Jenerali Ulimwengu: Staili za 'zimamoto' na ziara za kushtukiza haziendeshi serikali...

The Boss

JF-Expert Member
Aug 18, 2009
49,226
116,839
Naona Jenerali hapa kaandika katika ubora wake...
bila kupindishapindisha........

NIMEANDIKA huko nyuma kwamba iwapo tunataka kufanya mabadiliko ya kweli katika jinsi tunavyoendesha mambo yetu hatuna budi kuyawekea mifumo na mipangilio ya kuyafanya hayo mabadiliko. Aidha nimeandika kwamba ili kutimiza hilo hatuna budi kwanza kuanza na katiba mpya ambayo itatuwezesha kutunga sheria, taratibu na kanuni mwafaka zitakazosimamia utekelezaji wa vipengele vya katiba hiyo.
Jinsi alivyoanza Rais Magufuli aliwatia matumaini watu wengi humu nchini na hata nje ya nchi wanaoitakia mema nchi yetu. Hatua alizochukua katika maeneo muhimu yanayohusiana na ukusanyaji wa mapato ziliwatia moyo watu wengi, na walimuunga mkono.
Alichofanya Magufuli na timu yake ya watu wachache kabisa kabla ya kutangaza timu nzima ya baraza la mawaziri ilikuwa ni tiba ya mshituko (?shock therapy?) kuwaamsha watendaji wa serikali waliokuwa wamelala usingizi wa pono kwa muda mrefu chini ya Rais Jakaya Kikwete.
Ukali aliouonyesha Magufuli na waziri mkuu wake uliwafanya Watanzania na majirani zetu kuanza kusema kwamba mabadiliko sasa yanaweza yakatokea hapa nchini. Alivyotumia muda mrefu kuliko kawaida kuteua mawaziri wake, hisia za wengi zilidhani kwamba alikuwa anafanya uchambuzi na uchunguzi yakinifu ili asije akafanya makosa ya kuwarudisha mawaziri ambao walikuwa wamekwisha kudhihirisha kwamba ni mizigo katika serikali iliyopita.
Alipokuja kulitaja baraza lake, ukweli ninaouzungumzia ukajitokeza mara moja, nao ni kwamba kitakacholeta mabadiliko si hamasa na nishati binafsi ya mtu mmoja au watu wawili, bali ni kazi ya mfumo ambamo timu itafanya kazi kama timu yenye lengo moja linaloiunganisha.
Baraza la mawaziri aliloliteua halionyeshi kwamba kuna jambo kubwa litakalobadilishwa kupitia baraza hilo. Kwanza amewarudisha watu ambao tayari wanabeba shutuma za kufanya vibaya kutoka baraza lililopita, ama kwa utendaji mbovu ama kwa kushutumiwa kwa utovu wa uadilifu. Kuwarejesha katika baraza linaloitwa jipya ni kujipunguzia nguvu aliyoanza nayo Magufuli kabla hajawa na baraza.
Aidha, inaelekea mawaziri walioteuliwa walikuwa wamedurusu bosi wao mpya na kubaini kwamba staili yake pamoja na waziri mkuu wake ni kwenda kwenye maeneo yenye matatizo na kutoa maelekezo ya papo kwa hapo, na baadhi yao wakaanza kuiga staili hiyo. Hili ni tatizo litakalokuja kutusumbua huko tuendako.
Niliwahi kusema mara kadhaa kwamba mojawapo ya matatizo yetu ni watu kufanya kazi za watu wengine na kuacha kazi zao. Rais anafanya kazi ya waziri, waziri anafanya kazi ya katibu mkuu, katibu mkuu anafanya kazi ya kamishna na kamishna anafanya kazi ya ofisa wa chini. Wakati mwingine, waziri wa wizara X anafanya kazi ya wizara Y na waziri wa wizara Y anafanya kazi ya wizara Z. Dalili hizi tutazidi kuzishuhudia chini ya baraza hili kama hatua hazikuchukuliwa kuwaelekeza mawaziri kuhusu kazi zao.
Katika hali ninayoijadili hapa, tunapata mfano wa Katibu Mkuu Kiongozi, Ombeni Sefue, aliyeonekana akikimbizana na vitanda kwenda Hospitali ya Muhimbili kwa sababu rais katoa maagizo vitanda vipelekwe huko. Mimi nilijiuliza, hata kama ni rais kaagiza hilo lifanyike, ni kwa nini ofisa wa wizara husika asilitekeleze badala ya mkuu wa utumishi nchini?
Inabidi tukumbushane. Isipokuwa kama kuna maelekezo mbadala, kazi ya waziri ni usimamizi wa sera za serikali wizarani kwake, kusimamia utekelezaji wa maamuzi ya serikali yanayotokana na ilani ya uchaguzi wa chama chake. Hata hivyo, tunashuhudia mawaziri wakitoa maelekezo kwa watumishi wa ngazi za kati na ngazi za chini, ambao kiutaratibu wako chini ya katibu mkuu.
Katibu mkuu ndiye mtawala wa rasilimali-watu, fedha na vifaa ndani ya wizara. Yeye ndiye anapaswa kusimamia utendaji, nidhamu na uwajibikaji wa maofisa wote wa wizara, na yeye ndiye mwenye uwezo wa kusimamia nidhamu yao, upandishwaji vyeo na hata kuwafuta kazi.
Pia yeye ndiye mlipaji mkuu wa wizara kwa kuwa ndiye mshika kasma mkuu wa wizara. Vile vile, ni katibu mkuu anayewajibika kufanya manunuzi ya vifaa vinavyotumika wizarani (magari, samani, mashine nk.) na kusimamia matumizi yake.
Ofisa anayehusika na taaluma katika wizara si mmoja wa hawa wawili hapo juu. Mtu wa taaluma ni kamishna au kurugenzi, kutegemea wizara husika. Katika wizara inayoshughulikia afya atakuwa ni mganga mkuu wa serikali; katika wizara inayohusu elimu atakuwa kamishna wa elimu, na katika wizara nyingine kuna makamishna na wakurugenzi wanaohusika na utaalamu wa wizara zao.
Lakini katika mvurugano tulioukubali ukajijenga katika serikali yetu, tunawaona mawaziri wakitoa maelekezo kuhusu utawala, na makatibu wakuu wakitoa maelekezo ya kitaaluma. Wakati mwingine, mawaziri na makatibu wakuu wanatoa maelekezo ya kitaaluma kwa sababu tu zamani waliwahi kuwa watumishi katika fani hiyo au ni fani waliyoisomea.
Hata kama mhusika ni daktari kwa taaluma, wizarani hatakiwi kufanya kazi ya taaluma kwa sababu mwenye taaluma yupo, na waziri ni mkuu wa siasa wizarani pale. Pia, hata kama katibu mkuu ana shahada za uhandisi, katika wizara ya ujenzi hawi mtaalamu wa uhandisi bali mtawala wa rasilimali-watu, fedha na vitendea-kazi. Hili lisipoheshimiwa, kila siku kunakuwa na migongano kati ya mawaziri, makatibu wakuu na wanataaluma wa wizara.
Katika hayo yote, ambayo tayari ni magumu, tunaongeza utamaduni wa kutaka kuonekana tunatoa maelekezo na kuwapangia maofisa walete majibu mnamo siku saba au mnamo wiki mbili. Aidha wakubwa wanapenda sana kutoa maelekezo na maagizo hayo mbele ya kamera za televisheni, ili watu wamuone kwamba ?anachapa kazi?. Huu ni upuuzi mtupu, na ni tabia ya kujipatia umaarufu wa bei nafuu kwa watu wasiojua serikali hufanya kazi kwa njia gani.
Kazi ya serikali na maamuzi yote ya serikali ni budi yatiwe katika maandishi, la sivyo ni hewa tupu. Kusubiri kamera za televisheni kabla ya kuanza ?kuchapa kazi? ni upuuzi ambao umedumu kwa muda mrefu sasa, na hauna budi kukomeshwa. Iwapo mawaziri wa Magufuli watafanya kazi kwa staili hiyo, lazima tujue kwamba hakuna jambo la maana wataloweza kulifanya.
Tumekuwa na wakuu waliokuwa wakitoa amri na watu wanatetemeka. Leo najiuliza amri hizo ambazo tuliambiwa kwamba zimetekelezwa wakati ule, zimeishia wapi na ni kwa nini hatuoni dalili zake? Najua kwamba kutoa amri za papo kwa hapo huibua shangwe ya wananchi ambao wanaona kama vile wamepata mkombozi dhidi ya mifumo inayowakandamiza na kuwanyima haki zao. Lakini hiyo si dawa. Dawa mujarrab ni kuweka misingi inayoeleweka na kutabirika, na kujenga mifumo imara na inayoaminika ya utekelezaji na utoaji wa taarifa.
Iwapo kuna tatizo Ilala au Kinondoni na waziri anakimbia kwenda ?saiti? kutoa maagizo, je linapokuwa tatizo kama hilo hilo limejitokeza Bukoba au Sumbawanga, au Masasi, au Ulanga, anafanyaje? Hawa si mawaziri wa Dar es Salaam, kama nimeelewa vyema, ni mawaziri wa nchi nzima. Kote nchini, ikiwa ni pamoja na Ilala na Kinondoni kuna wakuu wa mikoa na wakuu wa wilaya, kama wale wa Bukoba, Sumbawanga, Masasi na Ulanga. Kwa nini hawatumiki?
Katika mambo ninayoyajua kwamba yanatukwamisha na yataendelea kutukwamisha hata kama Magufuli atatoa amri 100 kila siku, ni ubovu wa taarifa za utekelezaji zinazofuatia maelekezo yaliyotolewa na wakubwa kuelekea ngazi za chini. Binafsi kutokana na uzoefu mdogo nilio nao katika utendaji nchini hapa, siamini kwamba zaidi ya asilimia 30 ya taarifa za utekelezaji wa mipango ya serikali ni za ukweli.
Nyingi miongoni mwa taarifa hizo ni za kubuni na kutunga, na maofisa wa ngazi mbalimbali wamejenga uwezo mkubwa wa kuandika taarifa zilizosheheni takwimu za mafanikio ya utekelezaji, majina ya vijiji na tarehe za kuanza kwa mradi na idadi ya watu walionufaishwa na mradi au programu bila hata siku moja kukanyaga katika sehemu inayotajwa. Ni uongo mtupu.
Nimekwisha kuzungumzia umuhimu wa katiba mpya, na sichoki kulijadili hili, kwa sababu ni la umuhimu mkubwa kuliko jambo lolote jingine. Katiba ndiyo inaweza kutuelekeza ni namna gani iliyo bora ya kuiendesha nchi yetu, kuwapa wote wanaohusika majukumu mahsusi ya kutekeleza na kuainisha mifumo ya utawala.
Itaendelea - See more at: Raia Mwema - Staili za ‘zimamoto’ na ziara za kushitukiza haziendeshi serikali
 
Nakusaport kwa katiba mpya.lkn kuusu balaza la mawaziri umebugi tena c kidogo yaani ni sana maake mwenyewe kawa bungeni miaka20 xo anafaham michezo vizuri na wasafi na wachafu anawajua.xo kuliko kuponda bora uendelee kuhubiri kuhusu katiba mpya maake ndo la maana
 
Hawa kina mzee ulimwengu kasuku tu kama watajua zaidi si watafute nafasi za uongozi ili watumikie taifa hata kwa ushauri
 
This is a serious probleam. Nimeliona hili toka utendaji wa Mrema nadhani Watanzania wengi wanapenda hivi. Rais anafanya kazi ya waziri, waziri anafanya kazi ya katibu mkuu, katibu mkuu anafanya kazi ya kamishna na kamishna anafanya kazi ya ofisa wa chini. Wakati mwingine, waziri wa wizara X anafanya kazi ya wizara Y na waziri wa wizara Y anafanya kazi ya wizara Z. Dalili hizi tutazidi kuzishuhudia chini ya baraza hili kama hatua hazikuchukuliwa kuwaelekeza mawaziri kuhusu kazi zao.
 
Hawa kina mzee ulimwengu kasuku tu kama watajua zaidi si watafute nafasi za uongozi ili watumikie taifa hata kwa ushauri

Nyerere aliwahi kutusimulia methali ya Wachina
inasema 'mimi sio kuku lakini yai viza nalijua'

Sio lazima mtu aweze kuongoza ndo aweze kukosoa

wewe ukiliona yai viza unajua tu hili ni yai viza...
ingawa wewe sio kuku
 
Jenerali anasema:

Niliwahi kusema mara kadhaa kwamba mojawapo ya matatizo yetu ni watu kufanya kazi za watu wengine na kuacha kazi zao. Rais anafanya kazi ya waziri, waziri anafanya kazi ya katibu mkuu, katibu mkuu anafanya kazi ya kamishna na kamishna anafanya kazi ya ofisa wa chini. Wakati mwingine, waziri wa wizara X anafanya kazi ya wizara Y na waziri wa wizara Y anafanya kazi ya wizara Z. Dalili hizi tutazidi kuzishuhudia chini ya baraza hili kama hatua hazikuchukuliwa kuwaelekeza mawaziri kuhusu kazi zao.

Katika hali ninayoijadili hapa, tunapata mfano wa Katibu Mkuu Kiongozi, Ombeni Sefue, aliyeonekana akikimbizana na vitanda kwenda Hospitali ya Muhimbili kwa sababu rais katoa maagizo vitanda vipelekwe huko. Mimi nilijiuliza, hata kama ni rais kaagiza hilo lifanyike, ni kwa nini ofisa wa wizara husika asilitekeleze badala ya mkuu wa utumishi nchini?

Halafu anamalizia:

Iwapo kuna tatizo Ilala au Kinondoni na waziri anakimbia kwenda ?saiti? kutoa maagizo, je linapokuwa tatizo kama hilo hilo limejitokeza Bukoba au Sumbawanga, au Masasi, au Ulanga, anafanyaje? Hawa si mawaziri wa Dar es Salaam, kama nimeelewa vyema, ni mawaziri wa nchi nzima. Kote nchini, ikiwa ni pamoja na Ilala na Kinondoni kuna wakuu wa mikoa na wakuu wa wilaya, kama wale wa Bukoba, Sumbawanga, Masasi na Ulanga. Kwa nini hawatumiki?
 
The Boss
Taratibu tu, watatuelewa na hakika baadhi wanatuelewa. Wapiga debe wamegoma, ipo siku watasitisha mgomo na kuungana nasi kutafuta majibu ya kudumu na si shamra shamra. Tumelizungumzia sana hili tukaulizwa, wimbo wa mfumo ni kitu gani?

Tumesema sana, Mwinyi alikuja na staili yake, je imedumu? Mkapa akaja na yake je imedumu? JK kaja na zake zilizofeli kabla ya kuanza, hatuzijadili maana Magufuli anatuonyesha ubovu kwa kina

Leo tunasikia Polisi wanachunguza vifo vya watu wawili kwasababu 'hapa kazi'
Huko nyuma Polisi hawa hawa hawakufanya lolote kwa mambo kama haya, nguvu imetoka wapi na kwanini haikuwepo

Tunasikia mamlaka ya mapato inakusanya Trilioni 1.3, miezi miwili ilikusanya chini ya hapo.
Bila kuwa na ongezeko la vyanzo vya mapato, hali imebadilika. Je, tatizo ni nini kama si mfumo?

Tunasikia majipu, leo fulani kaondolewa na bodi kuvunjwa. Nani aliweka watu hao katika nafasi zilizoletea taifa hasara?

Je, tumeangalia kwanini tuna bodi hovyo, wakurugenzi 'sub standard"?

Nani anawateua na je tume fix tatizo la upatikanaji wa vyombo hivyo?

Nani watch dog wa hawa ? Tunasubiri Magufuli mwingine aje kutumbua majipu yatakayojitokeza siku za mbeleni?

Kama hatutakaa chini na kutafuta chanzo, na suluhu, hizi shangwe ni za miezi michache.

Zitashindwa, na kufeli hakuepukiki. Tatizo si dhamira bali njia za kutimiza dhamira hazipo kama si mbovu

Watatuelewa, taratibu tu!
 
The Boss
Taratibu tu, watatuelewa na hakika baadhi wanatuelewa. Wapiga debe wamegoma, ipo siku watasitisha mgomo na kuungana nasi kutafuta majibu ya kudumu na si shamra shamra. Tumelizungumzia sana hili tukaulizwa, wimbo wa mfumo ni kitu gani?

Tumesema sana, Mwinyi alikuja na staili yake, je imedumu? Mkapa akaja na yake je imedumu? JK kaja na zake zilizofeli kabla ya kuanza, hatuzijadili maana Magufuli anatuonyesha ubovu kwa kina

Leo tunasikia Polisi wanachunguza vifo vya watu wawili kwasababu 'hapa kazi' Huko nyuma Polisi hawa hawa hawakufanya lolote kuhusu kifo cha Mwangosi.

Tunasikia mamlaka ya mapato inakusanya Trilioni 1.3, miezi miwili ilikusanya chini ya hapo. Bila kuwa na ongezeko la vyanzo vya mapato, hali imebadilika. Je, tatizo ni nini kama si mfumo?

Tunasikia majipu, leo fulani kaondolewa na bodi kuvunjwa. Nani aliweka watu hao katika nafasi zilizoletea taifa hasara?
Je, tumeangalia kwanini tuna bodi hovyo, wakurugenzi 'sub standard"? Nani anawateua na je tume fix tatizo la upatikanaji wa vyombo hivyo? Nani watch dog wa hawa ? Tunasubiri Magufuli mwingine aje kutumbua majipu yatakayojitokeza siku za mbeleni?

Kama hatutakaa chini na kutafuta chanzo, na suluhu, hizi shangwe ni za miezi michache.
Zitahindwa na kufeli hakuepukiki. Tatizo si dhamira bali njia za kutimiza dhamira hazipo kama si mbovu

Watatuelewa, taratibu tu!

Mkuu Nguruvi3 .....niliwahi kusoma sehemu kuwa samaki

ana memory span ya dakika 3......kwa hiyo ndo maana unarusha ndoano
pale pale na unawavua tu....kila baada ya dakika tatu wanasahau kuna mtu kaja kutuvua...

Inawezekana na sisi Watanzania memory span ya baadhi ya wenzetu ni miaka 10 au mitano

maanake hawataki kabisa kukumbuka kuwa hata JK tu alifanya ziara za kushtukiza Muhimbili
ni kama kila anachofanya Magufuli ni kiipya kabisa.....
 
Last edited by a moderator:
Huyu mzee alishawahi kuwa kiongozi wa ngazi ya juu kisiasa hapa nchini. Sijui kipindi hicho alikuwa anatumia staili gani ya uongozi? Kocha anaona kikosi chake ni kizuri. Sasa mtazamaji au shabiki unataka kumpangia kocha wachezaji gani waingie uwanjani na formation gani wacheze?
 
Back
Top Bottom