Jehanamu Ya Bongo! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Jehanamu Ya Bongo!

Discussion in 'Jokes/Utani + Udaku/Gossips' started by Pazi, Oct 10, 2012.

 1. P

  Pazi JF-Expert Member

  #1
  Oct 10, 2012
  Joined: Mar 5, 2011
  Messages: 2,918
  Likes Received: 623
  Trophy Points: 280
  [FONT=&quot]MTU mmoja alifariki na kwenda jehanamu. [/FONT][FONT=&quot]Kufika huko akakuta kuna jehanamu tofauti tofauti kwa kila nchi. Akaamua kuzunguka zunguka ili aweze kuipata jehanamu yenye maumivu kidogo zaidi. Akaiendea jehanamu ya Ujerumani. Akamwuliza mtu aliyemkuta mlangoni. "Wanakufanyaje ukiingia humu?" Akajibiwa. "Kwanza wanakuweka kwenye kiti cha umeme kwa saa moja, kisha wanakulaza kwenye kitanda cha mizumari kwa saa moja nyingine. Kisha anakuja shetani wa Kijerumani anakucharaza bakora kutwa nzima." Mtu huyo hakuipenda kabisa
  jehanamu hiyo. Akaamua kujaribu jehanamu za Marekani, Uingereza, Urusi na nyinginezo nyingi. Lakini akagundua kuwa zote zina
  adhabu sawa tu na jehanamu ya Ujerumani. [/FONT]

  [FONT=&quot]Kisha akaifikia jehanamu ya Tanzania. Akastaajabu kuona kuna foleni ndefu kweli ya watu wakisubiri kuingia humo. Kwa mshangao usiosemekana akauliza, "Jamani kwani humu wanawafanyaje?" Akajibiwa, "Kwanza wanakuweka kwenye kiti cha umeme kwa saa moja, kisha wanakulaza kwenye kitanda cha mizumari kwa saa moja nyingine. Kisha anakuja shetani wa Kitanzania anakucharaza bakora kutwa nzima." [/FONT]  [FONT=&quot]Akazidi kustaajabu. Akauliza, "Lakini mbona kinachofanyika humu ni sawa kabisa na kinachofanyika kwenye jehanamu zingine, sasa kwa nini hapa kuna foleni kubwa sana watu wote wanakimbilia huku?" Jamaa mmoja akamshika mkono. Akamvutia pembeni. Akamnong'oneza, "Watu wanakimbilia huku kwa kuwa jehanamu ya Tanzania haina umeme wa uhakika, unakatika katika kila dakika kwa hiyo kiti cha umeme hakifanyi kazi. Halafu pia misumari ilishalipiwa lakini wala haijaletwa na mzabuni kwa hiyo kitanda cha humu ni raha tu kukilalia. Na jambo jingine ni kuwa shetani wa Kitanzania alipokuwa duniani alikuwa mtumishi wa umma. Kwa hiyo ameshazowea kufika ofisini na kusaini kitabu cha mahudhurio na kisha kuondoka zake kwenda kufanya shughuli zake binafsi.[/FONT]
   
 2. Belium

  Belium Member

  #2
  Oct 10, 2012
  Joined: Feb 1, 2012
  Messages: 9
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 5
  Hahaaahaaaaaa! Joke but its da truth.
   
 3. farkhina

  farkhina Platinum Member

  #3
  Oct 10, 2012
  Joined: Mar 14, 2012
  Messages: 12,831
  Likes Received: 775
  Trophy Points: 280
  Nimechekaaaaje

  Sent from my BlackBerry 9100 using JamiiForums
   
 4. kamtu33

  kamtu33 JF-Expert Member

  #4
  Oct 10, 2012
  Joined: Mar 15, 2012
  Messages: 973
  Likes Received: 190
  Trophy Points: 60
  Habari nyepesi nyepesi
   
 5. k

  kitero JF-Expert Member

  #5
  Oct 10, 2012
  Joined: Feb 21, 2012
  Messages: 563
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  ok, learning
   
 6. k

  kitero JF-Expert Member

  #6
  Oct 10, 2012
  Joined: Feb 21, 2012
  Messages: 563
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  is that TANZANIAN image?
   
 7. mapanga3

  mapanga3 JF-Expert Member

  #7
  Oct 10, 2012
  Joined: May 1, 2012
  Messages: 659
  Likes Received: 556
  Trophy Points: 180
  Jidanganyani tu
   
 8. PhD

  PhD JF-Expert Member

  #8
  Oct 10, 2012
  Joined: Jul 15, 2009
  Messages: 3,819
  Likes Received: 818
  Trophy Points: 280
  duh hii kali sana kwa kweli
   
 9. P

  Pazi JF-Expert Member

  #9
  Oct 11, 2012
  Joined: Mar 5, 2011
  Messages: 2,918
  Likes Received: 623
  Trophy Points: 280
  Jamani hii jokes tu ila Jahannam kweli hakuna mchezo tusiwache kuswali.
   
 10. G

  GADO Member

  #10
  Oct 12, 2012
  Joined: Oct 7, 2012
  Messages: 28
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mmmm usithubuku kukutwa ohoooooooo
   
Loading...