gimmy's
JF-Expert Member
- Sep 22, 2011
- 3,305
- 3,327
Ujenzi wa nyumba mikoani gharama zake ni tofauti kabisa na Dar.Nimeona niandike huu uzi ili kuwatia moyo wengi wenye nia yakujenga lakini wanakatishwa tamaa humu kwakutajiwa gharama kubwa mno.
Kikubwa simamia ujenzi wa nyumba yako mwenyewe ili kulinda thamani ya pesa yako(value for money) kukwepa wizi.
Ushauri wa wana dar waliopatia maisha dar na kukosa experience za mikoani unaweza kukatisha tamaa,watakuja na mikwara ya makadirio ya square mitre hapo basi tu ili mradi mbwewe.Ila kimsingi thamani ya nyumba nyingi Dar sio thamani halisi ya nyumba hizo,huwa wanapigwa sana na mafundi.
Mtu anafanya kazi posta nyumba inajengwa mbezi ya kimara.Kutoroka kazini ni ngumu kwani hatawahi kwasababu ya foleni.Usimamizi ni weekend tu.Hapo unategemea nini!
Wanaishia kujisifia nyumba ya gharama kubwa wakati thamani iliyoongezeka haikuongeza thamani ya nyumba bali imeibwa.
Yapo maeneo tanzania hii udongo wake unaruhu kufyatua tofali zakuchoma lakini pia kujengea udongo huo huo unao patikana hapo hapo eneo la ujenzi.Cement hutumika kwenye kufunga mkanda wa chini,lenta na plasta tu lakini ujenzi mzima ukawa wa udongo ambo huchimbwa hapohapo kwenye kiwanja chako.
Aina hii ya nyumba ni imara na hazina shida yoyote na ikifanyiwa finishing hakuna atakae itambua.
Wapo watu hupanga mawe kwenye mashimo ya makaro ya maji taka ya vyoo kuanzia chini kasoro jamvi tu ndio hufunikwa kwa zege la kawaida lenye kusukwa nondo lakini ujenzi wa mawe hawatumii cement ujenzi huu ni imara na hupunguza gharama kubwa.
Tujitahidi kuokoa gharama chamsingi kuzingatia ubora tu hawa wana Dar es Salama waacheni na maisha yao.
Ila binafsi naamini kama mwana Dar atatumia 30m kujenga nyumba inawezekana kabisa wa mkoani akatumia 18m-20m kwa nyumba hio hio na baada ya finishing hakuna tofauti yoyote.