Allen Kilewella
JF-Expert Member
- Sep 30, 2011
- 26,028
- 51,309
Jinsi viongozi na wanachama wa Vyama vya upinzani wanavyotendewa na wana CCM walioko kwenye uongozi wa nafasi za kisiasa na pia wanavyotendewa na Serikali kwa ujumla, Jee wapinzani hao nao wasilipe kodi kama kuonesha kupinga kwao kwa kubaguliwa huko?
Spika wa Bunge anaposema watu wa Arusha "you deserve better" anataka kusema kwamba Livingistone Lusinde ni bora zaidi kuliko Lema. Mbona hawaambii watu wa Jimbo la Mtera kama na wao wamepatia ama walikosea kumchagua Lusinde kuwa mbunge wao? Kwa nini maneno ya kebehi na dharau hutolewa kwa wapinzani kama vile wenyewe hawalipi kodi za nchi hii?
Kila jambo linalofanywa kwa wapinzani wa CCM hufanywa kama vile ni hisani, lakini linapokuja suala la kulipa kodi hata wale wanaokejeliwa na kudharauliwa nao hutozwa kodi. Ni kwa nini inaonekana ni halali kuwatenga wapinzani lakini linapokuja suala la kulipa kodi wapinzani hawatengwi?
Inakuwaje unachukua kodi kwa mtu ambaye akitaka kuitumia kodi hiyo ni LAZIMA ionekane kama vile ni dhalili sana au anatakiwa kuiabudu CCM na viongozi wake ili aitumie kodi hiyo? Kama CCM inaona inaweza kuendesha nchi bila ya wapinzani basi iache kutoza kodi kwenye majimbo na kata zote ambazo zinaoongozwa na upinzani!