Jenga Greenhouse kwa gharama nafuu

Kipaji halisi, soma post zote utapata majibu. Watu washauliza sana hayo na majibu yako humuhumu, sasa hivi tunataka watu waliokwishaanza project watupe mlejesho.
 
Unajua hii ni fursa nzuri kwetu sisi vijana tunaoanza maisha ila nina maswali kidogo
1. Kwa sisi tuliozaliwa mjini kilimo kidogo kilitupitia kando has hii horticulture je mnatoa mwongozoa au mafunzo yeyote
2. Je jumla ya gharama zote ni kiasi gani maana hapo sijaelewa. namaanisha mtu anahitajika awe na mtaji kiasi gani mpaka hiyo greenhouse iwe tayari imeanza kazi. mchanganuo mfupi
3. Je inahitaji umeme maana huku tuliko wengine umeme ni changamoto
4. Ofisi zenu ziko wapi?

Nimevutiwa sana na natamani kuanza hii project mara moja fursa huwa hazicheleweshwi.
 
Huwa nasikiaga tu kuhusu hiki kilimo cha Kwenda juu,angani. Ila leo nimepata kujua vizuri. Am interesting subiri nijipange nikutafute tufanye business mungu akijalia uzima,afya na rehema.
 
NAI SAVE NAMBA YAKO NA NTAKUPIGIA MWEZI WA NNE,kenya naona hata ufugaji wa samaki wanafanya kwenye greenhouses,samaki wanakuwa under controlled environment,ningependa nijue kama una access na watu wanaouza pond liners,nina bwawa la samaki la mita 20/30 nisingependa kulijengea,

Nitumie mchanganuo wa gharama please nimevutiwa na hii project:firstsaby@yahoo.com
 
aksante sana, hii kitu nimeipenda sana, itatutoa haswa watu waache kunywa kahawa vijiweni wakatumike tuinue uchumi wetu
 
Huyu jamaa kashapata wateja sasa anaringa kujibu sisi wateja wapya.kama kawaida yetu sisi wabongo kastama kea tanzania ni janga la taifa
 
Ni kweli hiki kilimo cha greenhouse kina tija nzuri sana. Kuna mdada mmoja ameacha taaluma yake ya uanasheria sasa anajishughulisha na hiki kilimo.
 
Ujenzi wa Banda la mfano umeshakamilika? Nataka nije nijionee kwanza kabla ya maamuzi. Na kwa kuwa ulisema unaiset kigamboni ni manufaa kwangu kwani nami nataka nianze mradi wangu hapo hapo kigamboni..
 
Huyu jamaa kashapata wateja sasa anaringa kujibu sisi wateja wapya.kama kawaida yetu sisi wabongo kastama kea tanzania ni janga la taifa

Jamaa nahisi kasitisha hii biashara, maana juzi kati alikua anauza vifaa vyake vya ndani, kesho yake akawa anapangisha Nyumba yake yenye GH ya mfano kule Mwikwambe, Kigamboni!!

Hizi ni dalili kua hatokuwepo nchini hivi karibuni
 
Jamaa nahisi kasitisha hii biashara, maana juzi kati alikua anauza vifaa vyake vya ndani, kesho yake akawa anapangisha Nyumba yake yenye GH ya mfano kule Mwikwambe, Kigamboni!!

Hizi ni dalili kua hatokuwepo nchini hivi karibuni

Imekuwaje tena. Biashara imekuwa ngumu? Angefanya ustaarabu wa kuaga kuliko kufanya kama kukimbia.
 
wadau, ningepata muwekezaj wa maana tungefanya hii biashara, nina shamba la ekari 30 liko karibu na ziwa victoria, tunaweza kulima nyanya na kulisha viwanda vya kusindika nyanya kenya, ukishakuwa na uhakika wa kuzalisha soko ni la uhakika!
 
Kipaji halisi, soma post zote utapata majibu. Watu washauliza sana hayo na majibu yako humuhumu, sasa hivi tunataka watu waliokwishaanza project watupe mlejesho.

Sio lazoma kusoma post zote, acha mwenye mada ajibu
 
Jamaa nahisi kasitisha hii biashara, maana juzi kati alikua anauza vifaa vyake vya ndani, kesho yake akawa anapangisha Nyumba yake yenye GH ya mfano kule Mwikwambe, Kigamboni!!

Hizi ni dalili kua hatokuwepo nchini hivi karibuni

Hata kama hayupo nchini si JF anaingia popote, basi tu siajabu anatuchora tu humu JF. Jamani kuna waliofanikiwa katika hili? tupeni mwongozo. Maana huyu jamaa katuacha njia panda
 
Hata kama hayupo nchini si JF anaingia popote, basi tu siajabu anatuchora tu humu JF. Jamani kuna waliofanikiwa katika hili? tupeni mwongozo. Maana huyu jamaa katuacha njia panda


Ukiona manyoya.......
 
Nauza Materials na kusadia ujenzi wa Greenhouse za ukubwa mbali mbali.

Kwa sasa Nina materials zinazoweza kucover greenhouse ya ukubwa wa mita nane kwa mita kumi na tano (8x15m), Zina uwezo wa kuzuia jua, kuzuia wadudu na vihatarishi mbali mbali vya mazao.

Bei ni Mil2.5 kwa materials pekeyake yaani 1/8 of an ancre drip lines, Polythene Cover (UV400 Protected sheets), 70% Micron insect Netting...Hizi zitakuwezesha kujenga Greenhouse yako bila matatizo. Kitakachohitajika kutoka kwako ni Wooden Poles (nguzo kama zinazojengewa baa za makuti nk), tanki la lita 500 la maji na maji ya uhakika.

Ntakupatia mafundi na muongozo mzima wa kujenga greehouse yako ili kufanikiwa.

Faida za kulima katika greenhouse ni nyingi mno, ikiwemo matumizi mazuri na sahihi ya ardhi, kwani kiwanja cha ukubwa wa mita 8x15 kinaweza kukupa Nyanya hadi Tani 10 kwa mwaka, Pilipili hoho tani 8 kwa mwaka na mazao mengine mengi yanayolimwa katika controlled environment.

Kuna wataalamu wa kutosha hivi sasa hapa Dar Es Salaam wanaoweza kukupa muongozo, mbegu bora na fertilizers za uhakika.. Tuwasiliane kwa simu namba 0714881500 ili kupeana muongozo.

Karibuni sana.
Ili uweze kufanikiwa katika kilimo hiki, unahitaji maji ya uhakika minimum lita 200 kwa siku kwa ajili ya kumwagilia nyanya kwa matone, Nitakupatia mabomba (driplines) zitakazokuwezesha kufanikisha hili.

NB: Kumbuka Greenhouse inajengwa kwenye eneo lililo wazi, lisilo na miti mirefu inayozuia jua...

Pia ni Muhimu kufanya Soil Test na Water Test ili ujue ni kipi unahitaji kuongeza kwenye ardhi yako ili upate mazao ya uhakika... Naweza kukusaidia kufanya soil na water test kwa gharama nafuu kabisa kutoka nchi ya Jirani (kenya). Gharama ni 250,000 kwa huduma hii pekeyake (Complete Soil analysis & Water Test).

NB::: UJENZI WA GREENHOUSE YA MFANO UMEKAMILIKA. IPO MIKWAMBE KIGAMBONI::: KARIBUNI SANA.

View attachment 140539 View attachment 140540 View attachment 140541 View attachment 140542 View attachment 140543 View attachment 140547

Kuna watu wengi sana wamenipigia na kuomba niwasaidie kufanya mchakato wa kuandika mchanganuo wa kuomba mkopo bank (bankable business plans and proposals) au taasisi za fedha ili wafanikishe mradi huu.

Habari njema ni kwamba, tumeingia makubaliano maalumu na kampuni moja hapa nchini (Biznocrats consulting enterprise) inayojihusisha na kuandika michanganuo ya kibiashara, ushauri wa kifedha, accounts nk na wamekubali kuwaandikia wateja wetu wote michanganuo hiyo kwa gharama ya asilimia moja tu (1%) ya mkopo Minimum 500,000 na wanakuhakikishia hautokosa mkopo wa aina yoyote.

Kama unahitaji huduma hii, tuwasiliane ili tuweze kufanikisha hili pamoja.

Karibuni sana.

Kaka na mimi naomba unitumie mchanganuo wa vifaa na gharama zake, naimani tutafanya kazi pamoja. Email yangu ni max.revocatus@yahoo.com
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom