Jambo Tz
JF-Expert Member
- Jul 19, 2013
- 670
- 203
Nimefarijika sana leo kuwaona hapa
marafiki zangu wengi. Ninapowatazama
hadi machozi yananitoka na kwa uwezo
wa Mungu tutashinda kwani nyote
mnajua nia na ndoto yangu WanaCCM
msiwe na shaka, tutavuka kwa nguvu
zetu... Wingi wenu huu unanipa faraja
katika safari yetu na kwa kumtegemea
Mungu tutashinda. ni kauli ya aliyewahi
kuwa Waziri Mkuu, Edward Lowassa.
Lowassa alitangaza hivi karibuni kuanza
rasmi kwa safari hiyo aliyoiita ya
matumaini ya ndoto zake, ambayo
anasema itatimiza ndoto za Watanzania
za kupata elimu bure, majisafi na
maendeleo ya uhakika.
Alitoa kauli hiyo katika ibada ya shukrani
na kuupokea mwaka mpya, katika Kanisa
la Kiinjili la Kilutheri Tanzania
(KKKT),Usharika ya Monduli Mjini mkoani
Arusha.
Bila ya kutaja safari hiyo ni ipi, Lowassa
anawataka waliohudhuria ibada hiyo
waungane na kaulimbiu yake, Tulifurahi
pamoja, tulihuzunika pamoja na
tutashinda pamoja.
Hafla hiyo ya kimkakati, ilihudhuriwa na
baadhi ya wabunge, wengi wakiwa wa
CCM, wenyeviti wa mikoa kadhaa wa
chama hicho, wakiongozwa na
Mwenyekiti wa Wenyeviti wa CCM,
viongozi wa jumuiya za chama na
wengineo.
Licha ya kutoweka bayana aina ya safari
anayoanza, Lowassa ni miongoni mwa
wanaCCM wanaotajwa kuwa wanaowania
urais, kumrithi Rais Jakaya Kikwete.
Dalili hizi za Lowassa kuutaka urais na
kutafuta kabla ya kipenga kupulizwa,
zimeishtua CCM na kumtahadharisha
kuwa atapoteza sifa ya kupitishwa ifikapo
2015.
Safari tangu 1995
Tamaa ya Lowassa kuutaka urais
haikuanza leo wala jana, ni ya tangu 1995
alipojitokeza kwa mara ya kwanza.
Mwaka huo alikuwa miongoni mwa
wagombea 17 wa CCM walioomba
kuteuliwa kuipeperusha bendera ya
chama hicho.
Majina hayo yalipaswa kujadiliwa na
vikao vitatu vya CCM Kamati Kuu,
Halmashauri Kuu na Mkutano Mkuu.
Kikao cha kwanza kilikua ni Kamati Kuu
ambacho Mwenyekiti wake alikuwa
Mwenyekiti wa CCM wakati huo, Ali
Hassan Mwinyi lakini Baba wa Taifa,
Mwalimu Julius Nyerere alikuwa bado na
ushawishi na nguvu kubwa ndani ya
chama hicho.
Nyerere bila kumungunya maneno,
alisema wazi akiwataja wazi Lowassa na
Waziri Mkuu mstaafu, John Malecela
kuwa hawakuwa wanafaa kugombea.
Nyerere alisema Malecela alikuwa na
madhambi mengi na kwamba alikuwa
ameyabainisha katika kitabu chake cha
Uongozi na hatima ya Tanzania ambacho
pia alielezea udhaifu wa Horace Kolimba,
aliyekuwa Katibu Mkuu wa CCM.
marafiki zangu wengi. Ninapowatazama
hadi machozi yananitoka na kwa uwezo
wa Mungu tutashinda kwani nyote
mnajua nia na ndoto yangu WanaCCM
msiwe na shaka, tutavuka kwa nguvu
zetu... Wingi wenu huu unanipa faraja
katika safari yetu na kwa kumtegemea
Mungu tutashinda. ni kauli ya aliyewahi
kuwa Waziri Mkuu, Edward Lowassa.
Lowassa alitangaza hivi karibuni kuanza
rasmi kwa safari hiyo aliyoiita ya
matumaini ya ndoto zake, ambayo
anasema itatimiza ndoto za Watanzania
za kupata elimu bure, majisafi na
maendeleo ya uhakika.
Alitoa kauli hiyo katika ibada ya shukrani
na kuupokea mwaka mpya, katika Kanisa
la Kiinjili la Kilutheri Tanzania
(KKKT),Usharika ya Monduli Mjini mkoani
Arusha.
Bila ya kutaja safari hiyo ni ipi, Lowassa
anawataka waliohudhuria ibada hiyo
waungane na kaulimbiu yake, Tulifurahi
pamoja, tulihuzunika pamoja na
tutashinda pamoja.
Hafla hiyo ya kimkakati, ilihudhuriwa na
baadhi ya wabunge, wengi wakiwa wa
CCM, wenyeviti wa mikoa kadhaa wa
chama hicho, wakiongozwa na
Mwenyekiti wa Wenyeviti wa CCM,
viongozi wa jumuiya za chama na
wengineo.
Licha ya kutoweka bayana aina ya safari
anayoanza, Lowassa ni miongoni mwa
wanaCCM wanaotajwa kuwa wanaowania
urais, kumrithi Rais Jakaya Kikwete.
Dalili hizi za Lowassa kuutaka urais na
kutafuta kabla ya kipenga kupulizwa,
zimeishtua CCM na kumtahadharisha
kuwa atapoteza sifa ya kupitishwa ifikapo
2015.
Safari tangu 1995
Tamaa ya Lowassa kuutaka urais
haikuanza leo wala jana, ni ya tangu 1995
alipojitokeza kwa mara ya kwanza.
Mwaka huo alikuwa miongoni mwa
wagombea 17 wa CCM walioomba
kuteuliwa kuipeperusha bendera ya
chama hicho.
Majina hayo yalipaswa kujadiliwa na
vikao vitatu vya CCM Kamati Kuu,
Halmashauri Kuu na Mkutano Mkuu.
Kikao cha kwanza kilikua ni Kamati Kuu
ambacho Mwenyekiti wake alikuwa
Mwenyekiti wa CCM wakati huo, Ali
Hassan Mwinyi lakini Baba wa Taifa,
Mwalimu Julius Nyerere alikuwa bado na
ushawishi na nguvu kubwa ndani ya
chama hicho.
Nyerere bila kumungunya maneno,
alisema wazi akiwataja wazi Lowassa na
Waziri Mkuu mstaafu, John Malecela
kuwa hawakuwa wanafaa kugombea.
Nyerere alisema Malecela alikuwa na
madhambi mengi na kwamba alikuwa
ameyabainisha katika kitabu chake cha
Uongozi na hatima ya Tanzania ambacho
pia alielezea udhaifu wa Horace Kolimba,
aliyekuwa Katibu Mkuu wa CCM.