Je, Zanzibar ni koloni la Tanganyika?

Je, Zanzibar ni koloni la Tanganyika?

mwankuga

JF-Expert Member
Joined
Aug 30, 2010
Posts
334
Reaction score
120
JE, ZANZIBAR NI KOLONI LA TANGANYIKA?

Rasimu ya Katiba mpya,sasa iko mikononi mwetu.Hii ni nafasi pekee kwetu Watanzania,kuisoma,kuielewa na kutoa maoni ya ama kuboresha,kuongeza au kupunguza chochote.Lakini sasa ni wajibu wa Mabaraza ya Katiba ya Kata na bunge la Katiba kuhakikisha wanajadili rasimu hiyo kwa kuweka masilahi ya Taifa mbele.

Kuna mapendekezo mengi sana katika rasimu ya katiba mpya.Lakini moja lililonigusa ni suala la Muungano.Tume ya mabadiliko ya Katiba mpya baada ya kupitia maoni ya watanzania imekuja,na mfumo wa serikali tatu,Tanzania bara (Tanganyika),Zanzibar na serikali ya Shirikisho.Kwa maana hiyo,kama mapendekezo hayo yatapitishwa na Mabaraza ya kata ya katiba,Bunge la Katiba na baadae kupigiwa kura na wananchi,ni wazi kwamba ule mfumo wa serikali mbili ambao umetumika kwa miaka 49 utakuwa umefika kikomo.

Mimi ni miongoni mwa watu wanaopinga pendekezo hilo.Sababu nitatoa.Kabla sijatoa sababu za kupinga mfumo wa serikali tatu,ningependa tujikumbushe japo kidogo tulikotoka.Historia ni mwalimu mzuri japo haiwezi kutufanya kuwa watumwa.

Ni miaka takribani 50 tangu nchi nyingi za Afrika zipate uhuru .Kizazi cha kwanza cha viongozi ambacho kilionja chungu ya ukoloni kwa kukamatwa,kupigwa,kuteswa na kuawa kiliona umuhimu wa bara la Afrika kuungana.Juhudi za kuungana kwa bara la Afrika ili kuwa na sauti moja kimataifa ziliongozwa na Kwame Nkrumah (Ghana) na Mwl.Nyerere (Tanzania).Japo miamba hii ya Afrika ilikuwa na maono/mawazo tofauti ya jinsi ya kufikia lengo la kuungana (AFRICAN UNION),lakini lengo lao lilikuwa ni moja,kuona Afrika inaungana na kukabiliana na ukoloni mamboleo (NEO-COLONIALISM),ambao kwa sasa tuungeita ni utandawazi (GLOBALIZATION).

Mwalimu Nyerere alikuwa ilipendekeza,ili kufikia lengo la kuwa na Afrika moja,basi ingekuwa vema kuanza na ushirikiano wa kikanda (REGIONAL INTEGRATION) kama vile EAC.Wakati Dr.Kwame Nkrumah alitaka kuharakisha kuungana kabla ya ukoloni mambo leo hajakita mizizi na kabla ya viongozi wapya wa Afrika huru hawajaona utamu wa madaraka.Mijadala ya wakati huo ilikuwa imegawanyika katika makundi hao,huku viongozi wengi wakipendelea wazo la Mwalimu Nyerere.

Ukisoma vitabu vya Nkrumah hasa AFRICA MUST UNITE (1963) na NEO-COLONIALISM (1965) ungeweza kuona dhamira ya wazi ya Nkrumah na hofu yake kwa ukoloni mambo leo.Viongozi wengi wa Afrika walimpinga na kumchukia Nkrumah huku wengine wakimwiita mroho wa madaraka.Lakini historia imethibitisha kwamba Nkrumah alikuwa ameona mbali sana.Hata katiba ya Ghana huru,ilikuwa na kipengele cha kwamba Ghana ingesalimisha mamlaka yake kwa Serikali ya Muungano wa Afrika endapo ingeundwa.Hata Mwalimu Nyerere akiongea kwenye maadhimisho ya miaka 40 ya uhuru wa Ghana,mwaka 1997 alikiri kuwa wazo la Nkrumal lilikuwa sahihi.

Baadaye tumeendelea na harakati za Pan-Africanism,ambayo mimi ni muumini,ingawaje kwa sasa imebaki jina tu.Mambo muhimu ambayo Pan-Africanism ilitakiwa kusimamia ni pamoja na maendeleo ya Afrika,kuimarisha demokrasia ndani ya bara la Afrika na kupinga ukoloni mambo leo.

Hata Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ilikuwa njia ya kuelekea kwenye umoja wa Afrika,japo kuna maelezo mengi kuhusu chanzo/sababu za Muungano huo,lakini kwa mtu yeyote mwenye akili timamu hawezi kupinga dhana ya kuungana.Kwa wakati ule inawezekana muundo wa Muungano ulikuwa safi.Na hili limewahi kuzungumzwa sana Mwalimu Nyerere.Kwamba isingekuwa rahisi sana kuunda serikali moja kutokana na historia.Wakati Tanganyika ilipoteza mamlaka yake,Zanzibar ikabaki na mambo kadhaa.Kutoka na sababu za kihistoria na udogo wa Zanzibar (geography and demography),ingeonekana kuimeza Zanzibar kwa kuunda serikali moja.

Lakini lengo lilikuwa kuona Zanzibar na Tanganyika zinaelekea kwenye serikali moja hatua kwa hatua.Lakini mambo yaliyoendelea baada ya Muungano kutoka pande zote mbili (Mwalimu Nyerere na Karume),pengine yaliharibu dhana nzima ya Muungano na kuzusha manung’uniko kutoka pande zote mbili,hasa upande wa Zanzibar.Inasemekena Karume,kabla ya kifo chake alikuwa najiandaa kuvunja Muungano kwa kile kilichoitwa Mwalimu Nyerere kukiuka makubaliano ya awali,akitumia sentensi “muungano ni kama koti likukubana unavua”.

Kuna watu wachache wanaamini kwamba Zanzibar ni koloni la Tanganyika,na hili linatokana na namna masuala/hoja za Muungano zilizokuwa zinashughulikiwa.Moja ni namna mambo ya muungano yalivyoongezwa kutoka 11 hadi 22,ambayo tafsiri yake ingekuwa kupoteza Mamlaka ya Zanzibar.Hili lilisababishwa na udhaifu wa Karume ambaye hakujali mambo ya kisheria na ubabe wa Mwalimu Nyerere kwa upande wa pili.

Lakini suala la pili ambalo naliona ni kubwa zaidi ni “kulazimishwa” kujiuzuru aliyekuwa rais wa Zanzibar (1972-1984) Aboud Jumbe,kwa kuhoji mambo ya Muungano.Tafsiri ya suala hili,lingeonyesha kwamba Zanzibar sio nchi huru.Inakuwaje rais wa nchi anaondolewa kwa namna ile,bila hata kuwashirikisha wananchi wa Zanzibar?

Suala la tatu ni namna mijadala ya Muungano ilivyokuwa inashughulikiwa na kuzimwa.Japo hata Tanzania bara (Tanganyika) kulikuwa na mijadala lakini upande wa Zanzibar ilichukua sura nyingine (Nationalism).Waliokuwa wanahoji Muungano walikuwa wanaitwa wahaini.(REJEA KESI YA AKINA MALIM SEIF).Chama cha Wanannchi Cuf ni matokeo ya ubabe wa chama katika kushughulikia mambo ya Muungano.Hata Malim Seif,ambaye mimi namwona msaliti wa Wazanzibar,alionja joto la jiwe.

Kimsingi tukubaliane tu kwamba kulikuwa na makosa kadhaa katika namna ya kushughulikia kero za Muungano.Kutokana na udhaifu huo,ndio umezaa Zanzibar Nationalism,na sasa tunalazimika kuifufua Tanganyika.Wakati unabadilika.Waasisi wa Muungano walifanya kazi yao.Badala ya kuwalaumu,ni vema na sisi kizazi hiki tukatizama namna ya kushirikiana kama njia ya kutimiza wajibu wetu.Hatupaswi kuambiana maneno ya kuudhi,na kutumia neno ukoloni vibaya.Tuangalie historia,tuangalie mahitaji ya wakati huu na wakati ujao.

Suala la serikali tatu halijaanza leo.Tume ya Jaji Nyalali iliyoundwa na Rais Mwinyi mwaka 1992 kuangalia uwezekano wa kuanzisha vyama vingi,ilikuja na mapendekezo ya serikali tatu ikiwa ni njia ya kutatua kero za muungano ambalo hata hivyo halikutekelezwa.Mwaka mmoja baadaye kundi la wabunge lililopachikwa jina la G55 likaja na hoja ya serikali tatu,ambayo kimsingi bunge lilipitisha kabla ya Mwalimu Nyerere hajaizima hoja hiyo.(REJEA KITABU CHA “UONGOZI WETU NA HATIMA YA TANZANIA KILICHOANDIKWA NA MWALIMU NYERERE).

Mwaka 1998,Tume ya Jaji Mstaafu Kisanga iliyoundwa na Rais Mkapa ikaja na pendekezo la kuwa na serikali Tatu.Mambo yakawa yaleyale,pendekezo hilo likatupwa tena kapuni.Wakati ule,kama nilivyosema awali kujadili mambo ya Muungano ilionekana ni uhaini na hivyo kuzalisha manung’uniko mioyoni mwa watu.

Sasa Tume ya Mabadiliko ya Katiba nayo imekuja na wazo la serikali tatu.Kuna tofauti kubwa sana ,wakati ule na wa sasa.Kwa sasa wananchi wako huru kujadili suala la Muungano,hakuna vitisho.Lakini kwa upande wa Zanzibar hali ni tofauti.Katiba mpya kwao inamaanisha Muungano.Kuna wakati sauti zinasikika kutoka Zanzibar,kwa sasa ni wakati wa Zanzibar kutua mzigo.Japo ni wachache,lakini kuna watu wanaamini kwamba Zanzibar ni koloni la Tanganyika,na kwamba sasa ni wakati wa Zanzibar kupata “uhuru”.Sauti hizi zinatoka kwa viongozi wa chama na serikali,kuliko hata wananchi wa kawaida.

Hivi karibuni nilimsikia Ismail Jussa akiongea na idhaa ya Kiswahili ya DW,na kwamba sasa ni nafasi ya Zanzibar kupata mamlaka kamili,akitaja hasa Benki Kuu,Mambo ya Nje,Uhamiaji na Mambo ya Ndani.Tafsiri yake ni kwamba hapo hakuna Muungano.Huwezi kuwa kwenye Muungano na ukabaki na mamlaka kamili.

Binafsi napenda sana kumsikiliza Ismail Jussa akiongea mambo ya Muungano.Upendo wangu kwa Jussa hautokani na vile anavyojenga hoja,bali jinsi anavyoshindwa kuficha hisia zake na chama chake cha CUF.Kwa kiasi fulani nawafahamu Wazanzibar.Ukikutana na Mzanzibar msomi,utapenda jinsi anavyoongea taratibu,kwa umakini na kujenga hoja,huku akiwa na msimamo usiyoyumba kwenye masuala ya msingi.Sasa najiuliza,huo ndio mwisho wa zama za Zanzibar,kwa kuwa na vijana wanaopiga kelele badala ya kujenga hoja?

Tumeishi na Wazanzibar bila matatizo yoyote.Wazanzibar wengi wana makazi Tanzania bara kama ambavyo watu wa bara wana makazi Zanzibar.Tumeishi kama ndugu.Leo tunaposema Zanzibar ni koloni la Tanganyika,tunamaanisha nini?nini tafsiri yake?Mimi naona huu ni ubinafsi wa viongozi wetu wachache ambao wanataka kuneemeka kwa kuvunjika kwa Muungano.Na dhambi hii itaendelea kututafuna Waafrika.Wakati Mataifa yenye nguvu dunia yanaungana,sisi tunaona kujitenga ndio muhimu.

Bara la Afrika tuko nyuma sana kimaendeleo kuliko vile ninavyoweza kusema,hivyo umoja ndio unaweza kutusaidia kama Nkrumah na Mwalimu walivyoona miaka 50 iliyopita.Umuhimu wa Afrika kuungana leo ni mkubwa zaidi kuliko hata zama za Nkrumah.Sasa tunapojadili suala la Muungano,hebu tuangalie kwa jicho la mbali.

Mimi napinga mfumo wa serikali Tatu na badala yake tuwe na serikali moja tu.Kimantiki mfumo wa serikali tatu,unamaanisha unavunja Muungano.Pili kuendesha serikali Tatu katika hali tuliyonayo,ya uchumi dhaifu,ni kuleta mzigo mkubwa kwa walipa kodi,na utachelewesha maendeleo.Tatu,lengo letu liwe kuelekea kwenye Muungano wa Afrika.Hivyo ni vema tukawa na serikali moja,huku Tanganyika na Zanzibar tukizipa kisogo.

Ni jambo gani la kimaendeleo ambalo lilishindikana wakati wa serikali mbili,na sasa litawezekana kwa kuwa na serikali tatu?Je,kukwama kimaendeleo ya Tanzania,ni kwa sababu ya muundo wa serikali mbili?Wananchi wanachotaka ni maendeleo hata kama tungekuwa na serikali 20.Wananchi wengi wa kawaida hawana shida na Muungano.Tatizo lipo kwenye viongozi wachache ambao wanataka kuanzisha himaya za utawala kwa kuwa na viserikali vingi.Je,Zanzibar haijaendelea kwa sababu ya Muungano?

Ni vema wakati wa kutoa maoni yetu kuhusu Muungano,tutoe hoja na kuwasikiliza wengine.Kupiga kelele,hakuwafanyi watu wengine wakusikilize.Pia,wakati tunatoa hoja/maoni yetu kuhusu aina ya muungano tunaotaka,ni vema tukatumia lugha nzuri na za staha,huku tukiheshimiana.Kutumia maneno kama vile “ukoloni” si vizuri hasa ukiangalia tulivyoishi vizuri,kama ndugu.

IMEANDIKA NA BABA TUSAJIGWE (MUGO)
MAPAMBAZUKO TANZANIA
 
Ile dhambi ya "sisi" na "wao!" Yetu macho na masikio!
 
Mkuu
mwankuga unaposema "ukiangalia tulivyoishi vizuri,kama ndugu" unakuwa mnafiki. Mimi niliwahi kufika Zanzibar wakati fulani. Nilikuta mazuri ya kule kama vile kuelekezwa njia bila kuombwa hela. Lakini hawa watu si ndugu zetu. Kuna askari polisi alifikia mapenzi na binti wa kizenji akazaa naye katoto kazuri ka kike; ila ikatokea kuwa yule askari hakuwa muislamu. walitaka wamkate majambia. huyu askari alikuwa mtu wa kwetu. wenzake walimtoa zenji kwa zengwe moja hivi asirudi kule hadi alipostaafu. bahati pekee yule mpenzi wake afikicha picha yake mahala na siku ya siku alikuja muonesha binti yake sura ya babake na binti huyu akafanya kitu cha ajabu sana katika kumfuata baba yake. ni stori kama movie kabisa wangeijua kina kanumba. Yule binti alimpata babake Kyela. Huku bara tumeachia binti zetu wangapi waolewe na wapemba bila kuwafuata na mikuki?

Jengine ukiwa Zanzibar lazima ufunge wakati wa ramadhani. Hawa watu ni mataliban wakae kivyao na sisi tukae kivyetu!
 
pumba na mizunguko miiiingi tatizo nin unahitaji muungano na zanzibar, nimekusoma sana, bt huna jipya uloliongea mshaongea mengi tumeyasikia lakini hatutafuata, ni kawaida ya ukweli hua mchungu nyinyi ni wakoloni tena weusi
ubaya wa wakoloni nyinyi(blacks) mnaamini nyinyi si wakoloni bt ni ndugu, na vile vile mnaamini mnapasw kuikolonise zanzibar milele. hali hii imekua tofauti na mkoloni mweupe, yeye aliamini ni mkoloni ba kuna siku ataondoka kuacha uhuru kwa anaowatala.
nadharia hio imekufanyeni nyinyi watanganyika kua wavivu wa kufikiri na kudhibiti zanzibar ili kufanikisha ukoloni wenu huku mkitumia mgongo wa muungano kuprotect ushenzi wenu huu mbele ya uso wa dunia.
kipi kinawafanya mnganganie muungano hali ua kua wenyew hawataki? nini kinawafanya muikabe zanzibar kama si inaoitwa ukoloni? kipi kinawafanya kudhibiti harakati za mabadiliko visiwani zanzibar kama si ukoloni tena wa kishenzi, kwa nini muwachukie wanasiasa wenye mrengwa wa kupnga muungano na kuukosoa muungano kama si uo ukoloni? kipi kinachowashinda kutatua kero za muungano kwa muda wq miaka 50 kama si uo ukoloni?
leo hii mtatumia fedha nyingi kuutetea kuupigia debe na kuulinda lakini tayari umeshatoka kwenye vchwa vya wazanzibar walio wengi, na hawatobadilika bcoz wameshajua nia na malengo yenu mahasidi wa uhai wa wazanzibar.
leo hii ata mkisema msomi hawezi kupnga muungano hatutawasililizeni, kheri mtuone sote vilaza lakini si kusuport ukoloni wenu.
NYINYI NI WAKOLONI, TOFAUTI YENU NA WAKOLONI WALIOPITA NI KUA NYINYI NI WATU WEUSI WENZETU
 
Tanzania tuna tatizo la uongozi na siyo mfumo wa Serikali.
Sio kihivyo bali mimi naliangalia hivi: ukiangalia kwa miaka mingi nyuma unaiona Zanzibar kama kisiwa cha Mafia kwa maana kwamba wakaazi wake wa asili wanatokea bara (Tanganyika). Alafu historia inawaleta wafanyabiashara wa aina tofauti ikiwamo na ya utumwa hali iliyopelekea Sultan wa Oman kuhamishia makazi yake Zanzibar kama ilivyokuwa Kilwa kisiwani miaka ya mwanzoni. Ndio maana asili ya Wanzibari wengi (indigenous) ni mchanganyiko wa makabila.
Kwa maana hiyo Kijiografia ni sehemu ya bara na kihistoria inakuwa koloni la Sultani (Oman) hadi mapinduzi yalipofanyika.
Sasa angalia katika hili vuguvugu la kujitenga/kuungana:

  1. Baadhi ya Wazanzibar (sio vizuri kuwataja) wanataka wajitenge ili iwe rahisi kupata misaada ya nje hasa Oman ambao wanaweza kuweka kabisa makazi hapo mradi pesa imepatikana.
  2. Wengine wanapinga kurudi kwa ukoloni na kujiona wako sawa tu na hali iliyopo maana inawawezesha kushirikiana na ndugu zao wa bara bila vikwazo na wako tayari hata kwa serikali moja.
  3. Kundi la tatu ndilo lisilofaidika na siasa na hawagombei nafasi za utawala kama hayo makundi mengine lakini wanategemea upepo wenye kasi kutoka kwa hayo makundi mengine.

Kama ilivyokwisha kuelezwa hapo mwanzoni kuwa ili nchi iendelee inahitaji vifuatavyo:

  • ardhi
  • watu
  • siasa safi
  • uongozi bora

Inawezekana hivyo vitatu vipo na ndio maana Muungano ukawepo lakini hapo kwenye red ndicho kimekosekana sasa ikipelekea sababu ya yote haya kutokea.
Nchi zote duniani zinaungana kwa sababu kuna watu wa kuwaongoza kuwaunganisha. Kumbuka Canada walishataka kutengana eti kwa sababu upande mmoja unaongea Kifaransa na mwingine Kiingereza!!

Kinachotaka kufanyika sasa ni chuki za watu na njaa kwa ngazi ya binafsi na makundi na ndio maana hata wakitengana kama alivyosema Mwalimu utangano huo hautaishia hapo.
Tafakari kama haka kamchoro kanafanana na hali ya Zanzibar:
znz.JPG
 
Mkuu !! Eee eee ee, ee unasema hayo... Hapa watakuambia unataka kuwaleta masultani au walabu !! mmh ngoja usikie
hao hawapendi maneno hayo ya ukweli.
 
La Msingi Wazanzibari hawautaki muungano hata ungeimba mpaka asubuhi....
Sioni kwanini sisi Watanganyika tunawalazimisha.

Ivi tunafaida gani kiuchumi na hata kisiasa kuungana na hawa watu?

Pengine nielimishwe kwani naona hasara zaidi ya faida.
Tunatawala wote Tanzania bara lakini Tanzania visiwani marufuku na hata ukiwaita hivyo hawataki

Ngoja aje Barubaru na kina embe Boribo hapa wakutolee uvivu!!

Let Zanzibar go Let Uamsho go, tunaitaka TANGANYIKA YETU tuliyopewa na Mungu!
 
Last edited by a moderator:
Sio kihivyo bali mimi naliangalia hivi: ukiangalia kwa miaka mingi nyuma unaiona Zanzibar kama kisiwa cha Mafia kwa maana kwamba wakaazi wake wa asili wanatokea bara (Tanganyika). Alafu historia inawaleta wafanyabiashara wa aina tofauti ikiwamo na ya utumwa hali iliyopelekea Sultan wa Oman kuhamishia makazi yake Zanzibar kama ilivyokuwa Kilwa kisiwani miaka ya mwanzoni. Ndio maana asili ya Wanzibari wengi (indigenous) ni mchanganyiko wa makabila.
Kwa maana hiyo Kijiografia ni sehemu ya bara na kihistoria inakuwa koloni la Sultani (Oman) hadi mapinduzi yalipofanyika.
Sasa angalia katika hili vuguvugu la kujitenga/kuungana:

  1. Baadhi ya Wazanzibar (sio vizuri kuwataja) wanataka wajitenge ili iwe rahisi kupata misaada ya nje hasa Oman ambao wanaweza kuweka kabisa makazi hapo mradi pesa imepatikana.
  2. Wengine wanapinga kurudi kwa ukoloni na kujiona wako sawa tu na hali iliyopo maana inawawezesha kushirikiana na ndugu zao wa bara bila vikwazo na wako tayari hata kwa serikali moja.
  3. Kundi la tatu ndilo lisilofaidika na siasa na hawagombei nafasi za utawala kama hayo makundi mengine lakini wanategemea upepo wenye kasi kutoka kwa hayo makundi mengine.

Kama ilivyokwisha kuelezwa hapo mwanzoni kuwa ili nchi iendelee inahitaji vifuatavyo:

  • ardhi
  • watu
  • siasa safi
  • uongozi bora

Inawezekana hivyo vitatu vipo na ndio maana Muungano ukawepo lakini hapo kwenye red ndicho kimekosekana sasa ikipelekea sababu ya yote haya kutokea.
Nchi zote duniani zinaungana kwa sababu kuna watu wa kuwaongoza kuwaunganisha. Kumbuka Canada walishataka kutengana eti kwa sababu upande mmoja unaongea Kifaransa na mwingine Kiingereza!!

Kinachotaka kufanyika sasa ni chuki za watu na njaa kwa ngazi ya binafsi na makundi na ndio maana hata wakitengana kama alivyosema Mwalimu utangano huo hautaishia hapo.
Tafakari kama haka kamchoro kanafanana na hali ya Zanzibar:
View attachment 97112
Mh. Umujubi good day;
Mkuu uliyochambua ni sawa tu, Sasa kwenye RED!! suali ni je, hapa nchini Tanzania hiyo ipo? au mkuki kwa nguruwe?
uhuru miaka 52 leo kwa macho yetu wenyewe tunaona tulipofika!!!!! Umetaja Uongozi bora = mie nakuambia UONGO + Zengwe + Ufisadi.
 
kama nilivyosema hii nchi ilikuwa moja na sasa no matter ni sababu za kijiografia, kiuchumi, kisiasa, kiuongozi au vyovyote vile, ilifika sehemu ikawa nchi mbili tofauti. Kiungwana na hasa kuangalia asili ya binadamu inabidi tuungane lakini kama upande mmoja hautaki huo muungano basi hakuna haja ya kulazimishana bali historia itatueleza ukweli huko mbeleni. Na Muungano mzuri ni wa serikali moja tofauti na hapo ni kuongeza gharama bila sababu kwa nchi masikini kama hii.

Kwanii msiungane na Rwanda kwa Kagame?
Hicho kisiwa cha watu 700,000 tu kinawashindeni
  • kimechukua madaraka yote hadi huku bara,
  • Wamechukua Biashara zote hadi huku bara
  • Kila siku wanaonewa wanataka nafasi zaidi maofisini
  • Wanataka zaidi,
  • Ardhi na maeneo ya kulima wakati Visiwani Mbara huruhuziwi
    • Hapo ni Nchi mbili Wabara hamfurukuti ETI SASA MNATAKA IWE NCHI MOJA TU, kwa kigezo gani hasa DINI au ni huo uOMAN
 
Mkuu
mwankuga unaposema "ukiangalia tulivyoishi vizuri,kama ndugu" unakuwa mnafiki. Mimi niliwahi kufika Zanzibar wakati fulani. Nilikuta mazuri ya kule kama vile kuelekezwa njia bila kuombwa hela. Lakini hawa watu si ndugu zetu. Kuna askari polisi alifikia mapenzi na binti wa kizenji akazaa naye katoto kazuri ka kike; ila ikatokea kuwa yule askari hakuwa muislamu. walitaka wamkate majambia. huyu askari alikuwa mtu wa kwetu. wenzake walimtoa zenji kwa zengwe moja hivi asirudi kule hadi alipostaafu. bahati pekee yule mpenzi wake afikicha picha yake mahala na siku ya siku alikuja muonesha binti yake sura ya babake na binti huyu akafanya kitu cha ajabu sana katika kumfuata baba yake. ni stori kama movie kabisa wangeijua kina kanumba. Yule binti alimpata babake Kyela. Huku bara tumeachia binti zetu wangapi waolewe na wapemba bila kuwafuata na mikuki?

Jengine ukiwa Zanzibar lazima ufunge wakati wa ramadhani. Hawa watu ni mataliban wakae kivyao na sisi tukae kivyetu!
Mkuu, hayo ni yote ni ya kijamii hata hapa nchini mengi kama hayo hutokea kila leo!! tusichukulie mambo madogo madogo... tafadhali tumezee mangine!!
 
Mkuu, hayo ni yote ni ya kijamii hata hapa nchini mengi kama hayo hutokea kila leo!! tusichukulie mambo madogo madogo... tafadhali tumezee mangine!!

He, weee. dogo hilo? katoto ketu kamepata taaabu sana kumfuata babake. we unaona dogo hilo? na kasingekuwa na ujasiri wa kwetu mbeya kangefika? acha izo bwana....
 
Back
Top Bottom