Je wajua?

Je wajua?

Ray M

Senior Member
Joined
Sep 23, 2012
Posts
182
Reaction score
61
Jana niliandika juu ya kutafuta mdada/mwanamke wa kuzaa naye mtoto kwa makubaliano. Nilipata kujifunza baadhi ya vitu kuhusu ndugu waliochangia ile mada. Baadhi walitumia busara kunishauri, na wengine bila kujali ama kunielewa wakawa wananitolea lugha za kejeli na wengine kudiriki kunitukana. Yote kwangu heri, lakini pamoja na hayo naomba niwashauri ndugu zangu badala ya kutumia kauli za Jazba ama dharau dhidi ya mtu usiyemfahamu basi ni bora ujikalie kimya. Kwanza itakuokolea muda wako na pia itasaidia usionekane “mtu wa ajabu”.

Baadhi ya akina dada walionekana kuchukia sana nilipoandika vile, hii ilinipa Impression kuwa huenda hawa wadada ndiyo wale waliohangaika kutwa kucha wakitafuta Bwana wa kuwaoa na imeshindikana, hivyo kila kitu anachokiongea mwanaume kikiwa ni kinyume na ndoto zao basi wanaamua kumsakama kwa jazba. Msiwe hivyo dada zangu. Fuateni ushauri huu hapa:

KWA WALE AMBAO HAWANA WENZA TUSUBIRI WENZA WETU KUTOKA KWA BWANA NDEGE WANAOFANANA HURUKA PAMOJA!

Naamini kuwa JamiiForums ni Jukwaa kwa ajili ya watu wote hence JamiiForums. Humu wapo watu wazima, Vijana na huenda pia kuna watoto wadogo (who knows?). Tujitahidi kwa nafasi tulizo nazo tuwe constructive kwenye kila mada tunayochangia. Bila kujali kama inatupendeza ama inatukwaza.

Hizi ni badhi tu ya Comments za Memba dhidi ya kile nilichokiandika jana.

Huyu alijaribu kunipa changamoto: Thanks
Wale wanaopataga watoto mapema zile ni bahati mbaya bro hawapangagi ivyoo...

Huyu akarukia:
Yaani huyu hata hajui maisha ninini Mungu wangu. embu msaidieni, anyway kama shida ni mtoto anaweza akaenda kuadopt kwenye vituo wako wachanga kibao aache ununda hapa

Huyu kwa hekima na Busara akanipa ushauri huu: Thanks
Miaka 26 ni umri unakuruhusu kuoa kabisa ikizingatia unasema una kazi na biashara zako. Nakushauri uoe ili mtoto atakaye zaliwa apate malezi mazuri ya wazazi wote.

Mwingine bila kujua tunajadili nini akaja na hii:
Aliyekwambia wewe ni damu ya babako ni nani? na Unamwamini?

Huyu akahoji, kisha akashauri: Thanks
Naona hujasoma maelezo yake vizuri, lakini swala la baba yake limeingiaje hapa? kama unakuwa unaona post haikuhusu chapa mwendo.

Huyu ndugu yeye akanipa moyo: Thanks
Mkuu RAY M natumai umeeleweka na atakayekuwa tayari kuambatana nawe basi atawasiliana nawe,nakutakia kila lenye heri katika kufanikisha mpango wako huo ila mwombe Mungu akupe afya njema ya kuweza kumjaza huyo mwanamke mimba maana wengine huishia kuweka mbegu shambani lakini mazao wasiyapate.

Wengine hawa:
Wewe huna hata kigezo kimoja cha kuwa Mume, sasa utapata vipi Mwanamke mwenye vigezo hivyo?

Unasumbuliwa na stress nenda kwa wataalam wa saikolojia watakusaidia.

Huyu inaelekea hajapata malezi ya baba na mama ndo mana anatafta mtu wa kuzaa nae tu ili aitwe baba, sio kosa lake kwani hajui utamu wa kuishi na wazazi wote wawili. Mi namtakiaa mafanikio katika hitaji lake

Kongosho hawa vijana wa KAWAMBWA watakuchemsha kichwa...yaani kamtukana hadi mama yake kuona wanawake ni kama ng'ombe au mbuzi...Nasema hivi kwani kijijini kwetu wanaazimishana ili amzalie mwazimaji ndama then akizaa tena anapewa mwenye Ng'ombe au mbuzi...shiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiit kameniuzi kweli haka kadogo.

Huyu naye sikuelewa dhima ya hii kauli yake hii:
upuuzi mtupu
Relax!!!

Kwa kumalizia ningependa kuchukua fursa hii kuwakaribisha kwenye huduma za Massage kutoka Wapendwa Massage Centre. Hii huduma itawasaidia kupunguza uchovu na hata hasira ambazo wakati mwingine zinapelekea kuchangia mada kwa jazba.

Asanteni na Karibuni.
Ray
 
Ingekuwa kila mtu baada ya kuanzisha thread anaandika mambo yaliyotokea nadhani kungekua na umbea mwingi.
 
Dada/kaka: lengo langu hapa siyo umbea bali ni kuwataka wahusika wawe positive. hii ni kwa manufaa yetu sote
 
Kwahiyo unataka ukiandika kitu kila mtu awe na mawazo sawa na yako?

Miafrika ndivyo tulivyo by Nyani Ngabu.
 
Unapotolewa ushauri hapa, inatakiwa utumie busara sana kupembua upi huufwate au ni upi huuwache coz ushauri unaotolewa hapa haulingani, kila mmoja ana mawazo na fikra zake binafsi, hata watu wakikuponda haina haja ya wewe kuwa na jazba na kuanza kuwa quot humu, ulitakiwa upuuzie tu na kufuata ule ushauri ulio kuridhisha.
 
Una hoja ndugu yangu sema sasa kila mtu na akili yake usishangae raia wanavyokuja juu
 
Kwahiyo unataka ukiandika kitu kila mtu awe na mawazo sawa na yako?

Miafrika ndivyo tulivyo by Nyani Ngabu.

sijasema watu wawe na mawazo sawa na yangu. hoja hapa ni watu wajifunze kutofautiana kimtazamo bila kutumia jazba,
 
Unapotolewa ushauri hapa, inatakiwa utumie busara sana kupembua upi huufwate au ni upi huuwache coz ushauri unaotolewa hapa haulingani, kila mmoja ana mawazo na fikra zake binafsi, hata watu wakikuponda haina haja ya wewe kuwa na jazba na kuanza kuwa quot humu, ulitakiwa upuuzie tu na kufuata ule ushauri ulio kuridhisha.

ni kweli uyasemayo dadaangu. lakini kupuuzia matatizo siyo suluhisho la matatizo. ni bora tuambiane ukweli ili tupate kujirekebisha.
 
Jana niliandika juu ya kutafuta mdada/mwanamke wa kuzaa naye mtoto kwa makubaliano. Nilipata kujifunza baadhi ya vitu kuhusu ndugu waliochangia ile mada. Baadhi walitumia busara kunishauri, na wengine bila kujali ama kunielewa wakawa wananitolea lugha za kejeli na wengine kudiriki kunitukana. Yote kwangu heri, lakini pamoja na hayo naomba niwashauri ndugu zangu badala ya kutumia kauli za Jazba ama dharau dhidi ya mtu usiyemfahamu basi ni bora ujikalie kimya. Kwanza itakuokolea muda wako na pia itasaidia usionekane “mtu wa ajabu”.

Baadhi ya akina dada walionekana kuchukia sana nilipoandika vile, hii ilinipa Impression kuwa huenda hawa wadada ndiyo wale waliohangaika kutwa kucha wakitafuta Bwana wa kuwaoa na imeshindikana, hivyo kila kitu anachokiongea mwanaume kikiwa ni kinyume na ndoto zao basi wanaamua kumsakama kwa jazba. Msiwe hivyo dada zangu. Fuateni ushauri huu hapa:

Naamini kuwa JamiiForums ni Jukwaa kwa ajili ya watu wote hence JamiiForums. Humu wapo watu wazima, Vijana na huenda pia kuna watoto wadogo (who knows?). Tujitahidi kwa nafasi tulizo nazo tuwe constructive kwenye kila mada tunayochangia. Bila kujali kama inatupendeza ama inatukwaza.

Hizi ni badhi tu ya Comments za Memba dhidi ya kile nilichokiandika jana.

Huyu alijaribu kunipa changamoto: Thanks

Huyu akarukia:

Huyu kwa hekima na Busara akanipa ushauri huu: Thanks

Mwingine bila kujua tunajadili nini akaja na hii:

Huyu akahoji, kisha akashauri: Thanks

Huyu ndugu yeye akanipa moyo: Thanks

Wengine hawa:

Huyu naye sikuelewa dhima ya hii kauli yake hii:
Relax!!!

Kwa kumalizia ningependa kuchukua fursa hii kuwakaribisha kwenye huduma za Massage kutoka Wapendwa Massage Centre. Hii huduma itawasaidia kupunguza uchovu na hata hasira ambazo wakati mwingine zinapelekea kuchangia mada kwa jazba.

Asanteni na Karibuni.
Ray
Ndugu wewe unahangaika na watu wa humu mbona utajichosha yani simple observation ni hii watu humu wengi wao wanastress za maisha, pili wanacomment kitu kutokana na hisia na mihemko wala sio logic..na wengi wao wamejikita katika either kumdiscuss mtu aliyeleta au kutoa mada badala ya kutoa ushauri halafu kuna tabia ambayo mtu akiona post lazima acomment hata kama hana cha kucomment..mfano..mara utasikia oooh ngoja wana kuja, ooh sijui na pita niggaahh u aint got nothing to say just chillax haupungukiwi chochote kile kwa kutoa comments za kilooser..lakini kama ulivyosema wengi wamekata tamaa kutokana na ndoto zao hazijatimia au kile wanachokiamini au kukitegemea kua hakijawa..so usiwaze brother...ndo utanzania huo tuvumiliane tuu..Over..!!!
 
ni kweli uyasemayo dadaangu. lakini kupuuzia matatizo siyo suluhisho la matatizo. ni bora tuambiane ukweli ili tupate kujirekebisha.

sijasema upuuzie matatizo, nilichosema ni upuuzie ule ushauri ambao wewe unaona haukufai, fuata ule ambao unakuridhisha.
 
Wewe mwenyewe ndio mwenye tatizo la kuangaika kutafuta bibi na hamna anae kutaka.
Wanaume wanaopendwa kikweli wanategeshewa mimba,
ila wale wasio pendwa kama wewe ndio wanaangaika kutafuta bibi
wa kuzaa nae.

Shukuru umeambiwa ukweli, na ukweli unauma, utaambulia patupu, ama kutapeliwa.
 
Ndugu wewe unahangaika na watu wa humu mbona utajichosha yani simple observation ni hii watu humu wengi wao wanastress za maisha, pili wanacomment kitu kutokana na hisia na mihemko wala sio logic..na wengi wao wamejikita katika either kumdiscuss mtu aliyeleta au kutoa mada badala ya kutoa ushauri halafu kuna tabia ambayo mtu akiona post lazima acomment hata kama hana cha kucomment..mfano..mara utasikia oooh ngoja wana kuja, ooh sijui na pita niggaahh u aint got nothing to say just chillax haupungukiwi chochote kile kwa kutoa comments za kilooser..lakini kama ulivyosema wengi wamekata tamaa kutokana na ndoto zao hazijatimia au kile wanachokiamini au kukitegemea kua hakijawa..so usiwaze brother...ndo utanzania huo tuvumiliane tuu..Over..!!!

Poa Braza nimekusoma. Sema wakati mwengine tuwe tunawapa watu ukweli ili wajirekebishe
 
Wewe mwenyewe ndio mwenye tatizo la kuangaika kutafuta bibi na hamna anae kutaka.
Wanaume wanaopendwa kikweli wanategeshewa mimba,
ila wale wasio pendwa kama wewe ndio wanaangaika kutafuta bibi
wa kuzaa nae.

Shukuru umeambiwa ukweli, na ukweli unauma, utaambulia patupu, ama kutapeliwa.

Asante
 
Kuna nati imelegea mahali, chunguza kwa umakini zaidi isije kupotea wakati safari inaendelea.
 
yani wewe ndo umeongea kabisa maana wengine wanafikiri wakiweka thread yao itachangiwa kwa positive na sio negative

Back
Top Bottom