Je wajua kipindi cha Apartheid South Africa; wachina walikuwa classified Km blacks na wajapani wazungu au honorary whites??๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚ imagine we ndo polisi unaanza kuamua nani mjapani na nani mchina na nani apendelewe kwa uzungu na nan aonewe au atengwe kuwa mweusi.๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚
IMG_6495.jpeg
 
Wachina, wajapan na wakorea wana chimbuko moja ndio maana wana fanana sana licha ya kuwa utofauti mdogo upo
 
Sidney Etemesi ni Mkenya aliyezaliwa akiwa na viungo vya uzazi aina mbili, uume na uke.

Maumbile yake yamekuwa changamoto kubwa katika uhusiano wake na watu wengine katika jamii. Kila siku, ameishi kukejeliwa kushoto kulia na wanaofahamu hali yake, japo si ya kujitakia.

Mwili wake Sidney umebeba viungo vya uzazi aina mbili, vya kike na vya kiume.

Lakini kwa kumwangalia tu, bila kujua hali yake ya kuzaliwa nayo, basi utamfananaisha na mtu wa kawaida tu.

Yeye huishi kama mwanamume ingawa kwa kiasi muonekano wake wa sura unaegemea upande wa wanawake.

Ni hali ambayo humchanganya Sidney kila kuchao, anapopambana na nafsi yake na kujaribu kujitambulisha kwa wengine.

"Kila siku ya maisha yangu, ninapoingia kwenye bafu nikijitazama maumbile yangu ya kuwa na uke na uume katika mwili mmoja huwa najihisi mnyonge na mwenye hofu kuu. Ila sina lakufanya," anasema Sydney.

Kuvunja ungo

Matatizo zaidi yalianza pale alipoanza kubalehe akiwa na umri wa miaka 13. Mwili wake ulianza kubadilika kama wanarika wengine, japo mabadiliko yake yalianza kufanana na yale ya kiume.

Alibaguliwa na kuchekwa kwa kujitambulisha kama mwanamume ilhali muonekano wake wa sura ulikuwa wa kike .

"Muonekano wangu bila shaka umekuwa ukiwakanganya watu sana. Sura yangu na maumbile yangu ya nje ya mwili yana muonekano wa kike zaidi. Lakini undani wangu hisia zangu na nguvu zangu nazihisi kama za kiume tangu zamani," anasema Sydney

Kipindi cha Sydney kuishi mitaani hakikuwa kirefu kwani kwa bahati alikutana na msamaria mwema aliyemuelekeza kwa muungano wa huntha nchini Kenya.

Hapo ndipo Sidney alipopata nafasi ya kujielewa. Aidha, alikutana na watu ambao wametekwa na maumbile ambayo ni tofauti na jinsi wanavyojitambulisha.

Changamoto za kuwa huntha

Sidney amekumbana na changamoto nyingi kila siku. Kwanza kabisa ni kuwa alichukua ujasiri wa kuoa kwani anasema kuwa yeye amekuwa na hisia za kupenda jinsia ya kike.


Anasema jinsia ya uume wake ndio yenye nguvu zaidi ya kike na kwa hivyo amefanikiwa kupata watoto wawili. Lakini ndoa yake imekumbwa na misukosuko.

Anasema mke wake ameikubali hali yake ya maumbile lakini upo wakati ambao mkewe hujawa na wasiwasi kumhusu mumewe.

"Hofu kuu kwangu ni kuwa mimi hupata hedhi, na huwa inaandamana na uchungu na damu nzito kuliko kawaida. "

Kero la kutokwa na hedhi ndio mojawapo ya mahangaiko mengi katika maisha ya Sydney kwamba amejitambulisha kuwa mwanamume lakini hupata hedhi.

La pili ni kusemwa na watu na kunyanyapaliwa kutokana na muonekano wake.

"Utamsikia mtu akinieleza na kusema 'yule mume-jike' "

Cha tatu ni kuwa ameshawahi kulazimishwa na watu ambao hakukubali kuwataja waliosisitiza kuwa lazima wavione viungo vyake vya uzazi.


View attachment 1481010View attachment 1481012
Picha ya hayo maumbile
 
#Jewajua : Nyota wa Manchester City Kevin De Bruyne kisheria angeweza kuichezea timu ya taifa ya Burundi iliyofuzu michuano ya Kombe la Mataifa ya Africa AFCON kwa mara ya kwanza mnamo mwaka 2019.

De Bruyne alizaliwa mjini Dronen, Ubelgiji japo mamake Anna ni mzaliwa wa Burundi, ikimaanisha kuwa kiungo huyo anaruhusiwa kisheria kuichezea timu ya taifa ya Burundi iwapo angetaka kufanya hivyo.

Source: DW Kiswahili
1711630007350.jpg
 
#Jewajua : Nyota wa Manchester City Kevin De Bruyne kisheria angeweza kuichezea timu ya taifa ya Burundi iliyofuzu michuano ya Kombe la Mataifa ya Africa AFCON kwa mara ya kwanza mnamo mwaka 2019.

De Bruyne alizaliwa mjini Dronen, Ubelgiji japo mamake Anna ni mzaliwa wa Burundi, ikimaanisha kuwa kiungo huyo anaruhusiwa kisheria kuichezea timu ya taifa ya Burundi iwapo angetaka kufanya hivyo.

Source: DW KiswahiliView attachment 2947227
mmmh
 
Back
Top Bottom