Jengo la gorofa la mtaa wa Indira ghandi lakamilika kubomolewa

Queen V

JF-Expert Member
Jan 19, 2012
775
1,332
JENGO la ghorofa 16 la mtaa wa Indira Ghandi lililokuwa likihatarisha maisha kutokana na kujengwa chini ya viwango.

Kufuaatia agizo la Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. William Lukuvi la kuvunja jengo hilo, jengo limekamilika kuvunjwa. Jengo hilo limevunjwa kufuatia pia kuanguka kwa jengo lingine lililokuwepo mita chache kutoka katika jengo hilo ambalo pia lilijengwa ghorofa 16 badala ya ghorofa nane. Jengo hilo liliporomoka na kusababisha vifo vya watu 34, mwaka 2013.

Hivi Karibuni Mhe. Lukuvi aliagiza kubomolewa kwa jengo hilo kufanyike ndani ya siku 90. Hatahivyo zoezi la ubomoaji limefanikiwa kukamilishwa kabla ya siku 50.

Mhe Waziri William Lukuvi akiwa na wataalamu katika ufuatiliaji wa ubomoaji wa Jengo la ghorofa 16 la mtaa wa Indira Ghandi.

Eneo palipokuwa na Jengo la ghorofa 16- Mtaa wa Indira Ghandi, baada ya kukamilika kwa ubomoaji.

Mhe. Waziri William Lukuvi akifuatilia ubomoaji wa jengo la mtaa wa Indira Ghandi ulivyokuwa ukiendelea .
 
Kiuhalisia hakuna jengo linalojengwa bila kuwa na consultant engineer.. hapo cha kujiuliza ni kwamba je kama alikuepo huyu mhandisi alikua hajui gorofa lili dizainiwa kuwa storey 8 badala ya 16????

Hapo kwa nnavyoona engineer alipewa kazi ya kuandaa michoro basi, lakini supervision haikua kwenye makubaliano yao!!! Mbaya zaidi mchoro wakapewa watu wasioelewa ndio shida kama hizo zinatokea!!!

Ni vyema wajenzi hasa ma injinia na contractors kufwata designs na sio kuongezea vitu ambavyo havipo kwenye design!!!

Zaidi ya yote, kampuni za ujenzi na wahandisi washauri wanaotambulika na ERB/CRB wakatumika na sio kuokota matechnician mtaani na kuwapa kazi zisizowahusu!!!

Ni wake up call kwa wahandisi kufwata taaluma zao na sio tamaa ya pesa!!

Pole aliyebomolewa mjengo wake!
 
JENGO la ghorofa 16 la mtaa wa Indira Ghandi lililokuwa likihatarisha maisha kutokana na kujengwa chini ya viwango.

Kufuaatia agizo la Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. William Lukuvi la kuvunja jengo hilo, jengo limekamilika kuvunjwa. Jengo hilo limevunjwa kufuatia pia kuanguka kwa jengo lingine lililokuwepo mita chache kutoka katika jengo hilo ambalo pia lilijengwa ghorofa 16 badala ya ghorofa nane. Jengo hilo liliporomoka na kusababisha vifo vya watu 34, mwaka 2013.

Hivi Karibuni Mhe. Lukuvi aliagiza kubomolewa kwa jengo hilo kufanyike ndani ya siku 90. Hatahivyo zoezi la ubomoaji limefanikiwa kukamilishwa kabla ya siku 50.

Mhe Waziri William Lukuvi akiwa na wataalamu katika ufuatiliaji wa ubomoaji wa Jengo la ghorofa 16 la mtaa wa Indira Ghandi.

Eneo palipokuwa na Jengo la ghorofa 16- Mtaa wa Indira Ghandi, baada ya kukamilika kwa ubomoaji.

Mhe. Waziri William Lukuvi akifuatilia ubomoaji wa jengo la mtaa wa Indira Ghandi ulivyokuwa ukiendelea .
Sawa haya,happy now???????????? limevunjwa,wewe tuonyeshe la kwako au la babaako au hata kakibanda ka kufugia kuku baaasi tuone au?
 
Jengo safi kabisa hilo. Nendeni Huruma mathare Kenya muone maajabu ya dunia. Mfuko m1 wa cement unajenga ghorofa 1. No wonder kila siku wanakufa kama kuku
Wacha utani bhana! Mfuko 1 ghorofa moja? Hiyo ni rekodi ya dunia!
 
Nakumbuka ilitolewa kauli na waziri wa Ardhi,mh.Lukuvi mwezi Janauary mwaka huu kuwa jengo moja liliko katikati ya Jiji(mtaa wa Indiraghandi) linatakiwa kuvunjwa kwa kujengwa chini ya kiwango ila mpaka leo naona kimya. Au limeshavunjwa? Kama bado,tatizo ni nini?

Naanza kukumbuka ya Naura springs pale jijini Arusha.
 
Kaka umekurupuka sana kuanzisha huu uzi...kwanza haupo specific kuhusu hilo jengo linalotakiwa kuvunjwa, maana yapo kadhaa kwa hapa mjini yenye kesi huko Mahakamani....Hivyo usipende tu kuanzisha uzi kama huna hoja zenye kukidhi hamu ya wasomaji. Toa taarifa za kutosheleza ili watu waelewe ni nini unataka kuwasilisha hapa.
 
Kaka umekurupuka sana kuanzisha huu uzi...kwa haupo specific kuhusu jengo linalotakiwa kuvunjwa, maana yapo kadhaa....Hivyo usipende tu kuanzisha uzi kama huna hoja zenye kukidhi hamu ya wasomaji.
Kumbe ni Hamy-D!!No wonder
 
Kaka umekurupuka sana kuanzisha huu uzi...kwanza haupo specific kuhusu hilo jengo linalotakiwa kuvunjwa, maana yapo kadhaa kwa hapa mjini yenye kesi huko Mahakamani....Hivyo usipende tu kuanzisha uzi kama huna hoja zenye kukidhi hamu ya wasomaji. Toa taarifa za kutosheleza ili watu waelewe ni nini unataka kuwasilisha hapa.
Soma nimerekebisha na ukumbuke waziri wa Ardhi alitoa mwezi mmoja kwa Manispaa ya Ilala na Shirika la Nyumba la Taifa kubomoa jengo hilo lililoko katika mtaa wa Indira Ghandi katika ya jiji.

Nakumbuka baadae ilikuja kuibuka issue ya mkandarasi wa kufanya hiyo kazi ila mpaka sasa naona kimya.
 
Back
Top Bottom