Je, Wewe upo kwenye kundi gani kati ya haya?

Galacha Maestro

JF-Expert Member
Sep 29, 2011
1,353
2,227
JE WEWE UPO KWENYE KUNDI GANI KATI YA HAYA?

Kuishi ni hatari, ndio kila siku tunakutana na hatari mbalimbali, lakini hatuachi kuishi.Katika maisha tunakutana na hatari mbali mbali, kuna ambazo tunaweza kuziepuka na kuna ambazo hatuwezi kuziepuka.

Kuna hatari moja ambayo wengi wetu huwa tunafikiri tunaweza kuiepuka au kuikwepa na hivyo kukazana kuikwepa, na mwishowe tunajikuta tunahangaika na kitu ambacho hakiwezekani.Hatari hii ni kufanya makosa, hata ungekazana kiasi gani, bado utafanya makosa na katika hatari hii ya kufanya makosa tunapata makundi mawili ya watu.

KUNDI LA KWANZA
Wale wanaofanya maamuzi yao kuepuka kufanya makosa. Hawa hukazana kuhakikisha hawafanyi makosa, hawapotezi na kwa njia hii hujikuta wakikosa fursa nzuri za kunufaika zaidi.

KUNDI LA PILI
Wale wanaojua makosa yapo ila wanakazana kuyapunguza hawa wanajua huwezi kukwepa kabisa makosa, badala yake unaweza kuyapunguza, kwa kuwa na maarifa sahihi na kuchukua hatua wakati sahihi hwa hunufaika sana kwa sababu huzichangamkia fursa wakati wengine bado wanaogopa kuchukua hatua.

Watu hawa wa kundi la pili sio kwamba hawaogopi au wanajitoa kichwa kichwa, ila wanakuwa na maandalizi ya kutosha na hivyo kupunguza sana hatari ya kufanya makosa.
 
mimi niko namba 2 mkuu.

kuna slogan moja huwa naitumia na huwa inanisaidia sana.

inasema:if you don't take risk you will end up working for others in your life.

so myself am a risk taker and i don't blame myself on the outcome.
 
halafu wewe ni ndugu na Paulo de serge nini? maana siku hizi simuoni akitupiamo vile vitu vyake badala yake umekuja wewe.

always cherish your posts.
 
mimi niko namba 2 mkuu.

kuna slogan moja huwa naitumia na huwa inanisaidia sana.

inasema:if you don't take risk you will end up working for others in your life.

so myself am a risk taker and i don't blame myself on the outcome.

Safi sanaaaa...
 
Mm nipo hilo la Pili makosa nayaona mengi ila najalibu pia kuyapunguza mengine yananishinda kutoka na watu walionizunguka
 
Back
Top Bottom