Je watanzani tutasubutu?

leonaldo

JF-Expert Member
Oct 26, 2014
2,585
3,179

Wenzetu wakenya wako mbioni kukamilisha Reli yao hivi karibuni, nawapongeza sana kwa mambo mawili makubwa.
1. wameshirikiana na vijana wengi sana wa kitanzania kufanya kazi hii kama maopareta wa mitambo mbalimbali, madreva na kazi nyingine nyingi zilizohitaji ujuzi maalumu
2. katika hili hawakutubagua majirani zao, tofauti na nilivyokuwa naamini.
SABABU
Watanzania kwa miaka mingi sasa tulikuwa tukishiriki kujenga miundombinu hivyo kuzalisha watu wenye ujuzi mbalimbali katika shughuri za ujenzi wa miundo mbinu kuliko majirani zetu wote, na kampuni ya CRBC, CCCC Zimefanya kazi hapa nchini hivyo walichukua wafanyakazi wengi toka katika miradi waliyofanya hapa nchini
SWALI
Je mtawavumilia wakenya pia watakapokuja kutusaidia kujenga ya kwetu hivi karibuni kwani tayari wana ujuzi katika ujenzi wa reli?.
 
Ushahidi uko wapi kua watanzania wamehusika kwa fani rahisi hivo???
Huwajui wakenya wewe
 
Tutasubutu= Tutathubutu au?
 
Ushahidi uko wapi kua watanzania wamehusika kwa fani rahisi hivo???
Huwajui wakenya wewe
Natoka kanda ya ziwa nawafahamu vizuri sana, hata mimi nashangaa kama wewe na pia nilikuwa na imani kama yako, maopareta wa mitambo ni viungo muhimu sana kwenye ujenzi wowote ule usidharau na ndio wajenzi wenyewe waliobaki ni wataalamu kwa maana ya kusimamia nawafahamu wengi binafsi kwa kuwa nimefanya kazi na makampuni haya.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…