Herbalist Dr MziziMkavu
Platinum Member
- Feb 3, 2009
- 43,069
- 34,839
JE WEWE NI MWENYE HUZUNI?
Ikiwa ni fakiri basi kuna wenzako wamefungwa kwa sababu ya madeni. Ikiwa humiliki kifaa cha usafiri kuna wenzako hawana miguu miwili. Ikiwa unasumbuliwa na maumivu kuna wenzako wanamiezi au miaka vitandani.
Ikiwa kama umefiwa na mtoto kuna wenzako wamepoteza watoto katika ajali moja. Usihuzunike! Maadamu wewe ni muislamu au Mkristo umemuamini Mwenyezi Mungu na malaika wake vitabu vyake, mitume wake, siku ya mwisho na mipango na makadirio ya Mungu.
Usihuzunike! Kwani kuhuzunika kwako huwezi lisimamisha jua wala kuurudisha muda nyuma. Usihuzunike maadamu wamiliki dua na Maombi na una theluthi ya mwisho ya usiku,muda ambao dua ya mja hairudishwi,muombe Mola wako. Usihuzunike! Kwani Allah kakuumbia ulimwengu na vilivyomo, miongoni mwa mabustani mazuri na anga lenye kupendeza.
Usihuzunike maadamu wapata kuingiza chochote mdomoni mwako na kuvuta hewa nzuri. Hujaona ni jinsi gani mawingu mazito yanavyo ondoka kwa kushuka na rehema ya mvua kwa waja,na usiku wenye kiza chenye kutisha ni jinsi gani waondoka na kuingia asubuhi yenye kupendeza!
Usihuzunike yafurahie maisha yako kama atakavyo Muumba wako.