Jela Miezi Sita Kwa Kukaidi Kuvua Baraghashia Mahakamani

duh, kweli kipofu?
Jamani hata kiswahili cha kawaida kinakushinda? sasa kofia na kilemba ni sawa?
Halafu mimi simwombei mabaya huyu ndugu lakini anaonyesha ana ukaidi wa nature kwa sabbu tayari alikuwa na kesi ya kusababisha fujo.Huwezi jua background yake.....
 
Jamani hata kiswahili cha kawaida kinakushinda? sasa kofia na kilemba ni sawa?
Halafu mimi simwombei mabaya huyu ndugu lakini anaonyesha ana ukaidi wa nature kwa sabbu tayari alikuwa na kesi ya kusababisha fujo.Huwezi jua background yake.....

muhimu ni haki imefuatwa?

huwezi tu kumfunga mtu kwa sababu anaonyesha ana ukaidi wa nature

manake tukienda kwa mtizamo huo, mtu aliyekwisha hukumiwa mara kadhaa kwa kosa la wizi, akishtakiwa tena ingekuwa haina haja kusikiliza kesi, na afungwe tu
 
Nimeambiwa jamaa kofia aliivaa ndivyo sivyo! Alifunika kabisa sura yake hata macho yalikuwa hayaonekani!
 
sasa km sio ujinga ninini?....wewe utakataaje kuvua kikofia chako km sio kuwa na asili ya ukaidi usio wa lazima..........angepigwa hata tumiaka tutatu kwa kudharau mahakama........au ni yale mambo ya mahakama ya kadhi ndiyo yanawasumbua na kuwa na misimamo na itikadi pasipotakiwa ??????...tuacheni upuuzi tufuate sheria..
 
BARAZA Kuu la Waislamu wa Tanzania (Bakwata) limetoa siku saba kwa mahakama kutoa ufafanuzi wa hukumu ya kifungo cha miezi sita jela, aliyopewa mshitakiwa Ally Sururu na Hakimu wa Mahakama ya Wilaya ya Ilala, Dar es Salaam baada ya kukaidi amri ya kuvua kofia ya Kiislamu (baraghashia) akiwa kizimbani.

Kwa mujibu wa Bakwata, hukumu hiyo ilitolewa juzi na Hakimu Wilberforce Luhwago baada ya mshitakiwa huyo kukaidi agizo hilo alilompa akiwa kizimbani na kusababisha majibizano yaliyofuatiwa na hukumu hiyo.

“Waislamu tunaamini kuwa Hakimu Luhwago ni kirusi cha udini kinachofanya katika chombo cha kusimamia sheria, tunaiomba mamlaka husika kufuatilia jambo hili kwa haraka na kumwajibisha mhusika ili Waislamu wa Tanzania waendelee kuwa na imani na chombo hiki…,” alisema Mwenyekiti wa Kamati ya Taifa ya Umoja wa Vijana wa Kiislamu ya Bakwata, Dk Seif Sulle.

Sulle ambaye alikuwa akitoa tamko kwa niaba ya Mufti Mkuu wa Tanzania, Shehe Issa Shabaan Simba, katika Ofisi za Makao Makuu ya Bakwata jana kuwa Dar es Salaam wamelisikia Septemba mosi kupitia vyombo vya habari na limedhalilisha mavazi ya ibada ya Kiislamu na kuingilia uhuru wa kuabudu.

Baadhi ya wanasheria waliozungumza na gazeti hili kwa kigezo cha kutotajwa majina yao gazetini, walisema hakuna sheria ya moja kwa moja inayozuia mtu kuvaa kofia mahakamani ila kuna utaratibu wa kimahakama ambao unahitaji kuheshimiwa na kufuatwa na kila anayepaswa kufanya hivyo.

Wameishaanza kukurupuka hawa watu!

Ona mwingine huyu

MKAZI wa Kimara Abduswamadu Shabani (25), mwalimu wa Shule ya kiisilamu (madrasa) ya King'ong'o amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi wilayani Kinondoni kwa tuhuma za kumbaka mwanafunzi wake.

Mwananchi
 
jamaa wanachukulia misimamo yako kama ndiyo ya chadema. ya kukipenda chama na kuuchukia uislam. ndio maana wanajf wengi waliowaislam humu wanaona ndio miisimamo ya chadema. kwahivyo sijui utaimarisha chadema humu au ndio unazidi kuiapka matope cahdema mbele ya waumini wa kiislam?
Kwani kuna uhusiano gani kati ya Rev na CHADEMA?kwani rev ndio Mbowe?
 
jamaa wanachukulia misimamo yako kama ndiyo ya chadema. ya kukipenda chama na kuuchukia uislam. ndio maana wanajf wengi waliowaislam humu wanaona ndio miisimamo ya chadema. kwahivyo sijui utaimarisha chadema humu au ndio unazidi kuiapka matope cahdema mbele ya waumini wa kiislam?

Best umepotoka! Nawapenda waislam sana kwanza ndiyo mabest zangu, kwenye familia yangu kunaupande ni waislam. Hata mchumba wangu Mzenj naye ni muislam. Maandishi ya JF yasikuumize roho broda
 
kuwa na kitu sio tatizo, tatizo moyoni mwako hao ulioano unawaona kama nnai? ikiwa unaandika humu hayo kila mtu mwenye akili timamu ndiyo yaliokuwa moyonoi mwako.

Mkubwa wangu,

Nadhani hizo ni fikra zako, usije niona in real life ukanipiga mawe! Futa hilo moyoni mwako! Siasa za JF zinaweza kukupotosha. Pamoja na akili zako kichwani usiusemee moyo wangu.
 
Ndugu Zangu waislamu! Tuache ushabiki na kushabikia mambo ambayo hamyajui.Kuhusu ayala la huyo jamaa aliye katas kutoa baragashia yake wakati alitakiwa kufanya hivyo ni kosa tena na weza kusema alionewa huruma kwasababu ningekuwa Mimi ndo hakimu nungemfunga meals mmoja.Kwa taarifa yenu ndugu zangu Moslems Mahakamani si mahala pa kufanyia mzaha,ni mahala pa kuheshimiwa na watu wote kam mnabisha embu jaribuni natumai mtakipata cha moto.Nchi yetu inaongozwa kwa misingi ya kisheria,niliwa na maana kuwa kuna Katiba ya Jamhuri ya Muungano ya Tz ya 1977 na marekebisho yake yote from time to time.Katina katiba hii imefafanua na kutenganisha mihimili mitatu yaani Excutive,legislature,na Judiciary hivi vyote vinatakiwa kufanya majukumu yake kikatiba bila kukiingilia chombo au mhimili mwingine,na katika mihimili hii yote mahakama ndo inasimamia ili kouna Kama serikali inafuta utawala wa Sheria na utawala bora vile vile mahakama ndo inatafsiri sheria zilizotungwa na bunge na iwapo sheria hiyo itatokea kupingana na katiba mahakama inaikataa na kilielekeza bunge lifanye marekebisho ilikuendana na katiba au litunge sheria nyingine.Nasema Gaya yote niliwa nataka nijibu wale wanaofikiria eti serikali inaweza kuihamrisha mahakama na kufanya vile serikali inavyotaka hili halipo na Walachia haliwezekani kwa taarifa yenu.Serikali ikifanya hivyo itakuwa imeingilia Uhuru wa mahakama na kuvunja katiba kitu ambacho hakitazamiwi kutokea hata Kidogo hivyo basi ile ndoto yenu ya kuipa serikali Siku 7,mnajisumbua bureeeeee maana serikali haiwezi fanya hivyo.Mahakama inataratibu zake ambazo mtu yoyote anapoitwa,unapotaliw kufanya hili au lile unatakiwa utii amri ya mahakama.Kila Hakimu ah Jaji yeyote yule anamamlaka kamiki na nguvu ya kutoa amri na ni lazima itekelezwe Mara mojarra kutotii amri ndo Kama haul yaliuomkuta huyo jamaa.Kama kweli yeye ni mtu wa kutotii amri na sheria,mbona alipotakiwa kuja mahakani alikuwa anakuja na kuhushuria Mara zote bila kukosa ,je hajui kuwa alikuwa anatii amri sasa kwa niño alikaidi amri halali ya mahakama iliyomtaka ayor kofia?alichokifanya huyu jamaa ni dharau na kuidharau mahakama.Hanoi inapaswa kuelewa kuwa,maakimu na majaji wanamamlaka ya kukufunga au kukuweka hahabusu kwa muda Flani Kama itakavyo wapendeza wao,ili mradi tu umekaidi kutii amri halali ya mahakama,mamlaka waliyonayo mahakimu Ma majaji Mara yanapotolewa huwezi kata rufaa,labda mumuombe na kujishusha kwa huyo huyo Hakimu au Jaji amsamehe na kumfutia hiyo adhabu vinginevyo mjhusika atatumikia hiyo adhabu Mpaka mwisho,kwa kiingereza tunasema hivi "every Judge and Magistrates they have the so called vested discretionary Vested Power and these power once exercised they are Unappellable in any court.So my advice in regards to situation I strogly urged my fellows Muslims and the community at large please respect the Tribunal,Court sessions and all the Orders given therein or thereunder.Wishing u all the best and I hope that you will follows and observed wham you are told to do and not to do.My God blessed u all.
 
Jamani jiulizeni : Sheria kifungu gani huyu mwananchi amevunja ? Na kwa kuvaa baraghashia mahakamani vipi kaidharau ? Je mtu akivaa baraghashia mahali pengine inakua amewadharau watu wengine walio karibu ? Hizi sheria zetu zilitungwa tangu enzi ya ukoloni na sisi vipofu tunazifata tu bila kujua ndio maana mahakimu wetu utawakuta wameevaa nywele za bandia nyeupe za singa mahamakamani - nini maana yake kama sio ujinga kwa hakimu muafrika kuvaa wigi la kizungu ? haya yote yametokana na ukoloni.

Muachieni huyo mzee aliefungwa hamna makosa anlinda haki yake ya uhuru wa kuvaa na kusitiri mwili wake.
 
Back
Top Bottom