Jengo jipya la Wizara ya Mambo ya Nje

Jengo jipya la Wizara ya Mambo ya Nje

Killmonger

JF-Expert Member
Joined
Jan 11, 2015
Posts
2,027
Reaction score
2,252
Nimepita hapa mtaa wa Garden na Chimara lilipo jengo hili la wizara ya mambo ya nje hapa jijini Dar es Salaam. Kwakeli kwa mtizamo wangu ni jengo hasaa! Si mchezo! Lakini maraa .. nikakumbuka kwamba wizara zote zimehamishiwa Dodoma[emoji15]‍♂️ . Nikapigwa butwaa! Jengo hili litatumikaje[emoji15][emoji15].
 
Hakuna wa kulikodi, kwasababu ya economic depletion, sasa hivi nenda kwenye mabenki lile nyoni la folen hakuna, sio kuwa watu wanatumia electronic transactions bali watu wanamiliki vihela kiduchu.
Mkuu hili nalo nimeliona pale Bank karibu na nyumba ya mmakonde.. hakuna watu kabisa na kuna siku mtu alitaka kutoa kiasi flani cha hela akaambiwa hawana hiyo hela. Mambo sio mambo kwakweli.
 
Hili wazo la makao makuu kuwa Dodoma lilileta maana enzi za Ujamaa na duniani kukiwa na Cold War pia wakati ule lengo letu lilikuwa Africa iwe huru. Hiyo ilitufanya tuwe target ya maadui hasa makaburu. Dodoma kuwa mbali na bahari ilileta usalama.

Kwa sasa hivi wangezingatia maendeleo ya kanda. Kuchagua miji ambayo itafanywa makao makuu ya kanda ilendelezwe na kutoa ajira kwa vijana
 
Back
Top Bottom