je, Watanzania hawa wanayo haki ya kulia?

je, Watanzania hawa wanayo haki ya kulia?

Hapana, hawa hawana haki ya kulia kwani hapa ni Jangwani (Dar Es Salaam), na hawa watu walishalipwa pesa zao za kuhama hii sehemu siku nyingi sana. Wengi wao walikula tu pesa kufkiri ni za msaada wa kuishi pale Jangwani na wengine wenye akili na kutihi amri walihama. Hawa kimekula kwao.
Baada ya serikali kuwalipa kwanini haikuzibomoa hizo nyumba. Kwani hao viongozi wa serikali huwa hawawaoni hao watu wakiwa bado wanaishi hapo bondeni. Kwanini haikuwashitaki kwa kosa la kula hela ya serikali na kuendelea kuishi hapo?
 
Ni kugumu ndio lakini wapo walioanzia hapo na sasa hawapo kwenye moja tena.
Maisha ni kupanga na kuchagua vile unataka yawe, ukiridhika namna unavyoishi basi hakika utaishia hapo hapo.

mh!ndio hivyo wenzio wanaangalia hapa
badala ya kule!wangehama yasingewafika
lakini ndio hivyo uelewa mdogo!

mi natamani wangesombwa na maji kabisa!!umasikini gani hapo ni kibri ndo kinawasumbua!!serikali imewapa viwanja mabwepande tena vilivyo pimwa!!na juzi mheshimiwa rais alionyesha dhamila yake ya kuwapatia mifuko 100 ya cement ili kuwasaidia kujenga,wao wameviacha viwanja hivyo wanajirudisha town!!!siwahurumii

kwa kweli nimemhurumia huyo mama. She seems to be helpless!
 
jana mmoja wa waathirika alisema kuna kujuana wengine walikosa! I am not sure to what extent is that statement true anyway!
well,huenda kweli,lakini kwanini asubiri hali hiyo ndo atoe kauli hiyo??angesema kabla ili jamii imsikie mapema na huenda angepata msaada wa kufuatilia ili kuona haki inachukua nafasi yake!!
 
pole yake!!umeona alipokumbuka kushika!!!!

Jamani amekusanya tu nguo zake ili aweze kutembea kwenye maji. Kwa kweli anatia huruma sana. Hapo ndio mama kaja mjini kumtembelea mwanae! Duh, hatokaa asahau!
 
Jamani amekusanya tu nguo zake ili aweze kutembea kwenye maji. Kwa kweli anatia huruma sana. Hapo ndio mama kaja mjini kumtembelea mwanae! Duh, hatokaa asahau!
ha ha ha ha!!umenikumbusha mabomu ya gongolamboto!mother alikuwa na siku mbili!!alikimbiaje na ubonge wake!!!!!hadi leo kwangu amesema hadi nihame gongolamboto!
 
Ha Ha Ha nacheka sana kuona serikali inajitekenya yanyewe alafu inacheka yenyewe. Embu waulizeni hao wa mabondeni, nguzo za umeme zimawafikia, ofisi za serikali za mitaa zipo. Serikali ikitoa huduma muhimu zote, hawa wabishi watahama tu.
 
maisha bora kwa kila mchina aah smahani kwa kila mtanzania.
Wewe kafiri mpenda haramu embu toa avata yako hiyo. Unatutoa kwenye udhu hapa. Umesikia wewe kitimoto
 
Baada ya serikali kuwalipa kwanini haikuzibomoa hizo nyumba. Kwani hao viongozi wa serikali huwa hawawaoni hao watu wakiwa bado wanaishi hapo bondeni. Kwanini haikuwashitaki kwa kosa la kula hela ya serikali na kuendelea kuishi hapo?

Sasa wewe unashangaa mambo ya Bongo? Hii nchi hakuna kitu kinachoitwa utekelezaji, umenipata hapo? Waalimu kibao mikoani wanapewa hela za uhamisho na wanajiandaa kuhama, utashangaa watakaa hata mwaka kuhamishwa hawahamishwi na hela wanazila. Hii ndiyo Bongo yetu. Hawa wa Jangwani walishalipwa, baadhi yao walifikiri ama walidanganyana kuwa serikali haitawafuatilia hivyo tule tu hela zao. Usishangae wakamlalamikia Kikwete awahamishe au kuwatafutia makazi mengine.
 
Baada ya serikali kuwalipa kwanini haikuzibomoa hizo nyumba. Kwani hao viongozi wa serikali huwa hawawaoni hao watu wakiwa bado wanaishi hapo bondeni. Kwanini haikuwashitaki kwa kosa la kula hela ya serikali na kuendelea kuishi hapo?
na ndipo unaweza kuona 'picha kubwa'. Kuwa wananchi wanakosea na serikali inaendeleza makosa hayo hayo. wale wanaosema kizungu wanasemage 'two wrongs don't make it right'.
Matakeo yake tunaitwa a failed nation japo mimi naona sisi ni 'a confused nation'
 
Ha Ha Ha nacheka sana kuona serikali inajitekenya yanyewe alafu inacheka yenyewe. Embu waulizeni hao wa mabondeni, nguzo za umeme zimawafikia, ofisi za serikali za mitaa zipo. Serikali ikitoa huduma muhimu zote, hawa wabishi watahama tu.
kwa suala la serikali nadhani kuna wazo ambalo ni gumu sana lakini ndio njia pekee ya kutokea nayo ni KUANZA NA MOJA!
Hawa watu waliopo ni wazito sana na mfumo huu wameujenga wenyewe kwa malengo la kujifaidisha hivyo wao tena hawawezi kuurekebisha. Angalia miji na hata vijiji vilivyo unplanned alafunalundika wawekezaji wanaolindwa na mikataba mibovu ukitegemea nini!?

Habari wanajf,

Nilifuatilia mlolongo wa matukio ya mji wa Dar es Salaam kupitia mvua kubwa zilizonyesha tarehe 21 December 2011 ambapo kiukweli maafa makubwa ya watu wengi kupoteza maisha yalitokea.
Serikali ilichukua hatua na kuwapimia viwanja wenye nyumba na wapangaji vya bure kule Mabwepande na kuweka huduma za msingi japo hazikuwa nzuri kihivyo.

Kilichotokea baada ya hapo ni baadhi yao kuvikataa ili waendelee kuishi 'karibu na mjini'.

Sasa hiki kilio wanamlilia Mungu, Serikali, ccm, cdm ....

View attachment 88114View attachment 88115nawasilisha.

Haki ya kulia wanayo, kwanza kutokana na hayo yaliyowakumba, mbili kutokana na uwezo wao kuwa mdogo kiasi cha kuendelea kukaa katika eneo hatarishi, tatu kutokana na wahusika kuwaacha bila kuwakataza pindi walipoanza kujenga maeneo hatarishi, nne kutokana na jamii kuwaona kama wamejitakia bila kuangalia upande wa pili kwamba hata huko walikoambiwa waende hakuna utaratibu maalumu , nne kutokana na jamii kutoshiriki katika mateso yao. Ni mtazamo
 
watanzania hata elimu ya mtaani hakuna kichwani loo!! Unakubari kufa coz eti serikali mpaka ikulpe ndio uhame mabondeni ulivyokwenda kununua kiwanja ilikuchagulia kiwanja lilia elimu na c ujinga huo na mwaka huu mtakiona sir god leta mvua.
 
na ndipo unaweza kuona 'picha kubwa'. Kuwa wananchi wanakosea na serikali inaendeleza makosa hayo hayo. wale wanaosema kizungu wanasemage 'two wrongs don't make it right'.
Matakeo yake tunaitwa a failed nation japo mimi naona sisi ni 'a confused nation'
That is CCM, si ajabu wanawaacha pale kwa kuhofia kukosa kura zao. Ukishakuwa na kiongozi anayejali kuendelea kutawala tu despite what goes along with the people, ujue unaongozwa na maiti. Na huko ndiko tuliko watanzania.
 
Baada ya serikali kuwalipa kwanini haikuzibomoa hizo nyumba. Kwani hao viongozi wa serikali huwa hawawaoni hao watu wakiwa bado wanaishi hapo bondeni. Kwanini haikuwashitaki kwa kosa la kula hela ya serikali na kuendelea kuishi hapo?

umeongea cha maana sana
 
Back
Top Bottom