Hivi ujenzi wa jengo la abiria uwanja wa ndege wa Mwanza kuna nini?
Je, linakwamishwa na maslahi binafsi au kuna mkono wa mtu unazuia lisimaliziwa kwa viwango. Juzi Mkuu wa Mkoa Adam Malima amefoka sana kuhusu mikingamo ya ujenzi wa jengo hili.
Kwanini Serikali kuu isilichukue na kulimalizia ili lianze kutumika. Huu ni mwendelezo wa kukwamisha uwanja huu, Arusha airport mambo yanakwenda sawa, Songwe haina mikwara, Msalato haina shida nk. Hapa kuna nini.
Mara tunasikia TAA mara Halmashauri na mara Mkuu wa mkoa anataka ajenge. Ugomvi wa nini kungombea fito. Hiki ni kizungumkuti.
Tunaomba wananchi jengo liishe kwa viwango vya kimataifa litumike. Mhe. Rais batilisha uamuzi wa awali wa Rais aliyekuwepo wa kujenga jengo hilo muhimu kwa force account atafutwe mkandarasi asimamiwe vizuri uishe pamoja na marekebisho yake.
Vinginevyo lijengwe jipya lenye kiwango na hilo litumike kwa ndege ndogo charter flights au domestic flights