Jenerali Ulimwengu asema Dr Slaa ndiye rais mtarajiwa

Jenerali Ulimwengu asema Dr Slaa ndiye rais mtarajiwa

Tunaka agombee kwa ajili ya nani? Haya maneno ukienda nayo mbele ya wana CUF hakika CUF wanajitoa siku hiyo hiyo, hii ni dharau kubwa , hata mimi sijaipenda.

Endelea kutopenda lkn ndo uhalisia huo
Kama hujaelewa explanation chini yake naamini hata uelewa vp huwez elewa probably u r just already biased!
 
CHADEMA iliyokuwepo 2011 ni tofauti na iliyopo sasa, na hata image ya Slaa wakati huo ni tofauti na sasa. Kwa wakati ule hata mimi nolikuwa na mawazo kama ya Jenerali, lakini katikati hapo CHADEMA wamefanya maamuzi kadhaa yasiyo na busara kiasi kwamba nina-doubt kama kweli wana uwezo wa kusimamia haki, demokrasia ya kweli na uchumi imara tunaoutaka.
 
Ndugu yangu TataMadabida, umepotoka. Unaposema wanachama wa CUF wakikusikia, una maana kuwa kwa kuwa Prof. Ibrahimu Lipumba ni CUF, basi unadhani watakaochukia kwa kauli ile ni wanachama wa CUF. Urais siyo wa CUF ni wa watanzania wote. Lpumba hagombei urais wa CUF anagombea urais wa Tanzania nzima. Swali 'anagombea kwa ajili ya nani?' Linalenga kutaka kujua idadi ya watanzani wataomuunga mkono. Watanzania wangapi kwa maana ya wanachama wa CUF? Jibu ni idadi ya wanachama wote wa CUF na wengine wasio wanachama wa CUF lakini wanamuunga mkono Lipumba. Kwa kuwa ushindi unapatikana kwa idadi kubwa ya wanaokuunga mkono, hivyo ukiungwa mkono na idadi ndogo huwezi kuwa rais wa Tanzania. Ndiyo maana ya swali 'kwa ajili ya nani' na wala siyo dharau kwa wana CUF kama unavyotaka tuamini. Ukiamini hivyo utakuwa unapotosha, lakini kizuri ni kwamba hujapotosha kwa makusudi bali kwa sababu ya uwelewa tu. Ukieleweshwa naamini utarudi kwenye reli. Mbaya ni kama utang'ang'ania kubaki nje ya reli.
Tunaka agombee kwa ajili ya nani? Haya maneno ukienda nayo mbele ya wana CUF hakika CUF wanajitoa siku hiyo hiyo, hii ni dharau kubwa , hata mimi sijaipenda.
 
Ukiona watu wanajifariji leo kwa makala ya 2011 maana yake hawana jipya leo wanajifariji kwa yaliyopita.

Dr Slaa aliishakwisha, Dr Slaa wa 2011 sio Dr Slaa wa leo, kachuja.Na CCM ya 2011 sio CCM ya leo, ipo juu zaidi.
 
Makala nzuri sana hii na itakuwa jambo la ajabu kama CHADEMA na hasa Slaa na Mbowe kama hawatazingatia. Maono ya Jenerali yamekuwa ni kweli, katiba imekwama! Aliyeianzisha ndiye aliyeikwamisha. Ni aibu tupu! Tumepoteza muda wetu na mabilioni ya pesa ambazo zingetumika kuwakopesha wanafunz wa vyuo vikuu au kushughulikia huduma za kijamii kama maji na afya.
 
Watanzania wanafiki sana. Hata wale unaodhani wamesoma na kuelimika nao wanafiki kama wakulima wa darasa la nne. Leo hii ndio Magufuri anapendwa? Mlimjua kuwa anapendwa na watanzania? Mbona mliimpigia debe Lowassa na kutuaminisha anapendwa sana na watanzania. Leo yuko wapi? Opportunists tu nyie. Hata angepitishwa Membe kwa unafiki wenu mngesema atashinda ana uzoefu wa kimataifa. Mtaacha lini unafiki? Kwanini hamkwenda kumshawishi Magufuri agombee na Kikwete aliwaambia muwashawishi watu kugombea? Mkaleta maagizo ya kumshawishi Lowassa akiwa ameshaandaa hema la kukaa. Acheni unafiki. Mnatafuta vyeo tu hapa kwa Magufuri hamna lolote. Eti Magufuri anakubalika na watanzania. Angewaambia mpige mbizi? Acheni unafiki. Mtaungua na moto nyie. Stand where you believe to be correct.

Taratibu mkuu, Lowasa alipigiwa debe na akina Kingunge na wabunge wengine waliokula pesa zake na kumdanganya kuwa ajitahidi kukusanya malaki ya wadhamini kama kigezo cha kukubalika na wananchi. Magufuli anakubalika kwa sana tu na atashinda kwa ushindi wa kishindo. Siko karibu na Magufuli wala siko kutafuta cheo kwa mgongo wake. MUNGU akipenda kunipa cheo atanipa tu.
 
Hiv James Mbatia hana haki ya kupeperusha bendera ya Ukawa...? Mbona mnawazungumzia wawili tu Slab na mchumi prof. Lipumba?

Mbatia hakugombea katika chama chake!! NCCR ilichagua mtu mwingine kugombea hata hivyo amejitoa na pia Makaidi amejitoa! Hivyo waliobaki ni Lipumba na Slaa!!
 
Mbatia hakugombea katika chama chake!! NCCR ilichagua mtu mwingine kugombea hata hivyo amejitoa na pia Makaidi amejitoa! Hivyo waliobaki ni Lipumba na Slaa!!

Slaa amwachie tu Lipumba yeye akagombee ubunge aongeze nguvu ya upinzani bungeni basi, Maana kwa uhakika urais UKAWA hawawezi kushinda na hili nasema toka rohoni na dhamiri yangu ikiwa safi kwa hili. Na Maguguli atashinda kwa kishindo tena kwa halali si kwa goli la mkono kama alivyosema Nape.
 
Thubutuuuuu CDM hawana hiyo spirit ya kuwaachia wengine wagombee! Hiyo ni haki yao hapo mpaka kieleweke tu LIPUMBA akae pembeni kuepusha msongamano!
 
Kwa sababu tunaongelea hisia hakuna sababu ya kubishana. Nami naamini pia kuwa Magufuli hawezi kushinda, na akishinda atashinda kwa margin ndogo kuliko hata ile aliyopata Kikwete 2010. Siyo kwa sababu Kikwete ni bora zaidi ya Magufuli (ninaamini Magufuli ni kiongozi bora kuliko Kikwete) bali kutokana na kuongezeka kwa uelewa wa Watanzania walio wengi dhidi ya uozo wa CCM. Nani yupo sahihi, itajulikana Octoba, hakuna sababu ya kubishana.

Mkuu kwa hili hata tukipinga nitakugaragaza kwa sana tu, tegemea ushindi wa kishindo kwa Magufuli. Sisemi kuwa Magufuli ni malaika lakini utendaji wake na kazi zake (tangible ones) zinaonekana tofauti na Membe. Kila wizara aliyopelekwa ikiwemo wizara ya uvuvi aling'ara. Kashfa ya samaki wabaya wake tu walimtelekeza na hao samaki gharama za kuwahifadhi zikawa kubwa lakini jamaa alitumia sheria na kuwakamata wale jamaa kihalali. Suala la kuuza nyumba hayo yalikuwa ni maridhiano ya baraza la mawaziri likiwa ni shinikizo la Mkapa. Kuuzia ndugu yake nyumba ni udhaifu wa kibinadamu tu ambao hata wewe ukiwa na nafasi ya kumsaidia ndugu yako kihalali ungefanya (nasema kihalali kwa maana kwamba hakumpa bure bali alimuuzia mtu asiyestahili kihalali). Kama ni suala la kuokoa pesa Magufuli kaokoa pesa nyingi huko ujenzi ambako lilishakuwa chaka la wezi wakati Mrema akikwa bosi wa TANROADS na Chenge na Kawambwa wakiwa mawaziri wa wizara hiyo. Pia aliamuru magari yote ya serikali na taasisi zake na yale ya miradi (now DFP) yalikuwa na namba za binafsi yasajiliwe upya kuokoa gharama za bima na matumizi mabaya kiasi cha kuwaudhi wakubwa mpaka Mkapa akamuongozea ulinzi. Wizarani kwake kuna mtu alisikika akisema anamchukia Magufuli kwasababu eti "anajifanya mazalendo sana na anawazibia ulaji).
 
Kwa uhalisia wa mambo kwa mwaka huu wapinzani hawawezi kumshinda Magufuli kwa uchaguzi wa urais. Hili liko wazi kabisa. CCM wangemsimamisha mtu kama Membe njia ingekuwa nyeupeeeeee kwa wapinzani! Magufuli anauzika na anapendwa na watu Tanzania hii. Kwa ushauri wangu namshauri Dr. Slaa amwachie tu Lipumba agombee urais na yeye agombee ubunge ambao ni rahisi sana kushinda. Akaongeze nguvu ya upinzani bungeni. Mtakubaliana na mimi kuwa Slaa akiwa mbunge ameleta mabadiliko mengi katika ulimwengu wa siasa hapa nchini na kuongeza nguvu ya upinzani. Dr. Slaa a.k.a mzee wa mabomu bungeni tunaomba urejee tena mjengoni mchnago wako ni wa muhimu sana kwa taifa hili.
Huu ni uwoga wa wazi kwa Dr Slaa.
 
Slaa amwachie tu Lipumba yeye akagombee ubunge aongeze nguvu ya upinzani bungeni basi, Maana kwa uhakika urais UKAWA hawawezi kushinda na hili nasema toka rohoni na dhamiri yangu ikiwa safi kwa hili. Na Maguguli atashinda kwa kishindo tena kwa halali si kwa goli la mkono kama alivyosema Nape.

Kwa nini Lipumba asigombee ubunge kuongeza nguvu upinzani!!!

Slaa amekwisha kuwa mbunge kwa miaka 15 amekwisha timiza wajibu wake kama mbunge na ana uzoefu wa kutosha!!
 
Hilo halipo. Mara baada ya uchaguzi wa mwaka 2010 CDM ilianza maandalizi ya kuchukua dola na ilimuandaa Dr Slaa. Yeye mwenyewe amejiandaa vya kutosha kitaifa na kimataifa. Lipumba akae pembeni tu kwani amejaribu mno, na sasa watu wamemchoka. Wakati CDM wanafanya hayo maandalizi kwa maandamano na mikutano nchi nzima, yeye amekaa Buguruni tu na kuishia kuita waandishi wa habari. Hatushindi kwa namna hiyo. CDM imepenya mpaka kila kijiji CUF wenyewe wanaishia misikitini.

CDM ndio viongozi wa ukombozi na lazima watoe mgombea kwa ticket ya Ukawa, na mtu huyo sio mwingine ni Dr Slaa. Kama Cuf hawataki waanze mbele, Ukawa itaendelea kusimama.
 
Tunaka agombee kwa ajili ya nani? Haya maneno ukienda nayo mbele ya wana CUF hakika CUF wanajitoa siku hiyo hiyo, hii ni dharau kubwa , hata mimi sijaipenda.

Hakuna mwenye chuki na Professor Lipumba kuwa mgombea wa kiti cha Urais ila inabidi tujiulize tunataka agombee kwaajili ya nini? Tunataka agombee ili ....
Lugha zimeishagongana tayari...kila mmoja ana maana yake hapo.
 
Hilo halipo. Mara baada ya uchaguzi wa mwaka 2010 CDM ilianza maandalizi ya kuchukua dola na ilimuandaa Dr Slaa. Yeye mwenyewe amejiandaa vya kutosha kitaifa na kimataifa. Lipumba akae pembeni tu kwani amejaribu mno, na sasa watu wamemchoka. Wakati CDM wanafanya hayo maandalizi kwa maandamano na mikutano nchi nzima, yeye amekaa Buguruni tu na kuishia kuita waandishi wa habari. Hatushindi kwa namna hiyo. CDM imepenya mpaka kila kijiji CUF wenyewe wanaishia misikitini.

CDM ndio viongozi wa ukombozi na lazima watoe mgombea kwa ticket ya Ukawa, na mtu huyo sio mwingine ni Dr Slaa. Kama Cuf hawataki waanze mbele, Ukawa itaendelea kusimama.

Umeeleza vyema mkuu lakini kwa hali halisi ilivyo mwaka huu Slaa hawezi kumshinda Magufuli. Angekuwa Membe au Pinda, njia ingekuwa rahisi sana. Lakini Kwa CCM kumuweka Magufuli wamechanga vizuri karata zao. Binafsi hata kwenye chaguzi zilizopita za serikali za mitaa nilichagua upinzani wote na nilishajiandaa kuchagua upinzani wote kwenye uchaguzi mkuu, lakini ujio wa Magufuli umenibadili nia. Sasa nitachagua rais Magufuli na Mbunge wa UKAWA. Na nikuhakikishie kuwa watu wa namna yangu wako wengi sana tu. Kwahiyo ingekuwa vyema tu Slaa akaenda kuongeza nguvu ya upinzani bungeni, kuongeza ruzuku kwa chama na kukipunguzia chama mzigo wa kumlipa Slaa mamilioni ya pesa kila mwezi kama makubaliano yao yalivyo.
 
Kwa nini Lipumba asigombee ubunge kuongeza nguvu upinzani!!!

Slaa amekwisha kuwa mbunge kwa miaka 15 amekwisha timiza wajibu wake kama mbunge na ana uzoefu wa kutosha!!

Sijuwi kama ana mvuto kihivyo kiasi cha kuweza kushinda ubunge kwenye jimbo fulani hapa TZ
 
Back
Top Bottom