Je, Wasandawe asili yao ni Afrika Kusini?

Jacobus

JF-Expert Member
Mar 29, 2011
4,700
1,721
Ukimsikiliza Msandawe, mkoa wa Dodoma, anavoongea hatofautiani sana na Mxhosa wa Afrika Kusini.

Kwa kuwa Wasandawe hapa kwetu ni wachache kulinganisha na Waxhosa wa Afrika Kusini, inawezekana basi Wasandawe walitokea huko? Wajuzi wa historia watujuze tafadhari.

"Xhosa. The Xhosa is the second most popular language after the Zulu out of all the South African tribes, the name means fierce or angry. .."
 
Wanafanana sana sio lugha pekee hata ukiangalia mavazi, chakula na sehemu wanazoishi. Ipo haja ya kutizama iwapo hizo lugha zao zinaingiliana.
 
Wanafanana sana sio lugha pekee hata ukiangalia mavazi, chakula na sehemu wanazoishi. Ipo haja ya kutizama iwapo hizo lugha zao zinaingiliana.
Ndipo hapo mkuu, ninachosangaa ni ki vipi watoke huko na kuja jikita ndani ya Kondoa? Hebu soma hapa 'Tanzania is home to more than 120 different tribes, most of them belonging to the big Bantu family. The fierce Masai are Nilotic people. The Hadzabe tribe, living along the remote shores of Lake Eyasi, is related to the South African bushmen.'
 
Je humu JF hakuna Wahadzabe wakatujuza?
 
Je humu JF hakuna Wahadzabe wakatujuza?
Mkuu, lakini huu uhusiano wa haya makabila inakuwaje? Maana toka Afrika Kusini mpaka Tanganyika tena katikati! Au asili ya Bushmen na Xhosa ni Tanganyika?
 
Mkuu, lakini huu uhusiano wa haya makabila inakuwaje? Maana toka Afrika Kusini mpaka Tanganyika tena katikati! Au asili ya Bushmen na Xhosa ni Tanganyika?
Bado sisi tunaulizana kulikoni hawa watu wakafanana lafudhi na matamshi, mavazi, chakula, mazingira wanayoishi, nk. Je asili yao ni wapi?
 
Wataalam wa lugha wanazigawa lugha zinazozungumzwa Afrika, hasa kusini mwa jangwa la Sahara, katika makundi manne.

Kuna lugha za Kibantu kama vile Kingoni, Kisukuma, Kinyakyusa, Kihaya, n. k. Halafu kuna lugha za Kikushi (Cushitic languages) kama Kiiraqw n.k. Zipo pia lugha za Kiniloti (Nilotic languages) kama Kimasai, na Kimang'ati. Mwisho kuna lugha za Khoisan, mfano mzuri ndio hao Wasandawe na pia Wahadzabe.

Hapa Tanzania lugha zote hizo zinazungumzwa. Hata hivyo Kibantu kinazungumzwa na wengi zaidi, na Khoisan zinazungumzwa na wachache sana. Kwa Afrika ya Kusini, Xhosa ni mfano mzuri wa Wabantu na mfano wa Khoisan ni Khoikhoi na San (Wazungu waliwaita Hotentots na Bushmen).

Kwa hiyo hakuna uhusiano wa moja kwa moja kati ya Wasandawe (ambao kimsingi ni Khoisan) na Xhosa (ambao kimsingi ni Wabantu). Kufanana kwa lugha zao (zote zinatabia inayoitwa "click") ni kutokana na mwingiliano wa kijamii na kiutamaduni. Yaani Xhosa waliathiriwa na lugha ya majirani zao Khoikhoi.

Inaaminika kuwa Wabantu wa Afrika ya Kusini wanaasili ya eneo la maziwa makuu ya Afrika ya Mashariki. Kuhusu Wasandawe, michoro ya mapangoni inaonyesha kuwa walikuwepo eneo hili miaka mingi sana iliyopita.
 
50701356c5987e586b5bacd115ea2f30.gif
[/IMG]
 
Back
Top Bottom