muhandu
JF-Expert Member
- Sep 25, 2011
- 311
- 84
Salama wana MMU.
Kitu mahusiano,mapenzi au urafiki (MMU) wa karibu kama watu wanavyopenda ifahamike pale kinapokolea kati ya watu wawili hasa nazungumzia jinsia mbili tofauti yaani -me na -ke,kwa kawaida hupofusha na kufurahiwa na wahusika kwa wakati huo.Lakini naweza kusema asilimia kubwa ya wahusika mmoja wapo huwa na ndoto za kuja kuishi pamoja muda muafaka ukifika,na mwingine anachukulia kama vile anajiburudisha na kufanya mazoezi tu, huku akijua kuwa iko siku atamwacha mwenza wake na kuchukua hamsini zake na kutafuta mwingine.Kana kwamba hawakuwa na mahusiano yoyote.Haya huitwa mapenzi ya pande moja.Adhari zake ni kubwa kwani wengi wamefikia kuchukua uamuzi mzito hata kujiua.(mapenzi niue)
Samahani kwa kabila nitakalo tolea mfano,siyo ndiyo kwamba wao wana tabia hiyo,la hasha bali nataka kufikisha ujumbe kwa kizazi hiki cha dot com na wanachama wote wa jf ili tujifunze kitu Fulani.NA HII NI HISTORIA YA KWELI.
Katika hali ya kawaida ilitokea nikawa najiuliza ni vipi mtu anaweza kuahama kabila lake na kuwa kabila lingine?nimegundua ni kweli ingawa ni chungu kukubali.Sikia hii:
Bibi yangu kabla ya kuolewa na babu yangu enzi hizo alikuwa na m m u na kijana mmoja wa kipare ambaye alikuja kijijini pale kufanya biashara.Bibi na huyo kijana wa enzi hizo waliendelea kuwa marafiki kwa muda murefu.Kumbuka bibi wakati huo alikuwa ni binti wa BABA mchungaji wa dhehebu Fulani ambalo lina amini katika mke mmoja na mume mmoja.Na kwakuwa walikuwa wamefunikwa na kitu mapenzi haikupita muda kujafahamu kuwa ni mjamzito wa miezi miwili.
Ilikuwa ni mshike mshike kwani baada ya siku chache MAMA mchungaji akaja jua kuwa binti yake kanasa,na kwa kutafuta muafaka BABA mchungaji akafahamishwa,ALISHTUKA,AKATAHARUKI LAKINI WAZEE WENYE BUSSARA WAKAMPOZA.Akatulia na ili kuona ni jinsi gani watatatua jambo hilo.Vikakaa vikao vya siri nyakati za usikuna,muafaka ukafikiwa kuwa atafutwe mchumba ambaye ataokoa aibu hiyo bila ya yeye mwenyewe kujua ni nini ambacho kinaendelea..
Kwa wakati huo babu yangu alikuwa ni mfanya biashara mkubwa sana mwenye mali ya kutosha na ushawishi mkubwa tu kijijini kwao yaani mmakonde mjanja mwenye wake wawil na watoto kadhaa,na bibi akajakuwa ni mke wa tatu.Kwa hiyo katika pitapita yake babu akasonteshewa kuwa kuna binti mchungaji anatafuta mchumba,kwa ukwasi aliokuwa nao akaona ni sawa kiongeza mke mwingine tena mtoto wa mchungaji!Basi akaingia kichwa kichwa akabeba mzigo,akatoa mali aliyoambiwa na kubeba mke wake mpaka kijijini.maisha yakaendela na hatimaye siku ikafika bibi akajifungua mtoto wa kiume.Akapewa majina ya kabila la babu la wamakonde.Ikawa asubuhi na ikawa jioni,siku mpya ikaja na mara siku mara wiki na miaka ikaenda.
Wadadisi wa mambo walijiuliza ni kwanini binti ya mchungaji akaolewa mitala-yaani mke na mtu mwenye wake wengi.Kuwa mke watatu?kwanini?kwa wenye akili walijua kuwa tayari mambo yalikuwa yameharibika.Maana siyo kwamba walikuwa hawajui ni nini kilichokuwa kinaendelea kati yake na kijana wa kipare.
Sasa mimi nilizaliwa mama akiwa shule,basi nilikuwa kwa mama maneno yakaanza kuwa Yule ambae ninamwita baba yangu hakuwa baba yangu mzazi.Udadisi ukaingia kichwani nikaanza kufanya uchunguzi na hatimaye nikangamua kitu.Nikaamua kwenda kule ambako walisema ni kwetu kwa baba yangu mzazi.Yaani orijino yangu,basi kufika kule nikamkuta bibi na babu wakanifurahia na kusema nafanana sana na baba yangu.Nikatambulishwa kwa ndugu na jamaa zangu ambo walikiri kuwa mimi ni mtoto wa pale.Maisha yakaendelea nikawa nashiriki kazi za pale utadhani nilikuwepo tokea siku nyingi kama kawaida,ila siku moja tukiwa tunaongea na bibi,aliniangalia sana na kusema `MTOTO WA KIPARE HUYUniliposikia hivyo ikakaa kichwani na nikajiuliza sana kwani nini aseme hivyo?Ina maana anajua kuwa mama alikuwa na mahusiano na kijana wa kipare na ni hivyo kwani nini walinipokea??Nikameza kama ilivyo na kukaa nayo moyoni.
Basi nikawafahamu ndugu za baba,lakini kila nikiwaangalia naona kuna tofauti sana,ingawa ni sawa kitu kama hicho kutokea kwani baiolojia inaweza kusema au kufafanua vizuri sana swala hilo.Basi nikaanza kuuliza na kutafuta nini kipo nyuma ya pazia.Ndiyo nikafahamu kuwa ingawa baba yangu ni mmakonde kumbe ndani yake ni mpare,Na baba yake halisi ambaye ni mpare aliamua kukaa kimya sijui ni kwanini.Au ndiyo wale ambao hujifurahisha tu na yanapokuja matokeo kama ya mimba huruka kimanga.Yeye ndiye mwenye jibu. Kwa mtindo huu ni wazi kuwa tunatendeana vibaya kumbe ni ndugu,tunabaguana kimakabila na kushadadia sana kuwa huyu ni wa kusini kumbe ndani yake ni wa kaskazini mwenzako.Mbaya zaidi tunaoana wenyewe kwa wenyewe tukidhani kuwa huyu ni kabila lingine unataka kufanya featuring ,kumbe ni ndugu kabisa ndo utakuta yale magonjwa ambayo hurithi kutoka kwa wazazi wetu tunayo wote,msala huo.
Natoa samahani sana kwa wale wote ambao nimewakwanza kwa namna moja ama nyingine.Ama kama kwa namna moja story hii itakuwa ni kama yak wake,ni kweli kuwa matatizo huwa yanafanana na ni sisi (thithi) ndo binadanamu wenyewe ambao yanatutokea haya. Nilifikiria sana kuwasilisha hili swala hapa jukwaani nikasita sana lakini siku moja nilikaa na ofisa mmoja wa kitengo maalumu cha gment anasikitika ni vipi atampata binti yakehuyo binti mwenyewe anaamini kuwa yeye ni mchaga wakati original yake ni mgogo kwa kuwa baba aliye na mama yake ni mchaga,pazito hapo.Na mbaya zaidi watu ambao tuna kumbwa na mikasa hii hufanana sana na hao baba zetu kiasi kwamba tukikaa pamoja hufanana kama korosho(AIBU),kumbe mama yake aliolewa akiwa na ujauzito wa huyo bwana mkubwa.Huyo binti sasa ni mkubwa ameolewa na ana watoto watatu.Sijui atamwingiaje na amwambie kuwa yeye ndiye baba yake mzazi.
HATUWEZI KUKWEPA HILI LAKINI NINA IMANI KUWA KWA KUFAHAMU HISTORIA YAKO UNAWEZA KUWA KATIKA NAFASI FULANI AMBAYO KWA NAMNA MOJA AMA NYINGINE UNAWEZA KUPUNGUZA MATATIZO KAMA HAYA.WAFIKRIE SANA WATOTO NA WATOTO WA WATOTO WAKO.
UNAKUTANA NA MTU KWENYE DALADALA AU SEHEMU NYINGINE,WEWE UNATANGULIZA KUOMBA PENZI,HUJUI ANAKOTOKA WALA ANAKOKWENDA,AU KAFIKA OFINI ANAOMBA KAZI NA ANA KILA SIFA LAKINI HUMPATII NAFASI MPAKA ULALE NAE.MWISHO WA SIKU NI AIBU PALE UKWELI UNAPOKUJA KUFAHAMIKA.
KWA HIYO HATA MIMI NI MMAKONDE LAKINI NDANI YANGU NI MPARE.KUMBE KWELI MTU ANAWEZA KUHAMA KABILA.INAWEZEKANA.