Je, wanaCCM wenzie wameshaanza kumgeuka?

Je, wanaCCM wenzie wameshaanza kumgeuka?

Mystery

JF-Expert Member
Joined
Mar 8, 2012
Posts
15,842
Reaction score
31,073
Hilo ndilo swali la msingi ambalo sisi watanzania tunapaswa kujiuliza, kwa kuwa kumeanza kujitokeza wanaccm ambao wameanza kuukosoa waziwazi utawala huu wa serikali ya awamu ya 5 ambapo hapo kabla ilikuwa haiwezekani kufanyika kitu kama hicho na badala yake tuliwazoea wapinzani pekee wakipambana na hali hii ya kupigwa risasi mchana kweupe na watu "wasiojulikana" kutekwa kwa raia mbalimbli na baadaye kupatikana, matukio ya kuuawa wananchi wasio na hatia na matukio mengi ya aina hiyo yamekuwa ya kawaida sana kwenye utawala huu wa serikali ya awamu ya 5

Wapinzani wamelalamika wee, wanaharakati wa haki za binadamu wamepigia kelele wee na baadhi ya viongozi wa dini nao wamelalamika weeee........ Lakini hakuna hatua zozote zilizochukuliwa kukomesha hali hiyo.

Tukaamza kuona mabandiko ya wanaccm kwenye mitandao ya kijamii, lakini Mara tu inapobainika na kuwekwa wazi kwenye jamii kuwa waliobandika mabandiko hayo ni wanaccm, watumiaji hao Mara moja wamekuwa wakikanusha kuwa siyo wao waliopost hizo taarifa na badala yake account zao zimekuwa hacked!

Refer taarifa za kukanusha za akina Ole Sendeka, Ridhiwan Kikwete na Shyrose Bhanji

Lakini hivi sasa wamejitokeza wanaccm "majasiri" na kueleza waziwazi msimamo wao kuwa hawakubaliani na mfumo wa kisiasa unaoendeshwa na utawala wa awamu ya 5

Wanaccm ambao wameonyesha kuupinga waziwazi mfumo huu serikali ya awamu ya 5 kwa kuwataja wachache tu ni Hussein Bashe na Nape Nnauye

Nimeanza kuyakumbuka maneno ya Mheshimiwa Tundu Lissu kuwa mtu huyu akishaumaliza upinzani atakuja kwenu CCM, kwa kuwa historia duniani kote ya "madikteta" ndiyo "formula" yao ya kuanza na upinzani na hatimaye kumalizana na wale "wanaowashwawashwa" ndani ya chama chake!

Hatimaye watanzania wote bila kujali itikadi zetu za kisiasa tumeamua kuupinga utawala huu kwa nguvu zote.

Kwa kuwa tumeona ndiyo njia pekee iliyobaki kabla Taifa letu halijasambaratika na kuelekea shimoni.

Mungu ibariki Tanzania
 
Mshahara wa dhambi ni mauti Bali karama ya Mungu ni uzima wa milelele, wameanza kuyajutia makosa yao
It's very true

Kwa kuwa weshaona "hatari" inayowanyemelea

Maana kwa sasa hakuna tena mfumo wa kupata mgombea ubunge kwa kura za maoni

Kwa mfumo huu "alioubuni" Bwana Mkubwa, 2020 tutarajie wabunge wengi "wakorofi" kupigwa chini na nafasi zao kuchukuliwa na wanakolomije!
 
Nyie maf.ala mnaangaika Sana mitandaoni.Naanza kuamini hamna kazi nyingine za kufanya, ila mkija kushtuka umri umewatupa mkono,serikali ni hii hii,CCM ni hii hii,katiba ni hii hiihii, tume ni hii hii na Raisi wa Jamhuri ni John Pombe Joseph Magufuli mpaka 2025.Haya mengine mnapoteza time tu.
 
Kwani kuna mtu kabisha?
 
Mimi sio mnafiki amenikera sana.
1.Rais ni mwongo maana aliongea tarehe 14/10/2017 kuwa kuna Watumishi wa Umma 59,000+ watapandishwa madaraja mwezi Novemba lakini hadi sasa hajapanda hata mmoja.

2.Rais alisema baada ya uhakiki kumalizika kutakuwa na maslahi bora kwa Watumishi wa Umma lakini hadi sasa wamepewa za uso.

Waandishi wa habari hizi hazifai kupamba kwenye front page maana sijawahi kuziona.

Kutoka hifadhi ya misitu ya Madihani
Mwanachama wa CCM.
 
Hakika inajiimarisha.

BAVICHA kwa kujipa moyo hakuna anayewazidi!

Endeleeni kulishana upepo wa kisiasa wakati CCM inazidi kujiimarisha kisiasa.
 
MFA maji hakosi kutapatapa, mmoja alisema watashinda kwa goli la mkono, sasa goli hilo limemtokea puani.
Hahaaaa......😀😀

Mkuu Ss Jr umenikumbusha mbali.....

Alijitokeza jamaa hapa akatuambia kuwa CCM imeshinda kwa gili la mkono!

Hivi sasa ni kweli goli hilo la mkono lishaanza kumtokea puani!
 
Namchukia sana huyu Mkara
1.Rais ni mwongo maana aliongea tarehe 14/10/2017 kuwa kuna Watumishi wa Umma 59,000+ watapandishwa madaraja mwezi Novemba lakini hadi sasa hajapanda hata mmoja.

2.Rais alisema baada ya uhakiki kumalizika kutakuwa na maslahi bora kwa Watumishi wa Umma lakini hadi sasa wamepewa za uso.

Waandishi wa habari hizi hazifai kupamba kwenye front page maana sijawahi kuziona.

Kutoka hifadhi ya misitu ya Madihani
Mwanachama wa CCM.
Nyie maf.ala mnaangaika Sana mitandaoni.Naanza kuamini hamna kazi nyingine za kufanya, ila mkija kushtuka umri umewatupa mkono,serikali ni hii hii,CCM ni hii hii,katiba ni hii hiihii, tume ni hii hii na Raisi wa Jamhuri ni John Pombe Joseph Magufuli mpaka 2025.Haya mengine mnapoteza time tu.
 
Vya dezo dezo ambavyo hakuna tena ndio mnyoosho wanaopata awamu hii.. watazoea tu
 
Back
Top Bottom