Je, wanachoniambia UPS ni sahihi?

Fuga Kisasa

Senior Member
Jan 16, 2016
165
91
UPS ni kampuni inayofanya shughuli za kusafirisha mizigo kutoka nje ya nchi kuja au kupeleka nje ya nchi.

Niliagiza mzigo wangu kutoka nje ya nchi, umefika tayari umefika na nimeambiwa natakiwa kuulipia.

SIFA ZA MZIGO WANGU:
1. Una KG 10
2. Una thamani ya USD 95 (Ambayo ni sawa na TZS 209,000)
3. Mzigo huo ni sample (hata nje ya mzigo umeandikwa hivyo)

MAMBO WALIYONIAMBIA UPS:

1. Natakiwa kulipia gharama zisizopungua laki moja na kumi na nne ambayo ni nusu ya bei ya kununulia mzigo.
2. Hiyo laki moja na kumi na nne= 80,000 ya clearing fee: 20,000= airport handling fee na 14,000 ni ushuru
2. Nimeambiwa naweza kuwatumia wao wafanye clearence ya huo mzigo au nitumie agent mwingine LAKINI nikitumia agent mwingine nitatakiwa kulipia 57,000 kwao ili wanipatie hiyo document kutoka customs ambayo ndio nitaiepeleka kwa agent mwingine ili anitolee mzigo wangu.
3. Nimewauliza hiyo doc kama wao wanapewa bure kwanini mimi nilipie 57,000? wakasema hata wao wanalipia hiyo gharama ya doc kwa Swissport.

NAOMBA KUFAHAMU YAFUATAYO:
1. Sample huwa inatakiwa kulipia ushuru?
2. Maelezo yote niliyoyapewa na UPS hapo juu ni sahihi?

Natanguliza shukrani wakuu

cc: Ndg.MWASALEMBA. JZHOELO Mwl.RCT Njunwa Wamavoko
 
Ndugu Fuga Kisasa

- Iwapo mzigo wako ungekuja kwa posta - usingelipia chochote, Kwa mizigo ipitiayo na kukaguliwa TRA (airtport) hata isiyostahili kulipiwa kodi, hulipiwa kodi, hili ni tatizo.

- Ila kwa kuwa umetumia UPS, walipe fedha inayohitajika na uchukue mzigo wako, Maana kadri utakavyokuwa kutunza ndio ghalama itaongezeka. Hivyo swali lako la Pili: Ni sahihi kwa taratibu zao walizojiwekea.

Angalia hii screenshot
1570179014748.png

- Nilitumia TNT, Na nilijuta kwa nini niliwatumia, nilitakiwa kulipia TSH 555,000, Kwa bidhaa toka USA yenye thamani ya US $162
Umeona hizi ghalama
1. Break-Bulk fee???
2. Agency Fee???

HITIMISHO
- Walipe uchukue mzigo wako
- Baadhi ya kampuni za usafirishaji si zakutumia kabisa

Thread Rejea

- Hili Halijapata Ufumbuzi kuhusu Ununuzi wa Vitu kwa Njia ya Mtandao (Online Purchase)
 
Attachments

  • 2016-09-28_03-50-52.jpg
    2016-09-28_03-50-52.jpg
    19 KB · Views: 74
UPS ni kampuni inayofanya shughuli za kusafirisha mizigo kutoka nje ya nchi kuja au kupeleka nje ya nchi.

Niliagiza mzigo wangu kutoka nje ya nchi, umefika tayari umefika na nimeambiwa natakiwa kuulipia.

SIFA ZA MZIGO WANGU:
1. Una KG 10
2. Una thamani ya USD 95 (Ambayo ni sawa na TZS 209,000)
3. Mzigo huo ni sample (hata nje ya mzigo umeandikwa hivyo)

MAMBO WALIYONIAMBIA UPS:

1. Natakiwa kulipia gharama zisizopungua laki moja na kumi na nne ambayo ni nusu ya bei ya kununulia mzigo.
2. Hiyo laki moja na kumi na nne= 80,000 ya clearing fee: 20,000= airport handling fee na 14,000 ni ushuru
2. Nimeambiwa naweza kuwatumia wao wafanye clearence ya huo mzigo au nitumie agent mwingine LAKINI nikitumia agent mwingine nitatakiwa kulipia 57,000 kwao ili wanipatie hiyo document kutoka customs ambayo ndio nitaiepeleka kwa agent mwingine ili anitolee mzigo wangu.
3. Nimewauliza hiyo doc kama wao wanapewa bure kwanini mimi nilipie 57,000? wakasema hata wao wanalipia hiyo gharama ya doc kwa Swissport.

NAOMBA KUFAHAMU YAFUATAYO:
1. Sample huwa inatakiwa kulipia ushuru?
2. Maelezo yote niliyoyapewa na UPS hapo juu ni sahihi?

Natanguliza shukrani wakuu

cc: Ndg.MWASALEMBA. JZHOELO Mwl.RCT Njunwa Wamavoko
Iwapo angetumia posta yani normal postage? Does it include DHL, EMS au only restricted to Posta?
 
Back
Top Bottom