Je YouTube itakufanyaje uwe milionea?

sley_mwombeck

New Member
Jul 16, 2021
4
3
MAKALA: MJASILIA MALI KUWA MILIONEA NA YOUTUBE
youtube ni nini?
YouTube ni tovuti ya kushirikisha video ambazo watumiaji wanaweza kuzinakili na kuzigawa kwa wengine. Wafanyakazi watatu wa zamani wa PayPal waliunda YouTube mnamo Februari 2005. Mnamo Novemba 2006, YouTube, LLC ilununuliwa na Google Inc kwa Dola bilioni 1.65, na sasa huendeshwa kama shirika dogo la Google.
Je YOUTUBE itakufanyaje uwe milionea
kitu Muhimu kinacho hitajika ni simu yako ya mkononi(smartphone) tablet au komputa (komputa ya mezani au mpakatao(laptop) na bando la simu la kukuwezesha wewe mjasilia maji kuwa milionea kwa kutumia simu yako twende sasa……

hapa nitaongelea sehemu 10 tu za ujasilia mali ambazo ukichagua fulsa moja inakufanya milionea.
1. MGAHAWA/MAMA NTILIE
A.Muonekano wa sehemu yako ya kazi pia unaweza kujifunza youtube jinsi ya kufanya mazingira yako yawe mvuto kwa wateja wako bila kutumia gharama kubwa ila ubunifu wa kuwateka wateja wako kwa kutumia youtube tu mfano angalia hii link jinsi ya kutengeneza mgahawa wako kuwa na muonekano wa kuvutia kwa wateja


B.kama mama ntilie unayo fulsa kubwa ya kuliteka soko la huduma yako mahali ulipo kwa kutumia youtube peke yake.
youtube utajifunza jinsi ya kumkaribisha mteja, itakusidia wewe kutengeneza mvuto wa sehemu yako pia na kuongeza wigo wa huduma yako.. mfano link jinsi ya kukarbisha mteja



C. mgahawa wako sasa uko na mvuto(mazingira) uko na wahudumu wanaojuwa kuongea na wateja vzuri lazma ujuwe jinsi ya kuandaa MENU ili kumsaidia mteja kufanya chaguo sahii na kwa mda mfupi mfano link

D.youtube pia utajifunza jinsi ya kuandaa chakula tofauti tofauti pia na kujifunza mapishi mapya na kupika chakula cha tofauti na kuonekana uko wa tofauti na na yeyote mfano jinsi ya kupika biryani pia jifunze kutenga siku mbili au 1 kwa wiki kupika chakula tofauti itakusaidia kuweka wateja wako atention, pia zingatia sana usafi wa vyakula vyombo na mazingira ya ndani na nje itaongeza mvuto zaidi katika sehebu yako ya kazi


2.WASHONAJI WA NGUO(DESIGNES)
kila mtu anaweza kuwa mshonaji wa nguo ila sio kila mshonaji wa nguo atakuwa atakuwa desginer mzuri lakini kwa kutumia youtube tu unaweza kuwa fundi mahili sana na ukawa milionea
A. njia rahisi ya kujifunza kushona suti mbalimbali kwa mitindo tofauti tofauti kwa kutumia youtube pekee na kujuwa ni aina gani ya suti za kiume zinavutia zaidi mfano link hii

B. kuandaa nguo za mabibi harusi.. kushona kupamba na kila kitu kuhusu aina iyo ya nguo yote yanapatikana youtube mfano link hii



3.KUWA BINGWA WA KUPAMBA KUMBI ZA SHEREHE
you tube inakufundisha yote hayo jinsi ya kupamba vzuri na mitindo mipya ya upambaji mfano linki hii


4. KUWA MPIGA PICHA BORA
youtube ina kila aina na kujifunza hatakama ujawahi kupiga picha mahali popote ila youtube itakufundisha A to Z na unaweza kuwa milionea kwa kazi iyo kwa kutumia youtube tu mfano link hii hapa


ni youtube peke yake inaweza kukupa maarifa yote ayo kama umechagua kuwa photographer au camera man


5. WASUSI WA NYWELE NA MAKE UP ARTIST
ni youtube pekee inayoweza kukufanya kuongeza kipato chako ww ni msusi wa nywele kwa kujifunza aina mbali mbali ya kutengeneza nywele ili kuwavutia wateja wako mfano link hii


pia makeup artist hatakama hujui utaanzia wapi au utaanzaje youtube inakupa fulsa ya kufanya hvo pia kuanzia kujifunza mpaka kuwa bora zaidi
hata kama ww tayari mjasilia mali na uko mtengeneza mekup mzuri pia youtube inakupa fulsa ya kuongeza wigo wa ujuzi bure kabisa link



6.KUJIFUNZA KUUZA NA KUNUNUA BIDHAA TOKA NJE
pia youtube inakupa fulsa ya kujifunza fulsa ya kuagiza bidhaa toka njee sio mpka uwe na ofisi au mtaji mkubwa hapana ila unaweza tengeneza mazingira na kuweza kuagiza bidhaa za watu au kuwagizia watu bidhaa kwa kujifunza kutumia youtube bure kabisa na ukaingiza kipato kizuri mfano jinsi ya kuagiza bidhaa za jumla na reja reja kutoka china kupitia kampuni ya alibbaa https://youtu.be/GOSNSlwuLRA


7.KUJIFUNZA KUUZA NA KUNUNUA FEDHA ZA KIGENI (FOREX)
watu wengi wanaingiza pesa wamekuwa mabilionea kwa kufanya hii biashara ya kuuza na kununua fedha za kigeni maalufu kama FOREX.. uzuri wa hii biashara unaweza kufanya hata ukiwa umelala nyumbani kwako na ukaingiza kiasi kikubwa cha fedha.. hakuna pesa inayokuja kiulahisi lazima upambane usisubiri ajira fanya forex sasa hata kwa kujifunza mwenyewe kupitia youtube mfano link
https://youtu.be/bWW3f0nCQLU
https://youtu.be/hX-appWESLg


8.UFUGAJI WA KUKU KISASA
wewe kama ni mjasilia mali wa kufuga kuku na ufugaji mbalimbali youtube itakufunza mengi na ambayo ujawahi kusikia kuhusu ufugaji wa kuku.. iwe wa nyama au wa mayai yote hayo utayapata youtube bure kabisa mfano link
https://youtu.be/8gVX7QtBfMM
https://youtu.be/1FQbHOtizvk


9.LIMA KISASA MAZAO YANAYOKUA KWA MDA MFUPI NA KWA NJIA ZA KISASA
kila utakacho utakikuta youtube ni wewe na matakwa yako yakoje
ulimaji nyanya kisasa link https://youtu.be/sexoTj5WjKk
ulimaji vitunguu kisasa
https://youtu.be/zRzDTrovOY0
ulimaji matikiti kisasa
https://youtu.be/hMHv5fwSY8k
https://youtu.be/TB4Mh83IwUM
nimekuwekea machache ayo ila unaweza tafuta mengi youtube na ukajifunza Mengi na ukapiga pesa ndefu kwa kutumia kilimo na technologia


10.UUNZI WA FANITURE ZA NDANI UREMBO WA NYUMBA DIZAIDI ZA KISASA NA MUONEKANO MZURI WA NYUMBA
kwa mafundi faniture, mafundi ujenzi, wakupaua miezeko mbali mbali design za ndani ya nyumba yote ayo yanapatikana youtube na kwa kutumia youtube unaweza ongeza maarifa mengi ukaongeza kipato zaidi ukatengeneza wateja wengi pia unaweza kuwa milionea kwa kutumia youtube tu mfano links mbalimbali hapa
dizaini za muonekano wa nyumba ndani
https://youtu.be/y7_Spedf2BI
dizaini za jikoni
https://youtu.be/BoOUZ6jGhl4
dizaini ya muonekano wa juu
https://youtu.be/oz3C5tjOoUc
na mengine mengi utajifunza youtube na kuingiza kipato kikubwa cha fedha..



ZIPO NJIA NYINGI MNO ZA KUINGIZA KIPATO NA KUKUZA UJUZI NA UFANISI WAKO KUPITIA YOU TUBE, LAKINI YOTE HAYO FANYA UKIMUOMBA MUNGU NA UKIMUAMINI PIA ATAKUONGEZEA MAAARIFA NA UTAFANIKIWA.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom