Kipenzi Chao
Member
- Oct 12, 2010
- 99
- 4
- Je, wanaume mwajua kuwa waweza kumtunza mkeo kwa kumpatia vitu kama gari zuri, nyumba nzuri, bank account iliyonona, uhuru wa kutosha, nafasi ya kushiriki kwenye maamuzi, mapenzi yote atakayo na kwa kiwango anachotaka, saloon, mavazi apendayo, simu nzuri, computers, kumsomesha, kumtafutia kazi nzuri, n.k, lakini huenda akadanganyika kwa vocha ya Tshs. 1,000 au lift?
- Je, wanawake mwajua kuwa mmeo anaweza kuwa na Tshs. 200,000 mfukoni, na akabania Tshs. 20,000 za kukupeleka wewe/mama yake mzazi hospitali, lakini akajikuta ametumia Tshs.100,000 kati ya hizo kumbembeleza kimada na bado akaambulia patupu?