Jeetu Patel na Kamlesh Pattni fundisho kwa Watanzania

Rubabi

Senior Member
Nov 30, 2006
170
11
Kuna mambo mengi yanayofanana kati ya ufisadi uliofanywa na viongozi wa kenya kwa kumtumia Kamlesh Pattni(goldenberg scandal,scandal kubwa kuliko zote katika historia ya kenya) na uchafu wa Balali BOT, zaidi ya kuwa wote ni wahindi.

Ninachojiuliza mimi ni kwamba je huyu Patel atachukuliwa hatua kali kweli hasa ikichukuliwa kuwa ameshirikiana katika ufisadi huu na baadhi ya viongozi wa serikari yetu?

Tuangalie Pattni.Miaka kumi na tatu sasa imepita,Pattni alitiwa mahabusu muda mfupi, alafu akaachiwa.Hivi sasa kesi yake bado inaendelea lakini inaelekea serikari ya kenya haitaki kumchukulia hatua zozote kubwa i.e kutaifisha mali yake nk.Na bado tu anapeta mitaani.

Zaidi Pattni ameazisha chama cha siasa, amekuwa mlokole (sasa anaitwa Paul) na sasa anaagalia kuingia kwenye bunge la Kenya-chama chake kimepata wafuasi na sitashangaa kusikia anakuwa MP soon.Kwa siasa za Kenya,akishakuwa MP, nani atamfuatilia?

Mfano huu ni funzo kwetu wa TZ.Kuna uwezekano kabisa hawa mafisadi watatumia tactics hizo hizo,mwishowe hakuna mtu hata moja atakayechukuliwa hatua zaidi ya kafara Balali.
 
Kuna uwezekano kabisa hawa mafisadi watatumia tactics hizo hizo,mwishowe hakuna mtu hata moja atakayechukuliwa hatua zaidi ya kafara Balali.
Rubabi,

Shukrani kwa ujumbe, sorry kwamba ujumbe ulikuwa duplicate nimeondoa nyingine baada ya kugundua hilo.

BTW: Kumradhi wanachama, kuna mwanachama mmoja nimelazimika kumfungia MOJA KWA MOJA kwani matangazo alokuwa akirusha hapa si salama kwenu. DO NOT purchase anything from the user ensyncltd1

Thanks
 
Back
Top Bottom