Jeff Bezos mtu tajiri duniani: Namna alivyounda kampuni ya Amazon.com

Drop shipping Tanzania

Senior Member
Jun 15, 2020
198
500
Namna ambavyo Jeff Bezos alivyounda kampuni ya Amazon na kuwa mtu tajiri zaidi duniani

Miaka 25 iliyopita Jeff Bezos , aliona kuwa hapo baadae kuwa mambo yatabadilika , maduka yatapoteza umaarufu na yatalazimika kutoa burudani ili yasifungwe.

Kutokana na wazo lake hilo alitengeneza kampuni.

Amazon, kampuni inayofanya biashara kwa njia ya mtandao iliyoanzishwa mwaka 1994, ikawa kampuni ya pili duniani yenye matrilioni ya dola kufikia Septemba 2018 (ikipitwa kidogo na kampuni ya Apple).

Ni vigumu kuamini ilianza kama kampuni ya kuuza vitabu vya mtumba.

Lakini sasa mmiliki wake Bezos ni mtu tajiri zaidi duniani, akiwa na mipango mikubwa katika kuubadili ulimwengu wa teknologia. Pia Jeff Bezos
Anamiliki gazeti maarufu la Washington post.

Kampuni yake ya masuala ya anga, iitwayo Blue Origin, ina malengo ya kupeleka vifaa na binaadamu mwezini ifikapo 2024.

Mwezi Septemba mwaka 2018 aliahidi kutoa dola bilioni 2 kutoka kwenye utajiri wake kuwezesha kifedha mtandao wa shule za msingi na kusaidia wasio na makazi Marekani.

Mke wake wa zamani Mackenzie Bezos aliyahidi dola bilioni 37 kwenye mradi huo.

Miaka kadhaa iliyopita , rafiki wake wa kike wa shuleni alisema kuwa alitegemea siku zote kuwa atakuwa tajiri , na kuweza kufikia ndoto za kufika kwenye anga la mbali.

''Suala halikuwa kuhusu fedha. Ilikuwa kuhusu nini fedha hizo angezifanyia kwenye kuibadili kesho,'' aliliambia gazeti la wired.

Makoloni ya angani
Dalili za ndoto za Jeff ziliibuka miongo mingi iliyopita.

Mtoto wa wazazi ambao walimpata wakiwa na umri mdogo na kuachana haraka baada ya kuzaliwa, alilelewa hasa mjini Texas na Florida na mama yake Jackie, na baba yake wa kambo Mike Bezos, aliyekuja kuwa afisa mwanadamizi wa kampuni kubwa ya Exxon aliyekimbia Cuba akiwa kijana mdogo baada ya Fidel Castro kuingia madarakani.

Alionesha kipaji cha uhandisi na sayansi toka akiwa na umri mdogo, akifungua kwa bisibisi kitanda chake kidogo akiwa na umri wa miaka mitatu, na katika hotuba yake ya kumaliza sekondari alizungumzia ndoto yake ya kuanzisha makoloni kwenye sayari za juu.

Jeff Bezos alikutana na mkewe ambaye wametalikiana hivi karibuni MacKenzie walipokuwa wameajiriwa pamoja jijini New York na wana watoto wanne

Katika Chuo Kikuu cha Princeton, Bezos alisomea uhandisi na sayansi ya komputa, na baadae kutumia ujuzi wake katika kampuni za kifedha za jijini New York ambapo alikutana na mkewe ambaye wametalikiana hivi karibuni.

Akiwa na miaka 30, aliacha kazi baada ya kubaini takwimu kuhusu kukua kwa mtandao wa intaneti.

Mwaka 2010 akiwa anatoa hotuba katika chuo cha Princeton, Bezos alikumbuka uamuzi wake wa kuanzisha na kampuni ya Amazon kama "njia isiyo salama".

''Niliamua nijaribu. Sikuwahi kufikiria kuwa ningejuta kujaribu na kushindwa. Na nilihisi kuwa ningejilaumu maisha yote kwa kufanya uamuzi wa kutokujaribu hata kidogo," alisema Mfalme wa biashara za mtandaoni

Kamari aliyoicheza Bezos kwa kuanzisha kampuni kwa mtaji wa $300,000 ambazo zilikuwa ni zake na kusaidiwa na familia ilipa kwa haraka.

Ndani ya mwezi mmoja tangu kuzinduliwa kwa Amazon mwaka 1995, tayari ilikuwa imesafirisha oda za majimbo 50 ya Marekani na katika nchi mbalimbali 45 kwa mujibu wa kitabu cha maisha ya bilionea huyo.

Miaka mitano ya kwanza ya Amazon, wateja waliongezeka kutoka 180,000 kufika milioni 17. Mauzo yakapanda kutoka dola laki tano mpaka nilioni 1.6.

Wawekezaji wenye majina makubwa kutoka kwenye wimbi la kizazi cha 'dot com'.

Mwaka 1997 kampuni hiyo ikaingia kwenye soko la hisa na kuweza kupata kiasi cha dola milioni 54 na kumfanya Bezos kuwa mmoja kati ya matajiri wakubwa duniani kabla ya miaka 35.

Mwaka 1999, gazeti la Time lilimtaja kuwa mfanyabiashara mdogo wa mwaka akiitwa ''mfalme wa biashara ya mtandaoni.''

Bezos ameiongoza Amazon katika kile alichokitaja kuwa mbinu za muda mrefu na kujikita zaidi kwa wateja.

Katika kutimiza kwa vitendo , kunamaanisha kuwa kampuni iko tayari kutumia pesa ili kuingiza pesa, wakati mwingine kuchukua hatua ya kupunguza faida , kwa kutoa huduma bure ya kusafirisha bidhaa.

Lakini Amazon haikusita kuweka akiba pale inapoweza, kuwafanya wafanyakazi wa makao makuu kulipia maegesho, kupambana na asambazaji, kupinga jitihada za kuunda vyama vya wafanyakazi na kuepuka kodi kadiri inavyowezekana.

Kampuni ilifikia hatua ya kushindwa , kama vile uwekezaji wa kwanza kwenye tovuti ya Pets.com ambayo baadae ilipoteza fedha.

Amazon ilikuwa na mapato ya zaidi ya dola bilioni 230 mwaka 2018, na kuajiri karibu watu 650,000 duniani, hiyo ni zaidi ya idadi ya watu wa nchini Luxembourg.

Kampuni hiyo inajihusha uuzaji, usafirishaji na uhifadhi wa mizigo,. Pia ni jukwaa la mamelfu ya makampuni ambayo yanauza bidaa zao na pia inahifadhi data za kimtandao na kuuza kwa kampuni mbalimbali ulimwenguni.

Makampuni makubwa kama ya malazi ya AirBnB na filamu Netflix na mengine zaidi ya milioni moja yanategemea mtandao wa amazon moja kwa moja kama uti wa mgongo wa huduma zao mtandaoni.

Mwaka huu pekee, Amazon imewekeza hisa ama kuyanunua makampuni kadhaa yanayojihudhi na maroboti, matangazo na magari yanayojiendesha yenyewe pamoja uhifadhi wa data mtandaoni.

Na viongozi waandamizi wa kampuni hiyo wanaendelea kutafuta makampuni mengine ya kuwekeza ama kuyanunua. Upinzani mkali
Kukua kwa Amazon hata hivyo hakujaacha kukosolewa, hususani jinsi ilivyoliteka soko, malipo ya kodi, uhusiano na waajiriwa wake na kuchupa kwa gharama za pango katika mji wa Seattle.

Amazon ilikuwa na mpango kabambe wa wa kujenga ofisi za pili kwa ukubwa katika jimbo la New York, lakini ikaachana na mpango huo baada ya kupingwa vikali na wanasiasa wa eneo hilo.

Mgogoro huo ulichangiwa na kiwango kikubwa na kiwango cha vivutio vya kikodi cha dola bilioni 3 ili kuiwezesha kampuni hiyo kutekeleza mradi huo.

Uwezekano wa kupata misamaha na vivutio vya kikodi kwa moja ya makampuni yenye mafanikio zaidi duniani imekuwa ni jambo ambalo Amazon ikikosolewa nalo mara kwa mara.

Ili kukabiliana na ukosoaji huo, Bezos ameanza kutumia zaidi mtandao wa kijamii wa Twitter, ambapo hutuma picha za wazazi wake na mbwa wake.

Pia Amazon imejibu mapigo kwa kutumia pesa, ikiongeza kwa zaidi ya mara mbili matumizi yake kwa kampuni za ushawishi kutoka mwaka 2014 mpaka kufikia dola milioni 14.4 mwaka jana, kwa mujibu wa tovuti ya OpenSecrets.org.

Kukosolewa na Trump
Rais Donald Trump amekuwa mkosoaji mkubwa wa Bezos (kulia) na gazeti lake la Washington Post
Pamoja na jitihada, Kampuni imekuwa na mkosoaji mkuu kabisa: Rais wa Marekani Donald Trump.

Amekuwa akiishutumu Amazon kwenye ukurasa wa twitter kutumia gharama ndogo za usafirishaji kutoka shirika la posta akisema kuwa wanaitumia vibaya ofisi ya posta kwa shughuli za manufaa yao kwa pesa za walipa kodi wa Marekani.

Akiwa na utajiri wa thamaniya dola bilioni 160, Bezos, 55 amekuwa akikabiliwa na maswali kuhusu shughuli za kujitolea.

Mwezi Septemba mwaka jana, alitangaza kutoa dola bilioni mbili kusaidia mtandao wa shule za msingi na kusaidia watu wasio na makazi Amerika.

Mbali na kupongezwa ulimwenguni, mwanzilishi wa Amazon alikumbana na ukosoaji mkali.

Bezos amesema ana mipango ya kutumia njia nyingine tofauti ya kusaidia jamii kuliko namna anavyofanya biashara akilenga matokeo ya haraka ya muda mfupi kuliko ya muda mrefu.

Dunia itakuwa ikisubiri kuona kama mpango huu utakuwa na mafanikio.
 

Root

JF-Expert Member
Jan 23, 2012
40,563
2,000
Huo utajiri
We usikie tu , usiushuhudie
All in all jamaa tajiri kana kwamba anaweza akasema yeye Mungu na wakafanya ibada fresh. Uzuri Hana majizuno nilikuwa nae Finland yuko simple kuliko mnavyodhani unaweza mpita bila salamu kumbe ndo mmiliki wa hela za dunia
Ukakutana naye. Yule jamaa nijuavyo ana security ya maana
 

Drop shipping Tanzania

Senior Member
Jun 15, 2020
198
500
Huo utajiri
We usikie tu , usiushuhudie
All in all jamaa tajiri kana kwamba anaweza akasema yeye Mungu na wakafanya ibada fresh. Uzuri Hana majizuno nilikuwa nae Finland yuko simple kuliko mnavyodhani unaweza mpita bila salamu kumbe ndo mmiliki wa hela za dunia
Jamaa yupo simple lkn security yake kwa siku inagharimu million kadhaa
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom