Jela miaka 30 kwa kumpa ujauzito mwanafunzi

Nyendo

JF-Expert Member
Joined
Jun 4, 2017
Posts
1,417
Reaction score
5,020
Mahakama ya Hakimu mkazi Mkoa wa Tabora imemuhukumu kutumikia kifungo cha miaka 30 jela kijana aliyefahamika kwa jina la RWAKI ZAKARIA baada ya kupatikana na hatia ya kumbaka mwanafunzi wa darasa la sita anayesoma Shule ya Msingi KIGWANHONA katika Kijiji cha Kigwanhona wilayani Uyui na kumsababishia ujauzito.

Katika shauri hilo namba 60 la mwaka 2020 ilidaiwa mahakamani hapo na Wakili wa Jamhuri, John Nkonyi kwamba mshtakiwa alitenda kosa hilo kati ya Januari na Februari mwaka huu kinyume na Kifungu cha 60 cha Sheria ya Elimu Sura ya 353 iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2019.

Ilielezwa Mahakamani hapo kuwa Rwaki ambaye ni mshtakiwa alikuwa akimchukua mwanafunzi huyo wa darasa la sita anayeishi na Bibi yake katika eneo la Kwandanae porini na kumbaka mara kwa mara na kisha kumrudisha nyumbani hadi kufikia hatua ya kumpa ujauzito na kusababisha kukatishwa masomo binti huyo.

Hakimu mkazi katika Mahakama hiyo ya Tabora, Ajali Milanzi baada ya kupitia ushahidi wa watu wanne wa upande wa mlalamikaji na ushahidi uliotolewa na mshtakiwa, Mahakama ilijiridhisha pasipo shaka yoyote kwamba mshtakiwa Rwaki Zakaria amehusika kutenda kosa hilo la jinai na kumhukumu kutumikia kifungo cha kwenda jela miaka 30 huku ikiacha nafasi kwa mshtakiwa kutafuta haki yake kwa kukata rufaa endapo hataridhika na hukumu hiyo.
 
Hii habari ya kusema kumbaka mwanafunzi mimi naona sio sahihi kabisa!Ingepaswa kuwa kumbaka binti wa miaka kadhaa ili wasomaji tujue!

Kusema mwanafunzi wa darasa la 6 haitoshi maana unaweza kukuta binti wa darasa la 6 lakini ana umri wa miaka 18! Sasa hapo unawakuwa ubakaji? Sifa ni nini?Mwanafunzi au umri mdogo?

Nways kwahiyo huyo binti japo kabakwa basi elimu ndio bye bye maana ujauzito unamkosesha sifa ya kuendelea na masomo katika mfumo rasmi!
 
Toka jan/feb? Inaonesha jamaa aligoma kuyamaliza na bibi ndio maana wakaamua kumfunga
 
Hii habari ya kusema kumbaka mwanafunzi mimi naona sio sahihi kabisa!Ingepaswa kuwa kumbaka binti wa miaka kadhaa ili wasomaji tujue!

Kusema mwanafunzi wa darasa la 6 haitoshi maana unaweza kukuta binti wa darasa la 6 lakini ana umri wa miaka 18! Sasa hapo unawakuwa ubakaji? Sifa ni nini?Mwanafunzi au umri mdogo?

Nways kwahiyo huyo binti japo kabakwa basi elimu ndio bye bye maana ujauzito unamkosesha sifa ya kuendelea na masomo katika mfumo rasmi!
Hapo ni mambo ya hasira na kukomeshana lakini hakuna atakayefaidika.

So mtoto atalelewa na nani au watatoa mimba?

Na kama atazaa, atakua akijua baba yaje yuko jela Miaka 30.

Hapo busara huwa ni mazungumzo tu.
 
jamaa alikuwa anapigia kwenye nyasi tu (porini)

IMG-20201222-WA0000.jpg
 
Hii habari ya kusema kumbaka mwanafunzi mimi naona sio sahihi kabisa!Ingepaswa kuwa kumbaka binti wa miaka kadhaa ili wasomaji tujue!

Kusema mwanafunzi wa darasa la 6 haitoshi maana unaweza kukuta binti wa darasa la 6 lakini ana umri wa miaka 18! Sasa hapo unawakuwa ubakaji? Sifa ni nini?Mwanafunzi au umri mdogo?

Nways kwahiyo huyo binti japo kabakwa basi elimu ndio bye bye maana ujauzito unamkosesha sifa ya kuendelea na masomo katika mfumo rasmi!
Hapo kosa ni kumpa mimba mwanafunzi, haijalishi ana umri gani. Kisheria tafsiri ya mwanafunzi, ni yule ambae yuko primary school au secondary school. Ingekuwa kosa ni kubaka tuu, sasa hapo ndo tungeangalia umri, aliyebakwa ana umri gani, kama binti ana umri chini ya miaka 18 hapo kosa la kubaka lipo.

Lakini kama yuko miaka 18 nakuendelea na huyo binti ameridhia kufanya mapenzi na huyo mwanaume basi kosa la kubaka halipo. Lakini kama ana miaka 18 na kuendelea halafu hajaridhia kufanya mapenzi na huyo mwanaume kosa la kubaka lipo.
 
Kuna binadamu wanasikitisha sana...

Ila kwenye kesi kama hizi, kuna ambao wanaofungwa kuna ambao wanaachiwa huru...

Cc: mahondaw
 
Kila siku zinatolewa adhabu za kubaka na kutia mimba wanafunzi lakini bado raia wanacheza na moto.

Kama kusengekuwa na miaka 30 jela nadhani hali ingekuwa mbaya zaidi.
Sijui Ile kitu imewekewa nn Yan watu wanarudia kosa Hilo hilo
 
Hapo kosa ni kumpa mimba mwanafunzi, haijalishi ana umri gani. Kisheria tafsiri ya mwanafunzi, ni yule ambae yuko primary school au secondary school. Ingekuwa kosa ni kubaka tuu, sasa hapo ndo tungeangalia umri, aliyebakwa ana umri gani, kama binti ana umri chini ya miaka 18 hapo kosa la kubaka lipo.

Lakini kama yuko miaka 18 nakuendelea na huyo binti ameridhia kufanya mapenzi na huyo mwanaume basi kosa la kubaka halipo. Lakini kama ana miaka 18 na kuendelea halafu hajaridhia kufanya mapenzi na huyo mwanaume kosa la kubaka lipo.
mahakama itajuaje km alidhiria au alilazimishwa
 
Mwezi huu tu huko tabora watu kibao wanaenda ngome kwa kesi hizo
 
Back
Top Bottom