Je, Wananchi wamezoea bure kila kitu?

Je, Wananchi wamezoea bure kila kitu?

Kamundu

Platinum Member
Joined
Nov 22, 2006
Posts
9,268
Reaction score
13,895
Inaelekea Tanzania tuna tatizo la wananchi kuzoea bure na misaada. Ukiangalia hata mijadala mingi watu wanaongea na kuandika kama vile kila kitu inatakiwa serikali kutoa.

Hatuwezi kuwa na machinga kila mahali hawalipi kodi halafu tushangae kodi kuongezeka kwenye simu. Ni lazima tujue bila makusanyo tutarudi kuwa watu wa kulalamika tu. Serikali isifanye kodi kisiasa
 
Nchi inayoongoza kwa kodi duniani ni Tanzania, lakini ni miongoni mwa nchi masikini kabisa duniani.
 
Na huko juu waache ubadhirifu maana kila ripoti ya CAG ikitoka yamepigwa mabilioni kadhaa....mkitoka hapo chimbo lenu ni Wanainchi kwa kuwashindilia matozo na makodi.
 
Mkuu nini ni Bure Tanzania ?

Hivi unajua kila unachonunua kina kodi ndani yake ? Wala yote yanafanyika sio hisani bali juhudi zako katika kuchangia hicho kidogo unachochangia ?, Kanunue Luku au angalia Risiti yoyote uliyonayo ndio utagundua kwamba kila unachonunua kuna mkono wa serikali...
 
Sio kwamba Wananchi wamezoea vya bule tatizo nchi Ina masikini wengi .yani watu zaidi ya million 20 n mafukara Sasa watalipaje Kodi .Siku nyingine ficha ujinga wako.Ccm ndo kiwanda kilichozalisha Hawa masikini
 
Kwanza Wachumi waliomshauri Mwiguli ni fake labda watuambie walilazimishwa.Yani kiuchumi huwezi ukaweka ongezeko la tozo kutoka shs 8,000-35,000 huku purchasing power ya watu wako ni ile ile mwendawazimu pekee ndio anaweza Fanya kitu kama hicho.

Na tatizo kubwa zaidi hata hizo hela zikipatikana matumizi yake ndio hayo kununua wabunge wa upinzani na kwenda kujenga nyumba za Marais wastafu.
 
Ni lazima tujue bila makusanyo tutarudi kuwa watu wa kulalamika tu. Serikali isifanye kodi kisiasa
Hakuna anayekataa kutoa Kodi. Tatizo ni ukubwa wa tozo. Halafu kwann tulipe TOZO wakati KODI tunalipa???
 
Kwaiyo tulikua hatukatwi kbsa kwnye miamala,tulivoanza kukatwa ndo watu wakaachukia?🤔
 
Acha ujinga Dogo, waliozoea vya bure ni viongozi maana kila kitu kwao ni bure, huku wakiwa na mishahara minono. Sasa kama marais, mawaziri wakuu, majaji, viongozi wa vyombo vya dola wastaafu, wanalipwa mpaka wafe huku hawafanyi lolote, nani anapenda bure hapo? Acha kupandisha hasira za watu tusije tukaingia mtaani hata kesho, mpuuzi mkubwa ww.
 
Na huko juu waache ubadhirifu maana kila ripoti ya CAG ikitoka yamepigwa mabilioni kadhaa....mkitoka hapo chimbo lenu ni Wanainchi kwa kuwashindilia matozo na makodi.
Tatizo siyo kodi tatizo kubwa matumizi. Kwa ujumla ubadhirifu
 
Acha ujinga Dogo, waliozoea vya bure ni viongozi maana kila kitu kwao ni bure, huku wakiwa na mishahara minono. Sasa kama marais, mawaziri wakuu, majaji, viongozi wa vyombo vya dola wastaafu, wanalipwa mpaka wafe huku hawafanyi lolote, nani anapenda bure hapo? Acha kupandisha hasira za watu tusije tukaingia mtaani hata kesho, mpuuzi mkubwa ww.
Halafu hao wanaopata vya bure kwa asilimia kubwa ndiyo ambao hawalipi kodi
 
Kati ya wananchi na serikali nani tegemezi kwa mwenzie kwa sasa.....punguza masifa bladifakeni!!!!!
 
Inaelekea Tanzania tuna tatizo la wananchi kuzoea bure na misaada. Ukiangalia hata mijadala mingi watu wanaongea na kuandika kama vile kila kitu inatakiwa serikali kutoa.

Hatuwezi kuwa na machinga kila mahali hawalipi kodi halafu tushangae kodi kuongezeka kwenye simu. Ni lazima tujue bila makusanyo tutarudi kuwa watu wa kulalamika tu. Serikali isifanye kodi kisiasa

Lakini si kwa Double Taxation. Au kurundika makodi kwenye bidhaa moja
 
Back
Top Bottom