maramia
JF-Expert Member
- Jul 17, 2015
- 2,030
- 1,345
Kati ya miaka ya 70 na 80 nikiwa shule nilifikiri Ulimwengu ni ofisa wa jeshi mwenye cheo cha jenerali na kwamba alikuwa ndiye kamanda wa majeshi yote ya dunia (ulimwengu) kwa namna alivyokuwa shupavu na jasiri asiye na woga.
Baadaye wakati wa utawala wa mwalimu nikamsoma katika gazeti moja kati ya Uhuru au Mzalendo kwamba alikuwa amejiuzulu ukuu wa wilaya (nafikiri ilikuwa moja ya wilaya za mkoa wa Singida) nilishangaa sana, miaka ile mtu kujiuzulu ukuu wa wilaya? Kabla na baada ya pale hapajapata kutokea tangu uhuru mkuu wa wilaya akajiuzulu nafasi hiyo.
Kwa maelezo ya gazeti lile Ulimwengu hakuwa amejiuzulu kwa kuwajibika au kwa kutenda makosa ila kwa kutokubaliana na baadhi ya maamzi ya serikali au ya mwalimu kuhusu mambo fulani fulani ya uendeshaji wa nchi wakati huo akiwa ni kada kindaki ndaki wa chama cha TANU.
Wakati wa kampeni za Mkapa kugombea urais Ulimwengu na gazeti lake la Rai alikuwa upande wa Mkapa akimuunga mkono aingie ikulu kwa kila hali na akafanikiwa. Cha ajabu baada ya muda mfupi, bila shaka baada ya kugundua kuwa Mkapa hakuwa msafi kama tulivyoaminishwa na mwalimu alimgeuka na kuanza kuishambulia serikali yake hadharani.
Mkapa naye kwa kutaka kumwonyesha mamlaka alimtangaza Ulimwengu kwamba hakuwa mtanzania halali, hali iliyosababisha Ulimwengu kutangazwa kutotakiwa nchini, na bila jitihada zake binafsi leo hii Ulimwengu angekuwa huko kwa Rais Kabila kwa Wanyamulenge.
Jana kwenye mdahalo wa kigoda cha Mwalimu, Ulimwengu bila kulemba maneno alimpasulia Kikwete kwamba anastahili kushtakiwa aeleze ni kwa nini alikwamisha kwa makusudi mchakato wa katiba mpya huku akiwa ametumia mamilioni ya kodi ya watanzania kuichakata.
Namuunga na naomba watanzania tusimame kidete kupigia kelele upatikanaji wa katiba mpya na hata kuhakikisha wale wote (wakiongozwa na Kikwete) waliokwamisha mchakato ule kwa makusudi wanaburuzwa mahakamani.