikuwa mbunge tangu mwaka 2005, na je hakuwaona hao walimu kuwa wan zaidi ya miaka 15 hawajalipwa? sa siku zote alikuwa wapi? huo ndo umbea wa viongozi wetu. Juzi tumesikia JK kazindua miradi ya maji, swali linbaki pale pale, je hayo matatizo ya maji yameanza mwaka 2009? Mbona hawa viongozi wan maskhara?
   
 15. M

  Masatu JF-Expert Member

  #15
  Jun 29, 2009
  Joined: Jan 29, 2007
  Messages: 3,285
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135

  Gobole = DCM Mbagala - Kariakoo au Gongo la Mboto - Kariakoo
   
 16. P

  Phillemon Mikael JF Gold Member

  #16
  Jun 29, 2009
  Joined: Nov 5, 2006
  Messages: 8,856
  Likes Received: 2,432
  Trophy Points: 280
  ..naukubali women solidarity....lakini sidhani kama ni muhimu kuteteana hata pale inapoonekana wazi katika hili kuwa waziri ghasia anaonekana kuwa na ka uzembe ,ka kiburi, na ubishi kwa jambo ambalo angeweza kumkubalia kiungwana tu kuwasaidia wale watumishi wenye sifa na wasiokuwa na sifa ....wangeweza aidha kustaafishwa [kupunguzwa]...na sana kama wangehitajika wangepewa mikataba mifupi mifupi...kama wanavyofanya sehemu nyingi tu.

  lakini pale ilionekana wazi kuwa mama ghasia na jenista wanalo zaidi ya hili ....na mara zote hali hizi ndizo zimekuwa zikidumaza ushirikiana wa nyie kina mama......kuna tabia ya kina mama kudharauliana....na sasa hii inatupa wakati mgumu kujuliza kuwa kama siku wakifikia kina mama asilimia 50% bungeni ...bunge linaweza jeuka sehemu ya kusutana na mipasho na kauli ya spika mstaafu msekwa ....ya ubishi wa "wivu wa kike" itakuwa dhahiri!!
   
 17. P

  Phillemon Mikael JF Gold Member

  #17
  Jun 29, 2009
  Joined: Nov 5, 2006
  Messages: 8,856
  Likes Received: 2,432
  Trophy Points: 280
  baada ya kikao kuahirishwa siku ile nilicheka sana ...kuna picha ilitoka ..mbunge suleiman kumchaya[ambaye amepata kuwa msaidizi wa mkapa siasa]..na moja wa wabunge wa lindi anakotoka ghasia...akiwa amemkumshika mkono anamkokota ..mama ghasia ...huku mama wa watu wazi akionekana na majozi ya kulia...na hasira ...kutokana na mabomu aliyorushiwa na jenista...inaonekana bifu lao litakuwa kali sana hawa!!..

  kuna aliyeuliza marriage status ya maama ghasia ...ameolewa na mtaalamu abdulrahman ghasia ambaye ni mwenyekiti wa TFF wilaya huko lindi...[sidhani kama ameshastaafu TFF]
   
 18. R

  Rwabugiri JF-Expert Member

  #18
  Jun 29, 2009
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 2,777
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135

  Hapa msitake muonea huyo Muhagama, yeye katimiza wajibu wake kbisaaaaaa kama mbunge, kawakilisha kero za wananachi wake,

  Utaratibu aliufuata, majina alimpa siku nyingi, hadi akafatilia kwa PM na kwa PM wakaandika walaka ambao hata hivo ofisi ya Ghasia wakaupuuzia?/hawakuwajibikwa kwao,
  Sasa mlitaka afanyeje? Haya mambo ya kuoneana haya na ksuema tumaliziane pembeni, tufunike wasisikie, ohoo, utakuwa umemsema mwenzio vibaya ndo yametufikisha hapa tulipo!

  Hawa angetimiza wajibu wake, Mhagama angemuanzaia wapi? Halafu anakuja na majibu mepesi kwa PM eti hawa ni darasa la saba hawana sifa kitu ambacho si kweli wengine wamemaliza hadi form 6, na si hilo tu, sheria zetu bado zinaruhusu hata hao std 7 kuajiliwa kama wamepitia kozi mbali mbali.

  Sipendi kabisa watu wanao taka kuleta double standard humu ndani JF, Ghasia hajatimiza wajibu wake, kalalamikiwa na mamlaka husika thats it! atimize wjibu wake basi,

  Afu hizo longo longo mwanamke mwenzetu, binafsi nilitegemea mwanamke awe na uchungu wa kuona mtu anafanya kazi 20 yrs bila ajira. Halafu unaposema mbali, kwani Hawa ndo anatakiwa aende huko mikoani? yeye ni waziri, ana watu chini yake kibao, ni kiasi cha kutoa agizo kwamba hili lishughulikiwe and thats it!

  Hata kama Mhagama ana mapungufu yake, hiyo haihalalishi asiseme mapungufu ya utendaji wa Hawa. Angekuwa alitimiza wajibu wake, ange muanzia wapi?

  Bravo Muhagama kwa kutimiza majukumu yako ya kuwakilisha kero za wanchi.
   
 19. Sikonge

  Sikonge JF-Expert Member

  #19
  Jun 29, 2009
  Joined: Jan 19, 2008
  Messages: 11,503
  Likes Received: 539
  Trophy Points: 280
  Rwabugiri,
  Maneni mazito sana Mkuu.

  Mie sijali kama huyu Mhagama ana sifa gani na kafanya nini huko nyuma. Hawa viongozi wetu wamejiachia sana. Wakiwa wanatunguliwa namna hii walau wataanza kuwa makini. Si mnaona hata Masha sasa hatumsikii? Nafikiri kashashika adabu yake. Sidhani kama bado anakunywa ovyo Rose garden na kuropoka (iliandikwa humu JF). Viongozi wetu walijiachia/wamejiachia sana sana utafikiri akina dada wakishaolewa, kutunza miili yao inakuwa historia. Siku anaolewa mwembamba, hapo ongeza sasa azae, atajaa utafikiri anaenda kucheza Sumo (akina dada don't take it personal na hii si akina dada wote na nafahamu wengine huwa ni matatizo ya hormons).

  Mama Mhagama, shambulia hawa wote. Na maadamu imeandikwa "achezae na upanga basi hufa na upanga", wapinzani wa Mhagama wameshapewa mfano wa jinsi ya kumkoma nyani. Kwani alikuwa wapi miaka yote nyuma? Na yeye atakomwa (na naombea akomwe) wakati wa uchaguzi. Hili joto likiwa kali, litatusaidia kujenga miiko ya viongozi kwani mtu ukimess up, wanakuondoa kwani utawapakazia wote.
  Hongera CHADEMA na hasa Dr. Slaa na Zitto kwa kuleta huu mchezo wa Mabomu ingawa muasisi wa mabomu ndugu Mzindakaya alirubuniwa ki-siasa na Mkapa na akapata kitu kidogo na sasa mabomu yake kayafiata kabisaaa. Shame on you Mzindakaya na Mafisadi wote waliokuingiza kwenye Mduara wao.
   
  Last edited: Jun 29, 2009
 20. Junius

  Junius JF-Expert Member

  #20
  Jun 29, 2009
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,183
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 133
  Mnataka Da Jenny alione bunge lijalo katika tiviii siyo?
   
Loading...