digba sowey
JF-Expert Member
- Mar 1, 2017
- 10,401
- 22,956
Hii inanifikirisha sana mimi,ndo maana kesi za namna hii haziishi sababu sheria hii hailengi kutatua kero za wanafunzi au watoto wadogo chini ya miaka 18 kuhusu kujihusisha na mapenzi ,sheria omekaa katika kumkomoa mtia mimba (mbakaji) mtiliwa mimba (baba/mama)na mtiwa mimba(binti) hapo hakuna namna mzazi wa binti lazima abebe jukumu la kulea mimba na mjukuu na atakayezaliwaSasa hiyo mimba wataitoa ama maana baba kijacho ndo huyo mmempelka gerezani
Binafsi kama serikali itadhamiria kulimaliza hili tatizo haina budi kutoa pesa kwa familia za waathirika ili kumuhudumia mwathirika na mtoto atakayezaliwa,hii ni kwa sababu kwa mtu kama mimi siwezi mfunga mtu kisa kapiga mimba binti yangu harafu baadae nijitwike mzigo wa kulea na kuhudumia mjukuu asiye na baba,ni kheri kumwajibisha mkosaji wangu kwa faini au awajibike katika malezi,lakini kama government itawajibika kutoa japo pesa kidogo ili kumhudumia mwathirika watu wengi watajitokeza kuripoti wabakaji wote.Mwisho wa siku kesi kama hizi zitakuwa historia
Mimi hapa mwaka huu nilikuwa mwalimu wa darasa kidato cha pili,wanafunzi waliopigwa mimba kwa darasa langu ni zaidi ya watoto watano ajabu ni kuwa hakuna mtia mimba hata mmoja aliyepelekwa gerezani,hii ni kutokana na utaratibu wa wazazi kuyamaliza wao kwa wao ili angalau mtoto atakayezaliwa asikose baba.