Jenga Greenhouse kwa gharama nafuu

Uzi huu upo karibia mwaka na miezi 4, bila shaka kuna waliojaribu na kufanikiwa, tunaomba feedback.

Nimemtembelea rafiki yangu mmoja aliyewekeza kwenye huu mradi, nimekuta anapanga kufyeka hicho kitalu ahesabu hasara. Anadai amefuata masharti ya utunzaji na mtaalamu mshauri wa kampuni ilyomjengea amekuwa anaemtemebelea kila wiki lakini bado matokeo sio kama alivyotegemea.

attachment.php
 

Attachments

  • 176.jpg
    176.jpg
    156.8 KB · Views: 1,982
GREEN HOUSE

Hebu piga hesabu vizuri 1/8 ya ekari ni 500mita za eneo sawa na 50m*10m au 25m*20m. sasa wewe unasema 8m*15m =120mita za eneo hii sio 1/8mkuu kwani ekari ina 4000mita za eneo rekebisha hapo. pia nisaidie tank la lita500 linamwagilia mda gan kwenye vipimo vyako vya 8*15 likiwa limejaa? pia 8*15 idadi ya miche ni mingapi?
 
Tembelea MASKANI | Horti Organics ukurasa wa maswali na majibu. Utapata kila kitu hapo.

Habari, Kwanza asante kwa mmarifa yaliyoko katika wavuti yenu. Ila nimejaribu kuwapigia simu kwa namba mlizoweka katika mtandao wenu ( +255 785 ... 821) anapokea mtu tofauti kabisa na hana hata akijuacho. Can you please update on the same. Ntashukuru sana kuweza ongea nanyi kwani ni mengi nahitaji toka kwenu na nimekua nikitafuta ujuzi huu hadi KENYA so itakua vyema nikapata consultants from where my Farms are.
 
Dah... Kwa mlioko Dar es salaam kwanini msipitie mikwambe kuangalia greenhouse yake ya mfano? Kuona ni bora kuliko kuambiwa...
 
Haya hii hapa green house yake ya mfano.... Hata picha zake alizoweka kama gh ya mfano inaonekana si za pale... Kwani green house hiyo na hii ziko tofauti. Chini ni kitalu . Nyumba iko na wapangaji
 

Attachments

  • 1436187064584.jpg
    1436187064584.jpg
    60.1 KB · Views: 420
  • 1436187090680.jpg
    1436187090680.jpg
    77.4 KB · Views: 377
  • 1436187111260.jpg
    1436187111260.jpg
    97.7 KB · Views: 390
  • 1436187131188.jpg
    1436187131188.jpg
    70.9 KB · Views: 398
GREEN HOUSE

Hebu piga hesabu vizuri 1/8 ya ekari ni 500mita za eneo sawa na 50m*10m au 25m*20m. sasa wewe unasema 8m*15m =120mita za eneo hii sio 1/8mkuu kwani ekari ina 4000mita za eneo rekebisha hapo. pia nisaidie tank la lita500 linamwagilia mda gan kwenye vipimo vyako vya 8*15 likiwa limejaa? pia 8*15 idadi ya miche ni mingapi?

Nmependa Umakini Wako Mkuu.
 
For Irrigation, Green Houses and associated material contact this man send msg on his whatsapp number +96898537738. He is
available here in TZ
 
GREEN HOUSE

Hebu piga hesabu vizuri 1/8 ya ekari ni 500mita za eneo sawa na 50m*10m au 25m*20m. sasa wewe unasema 8m*15m =120mita za eneo hii sio 1/8mkuu kwani ekari ina 4000mita za eneo rekebisha hapo. pia nisaidie tank la lita500 linamwagilia mda gan kwenye vipimo vyako vya 8*15 likiwa limejaa? pia 8*15 idadi ya miche ni mingapi?

Baba D,
1/8 of an acre niliyozungumza hapo sio 120 square meter ni ukubwa wa drip lines ambazo ningesupply katika material ya ujenzi wa Greenhouse ya 8*15, yaani yangetosha kumwagilia ndani ya gh na nje kwa mita za mraba zisizopungua 380. Hivyo kucover 1/8th of an acre. Nadhani umenielewa sasa.

Tank la lita 500 linamwagilia greenhouse ya 8*15 kwa saa moja (dk 60) hii itategemea na usafi wa maji. Kama maji ni masafi saa moja linamaliza tank na kama ni ya vumbi kama mto nk yatamwagiliwa kwa muda mrefu kudogo kwasababu ya filtration.
Idadi ya miche inategemea na aina ya zao. Kila zao na plant spacing yake, mf nyanya zinapandwa kwa umbali tofauti na pilipili mbuzi, hoho zinapandwa kwa umbali tofauti na matango au biringanya etc.
 
Uzi huu upo karibia mwaka na miezi 4, bila shaka kuna waliojaribu na kufanikiwa, tunaomba feedback.

Nimemtembelea rafiki yangu mmoja aliyewekeza kwenye huu mradi, nimekuta anapanga kufyeka hicho kitalu ahesabu hasara. Anadai amefuata masharti ya utunzaji na mtaalamu mshauri wa kampuni ilyomjengea amekuwa anaemtemebelea kila wiki lakini bado matokeo sio kama alivyotegemea.

attachment.php

Ni kweli kabisa kwamba kilimo cha greenhouse sio rahisi hata kidogo, nimeshasema kwenye huu uzi mara nyingi sana na kwenye TV pia, na wale wote waliokuja kuonana na mimi watashuhudia haya. Kama ukitembelea website yetu utaona majibu niliyotoa kuhusu urahisi na ugumu wa ukulima wa namna hii. Mshauri rafiki yako asifyeke hilo eneo, bali aangalie wapi alikosea kwa umakini na kuwa mkweli kwa nafsi yake. Isije kuwa anasema amefata masharti yote kumbe alikuwa anatoa maelezo kwa kijana wa shamba bila supervision halafu anaona kafata kila kitu. Pia aina ya zao, uchaguzi wa mbegu na kanuni zote huchangia kureflect ni matokeo yapi unapata. Greenhouse ni kama kitendea kazi na ndio mtaji ulipo, je ukijenga hoteli halaf watu wasije kula kwa miezi sita utaibomoa au utabadili mbinu ya kujitangaza na kuisimamia? Ameinvest kwenye jengo na si mazao, yakigoma mara ya kwanza ajipange upya alime mara ya pili na ya tatu mpaka pale atakapoweza na kuelewa hilo zao kikamilifu.
Ni makosa makubwa sana kuassociate gharama za ujenzi na mafanikio ya ukulima, mf unaposema nimeshatoa mil 6 halaf napata mazao ya laki3??? Unatakiwa ufikirie je hiyo m6 uliyotoa imefanyaje kazi mpaka umezalisha laki3? Angalia ulipokwama na ikiwezekana badili aina ya zao.

Ofcourse kuna makosa mengine si ya mkulima bali ni ya ujenzi mbaya uliyojawa na tamaa za kuwakandamiza watu ili mjenzi apate zaidi, kama gh yake ina urefu usiozidi mita tatu na upana wa ventilation ya juu ya paa hauzidi mita moja basi hilo ni tanuri na si shamba na hivyo kanuni za ujenzi hazikifatwa. Aangalie uwezekano wa kubadili baadhi ya material ili kurekebisha ujenzi.

Asilimia kubwa ya niliowajengea greenhouse walianguka na kukosa mazao katika msimu wa kwanza, baada ya kukaa nao chini na kuwaeleza makosa sasa hv almost wote wanazalisha vizuri sana. Kwa walio dar wanaweza kupita oysterbay nyuma ya donbosco kwenye kituo cha mbuyuni mtaa unaitwa Ali Bin Said nyumba ya kona kabisa, mkapate real farmers experiance ya greenhouse farming. Huyo mama hakuvuna hata kilo 20 za zao alilopanda katika msimu wa kwa za na sasa ndio the best producer wa hoho za njano na nyekundu kwa wote niliowajengea gh mwaka jana.

Samahanini kwa kutokuwa hewani muda mrefu, nilikuwa nje ya nchi kikazi na bado ntaendelea kuwa huko kwa muda japo mwezi huu nipo Dar,

Kwa anayehitaji kuwasiliana nami tagadhali apige namba 0714881500 au atembelee tovuti yangu www.hortiorganics.co.tz. Kwenye tovuti kuna kazi zetu nyingi sana tumeziweka zitajielezea sisi ni kampuni ya namna gani.

Kuna mdau hapo juu amehoji kwanini nimeondoka bila kuaga. Kwakweli haiwezekani kumuaga kila mtu. Wale waliofungiwa greenhouse nami wote wanajua nilipo na niliwaaga kwa kuendesha semina harbour view tower na kuwapa muongozo mzuri ambao sasa unawasaidia kuzalisha. Pia tuna group ya whatsapp ambayo chochote kinachoulizwa wakulima wote wanakiona na kuna mtaalamu anajibu maswali yote.

Wakulima wote nimewalink na kampuni kubwa sana ya mbegu ya kiholanzi wanaweza kusource kila kitu wenyewe na wanaweza kuzalisha au kuanzisha mashamba bila mimi kuwepo.

Kwa wale mtakaopata wasaa wa kwenda nane nane lindi tafadhali msikose kupita kwenye banda la JKT nimejenha greenhouse kubwa pale na kupanda matango, hiyo greenhouse ni mfano mzuri sana wa uzalishaji unaosimamiwa vema kwa kufata kanuni zote za ukulima kiweledi.

Mwisho kabisa napenda kusema kwamba, mkulima usiridhike na information au muongozo unaopewa na aliyekujengea gh tafadhali jiongeze kwa kusoma sana kwenye internet na hasa youtube njia mbali mbali za ukuzaji wa zao unalolima, tafuta vitabu nunua na usome uelewe nini unafanya. Kulima kwa kufata muongozo uliopewa una page 3 sio ukulima huo.

Kama kila kitu unafata sawa, na bado matokeo mabovu basi tatizo lipo kwenye dawa na mbolea unazotumia. Nchi yetu imejawa mbolea na dawa feki nyingi sana, hata mimi yalishanikuta. Hata kampuni kubwa kabisa za mbolea na dawa zinachakachua. Badili source uone kama matokeo yatajirudia.

Karibuni.
 
Kwa nini mkuu??kuna nn ndani yake?
kwanza mavuno yapo exaggrated na pili hakuna tofauti ya bei ya mazao ya hizo greenhouse na yaliyolimwa shambani. tatu greenhouse inatakiwa kuwa all weather hizi zetu haziwezi kuhimili baridi kali.
 
kwanza mavuno yapo exaggrated na pili hakuna tofauti ya bei ya mazao ya hizo greenhouse na yaliyolimwa shambani. tatu greenhouse inatakiwa kuwa all weather hizi zetu haziwezi kuhimili baridi kali.

Call my friend Mr. Kindi for all weather EU standard Green Houses and Chicken houses
 

Similar Discussions

61 Reactions
Reply
Back
Top Bottom