JE WEWE NI MWENYE HUZUNI?
Ikiwa ni fakiri basi kuna wenzako wamefungwa kwa sababu ya madeni. Ikiwa humiliki kifaa cha usafiri kuna wenzako hawana miguu miwili. Ikiwa unasumbuliwa na maumivu kuna wenzako wanamiezi au miaka vitandani.
Ikiwa kama umefiwa na mtoto kuna wenzako wamepoteza watoto katika ajali moja. Usihuzunike! Maadamu wewe ni muislamu au Mkristo umemuamini Mwenyezi Mungu na malaika wake vitabu vyake, mitume wake, siku ya mwisho na mipango na makadirio ya Mungu.
Usihuzunike! Kwani kuhuzunika kwako huwezi lisimamisha jua wala kuurudisha muda nyuma. Usihuzunike maadamu wamiliki dua na Maombi na una theluthi ya mwisho ya usiku,muda ambao dua ya mja hairudishwi,muombe Mola wako. Usihuzunike! Kwani Allah kakuumbia ulimwengu na vilivyomo, miongoni mwa mabustani mazuri na anga lenye kupendeza.
Usihuzunike maadamu wapata kuingiza chochote mdomoni mwako na kuvuta hewa nzuri. Hujaona ni jinsi gani mawingu mazito yanavyo ondoka kwa kushuka na rehema ya mvua kwa waja,na usiku wenye kiza chenye kutisha ni jinsi gani waondoka na kuingia asubuhi yenye kupendeza!
Usihuzunike yafurahie maisha yako kama atakavyo Muumba wako.
Champion Harufu, hebu tupe mbinu za kuwa mtu mwenye furaha.....
Mkuu HARUFU Kwa hayo Maneno uliyoyasema basi utafanikiwa katika Maisha yako yote hapa duniani hongera sana.Kitu cha kwanza kabisa namuweka Muumba wangu mbele. Kwa lolote au kwa chochote kinachotokea au kitakachonitokea najua ni kwa ajili yake yeye ametaka iwe hivyo na ni kwa ajili ya kudra zake, hilo halina mjadala hata kidogo.
Nashukuru Mkuu... umenifaa na kunizindua mambo mengi!!Kitu cha kwanza kabisa namuweka Muumba wangu mbele. Kwa lolote au kwa chochote kinachotokea au kitakachonitokea najua ni kwa ajili yake yeye ametaka iwe hivyo na ni kwa ajili ya kudra zake, hilo halina mjadala hata kidogo.
Sikatai, mimi ni Binaadam kama Binaadam mwingine yoyote yule, kwahiyo mapungufu lazima yawepo na hii yote ni kutokana na udhaifu wa kiBinaadam sababu mimi si Malaika. Kwahiyo nina mapungufu yangu mengi sana ambayo siwezi nikajifanya kuyaficha nyuma ya pazia ili nionekane mbele ya uma kuwa mimi ni mtu mwema, hapana. Mimi napenda sana maisha ya uhuru, na kujiachia.
Na kingine mimi ni mtu wa kupotezea(au sijui kwa Swahili fasaha niwekeje, ila bila shaka unanifahamu vizuri sana, kumradhi kama nitakuwa natumia maneno/lugha ya/za mitaani). Nikiwa na maana kwamba labda mathalani nilipoteza/niliibiwa/niliteketezewa Mali au Haki yangu, kwa kweli kwa kiBinaadam inauma sana ila pamoja na yote itaniuma siku chache za mwanzo tu, baada ya hapo(baada ya kipindi kifupi) nakubali matokeo, na naendelea na maisha yangu. Au kwa lugha nyingine mimi ni mtu wa kuchukulia poa.
Pili naishi hapa Ulimwenguni nikijua fika siku yoyote nauacha huu Ulimwengu(Dunia mapito) kwahiyo niko tayari muda wowote na kwa roho kunjufu siku yangu ikifika niachie ngazi.
Tatu, kwa leo ntaishia hapa vinginevyo ntakuchosha kwa maelezo marefu.
Mimi ni mtu ambae nazingatia sana michezo na napenda sana michezo, na mazoezi kwa ujumla