Je, Wewe umepitia na kukulia kwenye TOXIC parenting?

One of the fact that opened my eyes
It say
“No one likes you and if they like you it’s for a reason, without that reason no one likes you and they hates you when you act real

The one who Truly loves you is God”
 
Safi sana.. naamini hawakuwa toxic mkiwa wadogo? Isn't it?
Hapana walikuwa watu poa sana ila wakali kwa mambo ya kipuuzi. Mama yetu ametunyoosha sanaaa, ila no matusi wala kuitwa majina ya ajabu.
Familia toxic nimekuja kukutana nayo ukubwani, familia ya mume wangu, yaani vurugu mechi mambo ya ajabu ajabu nimeshangaa hadi nimewazoea😀. Na ni walokole
 
Toxic people hujifanya sana ni wacha Mungu na hutumia hiyo kama "cover up".. Hii kitu nimewahi soma pia kwenye riwaya moja ya kinaijeria inaitwa "purple hibiscus"..
 
Yaani wanakuvuruga unaweza ukaanza kufanana nao. Wamenifanya hadi nimekuwa nunda wakati nilikuwa mtoto mzuri
 
Imekuathiri vipi kwa maisha yako ya ukubwani?.
Je umekulia kwenye familia ambapo wazazi
  1. Walikuwa na excessive controls na kukudhibiti kwa kila hatua yako ya ukuaji kiasi cha kukuathiri kisaikolojia?
  2. Wanatumia njia ya kukunyima chakula, kukunyima usingizi na kukufanyia body Shaming kama adhabu pale unapokosa hata kama kosa lenyewe ni dogo?
  3. Wanakutumia kama kama njia ya kujiingizia kipato kwa njia ya udanganyifu n.k?
  4. Ambao walikufanyia bullying na kukutukana na kukutamkia maneno mabaya kiasi kwamba yana ku "Hunt" hadi leo?
  5. Ambao walikuwa wanakuadhibu kwa njia za kikatili mfano kupigwa kichwa kikiwa chini miguu juu ?
  6. Ambao walikunyanyasa na kukudhulumu kingono? (Hususani kwa wale waliokuwa na wazazi wa kufikia :step family)
  7. Wakijamba wakubwa wewe mdogo unaangushiwa kipigo heavy?🤨🤨
Hakika Maisha ya Afrika hususani kwenye swala la malezi ya watoto tumefeli..
Tupeane uzoefu na kuhusiana na mada na njia za kudhibiti toxic parenting .
View attachment 3445393
Mimi nashukuru sijapata wazazi waliofikia hapa wala sijawahi kunyimwa chakula au mambo yaliyokithiri. Lakini viboko kutoka kwa mama nimevipata sana. Matokeo yake, leo hii siwezi kabisa kumwelekeza mwanangu kwa njia nyingine zaidi ya hiyo niliyoishuhudia. Ni mtu mwenye maelekezo ya hasara, ninachapa sana watoto na bado sidhani kama wamenyooka. Sijui namna ya kuongea nieleweke bila kuwapiga. So, mara nyingi kama mama sina furaha maana najua nawaumiza lakini pia sitaki wapotee. Sad
 
Ndo ule msemo wa mtoto umleavyo ndo akuavyo..
Yani wazazi walikulea kwa fimbo aoutomatically na ww ukaiga na ku adapt huo mfumo...
Yani inabidi sana ujitahidi kujicontrol
 
Una tatizo la kiakili ambalo umepewa na wazazi wako,usishtuke ndio ilivyo.
Anza kufuatilia haya mambo kisha taratibu brain structure yako itaanza kukunjuka na kuona kwamba hiyo sio njia sahihi
 
Ndo ule msemo wa mtoto umleavyo ndo akuavyo..
Yani wazazi walikulea kwa fimbo aoutomatically na ww ukaiga na ku adapt huo mfumo...
Yani inabidi sana ujitahidi kujicontrol
Sana, sana. Sasa unawaza ufanyaje maana sio kwamba hawakosei. Wanakosea sana na ninajua sipaswi kukaa Kimya, ila je nifanye nini? Sina mbinu za kuwaelekeza.
 
Wazazi/walezi wa kibongo hudhani watoto wote ni wachangamfu, ni waongeaji, wapenda michezo nk ni ngumu sana mzazi kumsoma mwanae.

Kama ni mpole, ataitwa mzembe mzembe, kazubaa na kuna vitu hatapata kwa kua hivyo alivyo.

Wazazi wa kibongo wana namna yao ya tofauti sana ya kuonesha upendo.
 
Back
Top Bottom