Je, wewe ni bei gani?

Je, wewe ni bei gani?

Equation x

JF-Expert Member
Joined
Sep 3, 2017
Posts
41,758
Reaction score
65,393
Tunaajiriwa kwa sababu tunauza ujuzi au huduma kwenye shirika au taasisi husika.

Ifikapo pale huduma isipohitajika, maana yake haitanunulika na kama ni bidhaa inayoharibika, itabidi kuacha ioze au kuiuza kwa bei ya hasara.

Mishahara tunayolipwa inatafsiri thamani ya uwepo wako kazini, kama unalipwa elfu hamsini, tafsiri yake bei yako wewe ni elfu hamsini. Na kama unalipwa milioni mbili, tafsiri yake wewe bei yako ni milioni mbili n.k

Mfano; kuna mtambo mmoja ulinunuliwa kutoka nchi x,kwa ajili ya kuja kufanya uzalishaji wa bidhaa za chuma, wakati ule mtambo ukizalisha zile bidhaa ukapata hitilafu; kwa mazingira yale hakuna mtu aliyeweza kutatua ile changamoto ingawa mabingwa wao wabobezi ma injinia waligusa hapa na pale na ikawa bila bila, ikabidi uongozi wa kiwanda uwasiliane moja kwa moja kwa waliowauzia mtambo; wauzaji wa mtambo wakasema tutawatumia mtaalamu wetu, itabidi mmlipe usafiri wa kutoka na kurudi huku nchini kwetu,mgharamie malazi, chakula, usafiri, na pia posho zake.

Wenye kiwanda wakakubali, jamaa baada ya kufika akosoma 'signal' tu ya ule mtambo, akaenda moja kwa moja sehemu ya 'button' ya kijani; ile kugusa tu mashine ikawaka na ikaanza kupiga kazi; hakutumia ata dakika 5, jamaa akasema alipwe pesa zake aondoke. Wenye kiwanda wakaanza kugoma, inakuwaje tukulipe hela zote hizo kwenye kitu ulichokifanya ndani ya dakika 5?

Mtaalamu akawajibu, ''utaalamu wangu nilijua wapi pa kugusa kutokana na 'signal' husika; kama msingenihitaji nanyie mngetafuta ujuzi wa kujua wapi pa kugusa.''

Ilibidi wamlipe pesa alizostahili; bei yake ndio ile pesa aliyolipwa.

Je, wewe ni bei gani?​
 
Tusiojariwa bei yetu ni kama ifuatavyo Figo moja Tsh 70,000 * 2=Tsh 140,000,000/= hapo sijaweka Vidole na Vinginevyo kama Kuuuza Roho alsmost kama Us Million 2 kwa sisi maJobless
Kutokuajiriwa wakati mwingine inatafsiri, bei yako ni kubwa ndio maana hujaajirika kwa malipo madogo; wapo waliokataa mishahara na wakafanya mambo yao na sasa ni watu wakubwa duniani. Wale bei zao ni kampuni wanazozimiliki.​
 
Tusiojariwa bei yetu ni kama ifuatavyo Figo moja Tsh 70,000 * 2=Tsh 140,000,000/= hapo sijaweka Vidole na Vinginevyo kama Kuuuza Roho alsmost kama Us Million 2 kwa sisi maJobless
kwa hesabu hizi unaajiriwaje sasa mkuu. ili ukalete hasara
thamani yako ni negative
70,000 *2 inakujaje milioni 140?
 
Vipi wale wanaohonga ili wapate kazi
Ile ni bidhaa iliyokaribia kuoza, inapambana iweze kununulika sokoni; lakini inakuwa haina ubora. Ni sawa na kuuziwa samaki kwa bei kubwa, baada ya kufika nyumbani unagundua umeuziwa kitu kilichooza.​
 
Back
Top Bottom