Jenereta Laua 4 Zenji

Bujibuji Simba Nyamaume

JF-Expert Member
Feb 4, 2009
74,871
155,834
WATU wanne wa familia moja wamekufa baada ya jenereta lililokuwa limefungiwa ndani ya nyumba hiyo kupasuka na kuwaka moto.

Tukio hilo limetokea usiku wa kuamka leo, Kibwenzini Zanzibar wakati familia hiyo ikiwa bao imelala.

Akizungumza na gazeti hili kwa masikitiko baadhi ya majirani wamedai kuwa familia hiyo isingeteketea kwa maoto kama suala la umeme lingepatiwa ufumbuzi muda mrefu.

"Tumesikitishwa na vifo vya hawa ndugu zetu kwani kama Serikali ingelitafutia ufumbuzi suala la umeme muda mrefu wasingeteketea, " amesema jirani mmoja aliyejitambulisha kwa jina Yahyaa Juma Salehe mkazi wa Kibwenzini.

Amedai kuwa kutokana na kutokuwepo kwa umeme muda mrefu baadhi ya wakazi wenye uwezo wamenunua majenera ili kuweza kukabiliana na kero ya umeme.

Amedai kutokana na hali hiyo kumekuwepo na kero ya kelele mitaani huku wamiliki wa majenereta hayo wakiweka ulinzi ili kuhakikisha kuwa hayaibiwi.

Amedai kuwa familia hiyo ilinunua jenera hiyo kutokana na kero hiyo ambalo lilikuwa linafanyakazi likiwa ndani kila siku.

Amedai kuwa ilipofika sa 11 alfajiri wakati familia hiyo ikiwa bado wamelala ghafla jenereta hilo lililipuka na kuwaka moto.

Amedai kutokana na kitendo hicho moshi na moto ulizagaa nyumba anzima ambapo milango na madirisha vilikuwa vimefungwa hali iliyopeleka familia hiyo kushindwa kutoka na kufia ndani ya nyumba.

Amedai kuwa waliokufa katika ajali hiyo ni Safia Shabani, Ahmed Shabani, na mtoto ambaye hakuweza kupatikana jina lake akiwemo msichana wa kazi Sikudhani Nasorro.

Juhudi za gazeti hili kumpata kamanda ili kuzungumzia zaidi kuhusiana na tukio hilo haikuweza kuzaaa matunda kutokana na simu yake ya mkononi kutopatikana.
 
Mungu aziweke roho za marehemu MAHALA PEMA PEPONI
Aidha.... Mtaa unaitwa Kibweni sio KIBWENZINI
 
Back
Top Bottom