KUMBUKUMBU MUHIMU SIKU KAMA YA LEO KWA MECHI DUME YA SIMBA SPORTS CLUB
Simba Sports Club kama Club kongwe nchini na barani Africa yenye kusheheni mambo mengi sana ni lazima kuwepo na vitu muhimu kama kumbukumbu ambayo haiwezi kuondoka kwenye Wanachama, mashabiki na Wapenzi wa Club ya Simba.
Miongoni mwa mambo mengi ila leo nitakuletea Kumbukumbu moja muhimu sana ya mechi iliyochezwa kipindi hiki ambayo ni historia nzuri sana.
KUMBUKUMBU HIYO
Kombe la CAF wakati huo ilikuwa linachezwa kwa mara ya 3 chini ya ufadhili au udhamini wa aliekuwa mfanyabiashara maarufu nchini Nigeria kipindi hicho aliitwa Moshood Abiola, Tanzania ikawakilishwa na Simba kwa mara ya kwanza.
Ilikuwa ni 18 September 1993 Miaka 17 iliyopita Simba Sports Club iliweza kutinga Nusu Fainal ya Kombe ya CAF baada ya kucheza mechi ya Robo Fainal siku hii na kufungwa 2 kwa bila na USM EL HARRACH mechi ilichezwa jijini Algiers nchini Algeria, hii ikiwa ni mechi ya marudiano huku ya kwanza ikiwa Dsm 05 September 1993 Uwanja wa Uhuru Simba ilishinda Goli 3 kwa 0 magoli ya Simba yakifungwa na Abdul Machine, Edward Chumila na Malota Soma.
Ikumbukwe kuwa kabla ya mechi hii ya Robo Fainal Simba Sports Club iliweka kambi nje ya bara la Africa Jijini NICE - FRANCE.
MECHI DUME YA NUSU FAINAL KIDOGO
Hii ndio ilikuwa moja ya mechi Dume ya Simba Sports Club maana timu iliyokutana nayo ilikuwa ni kifaa hatari sana na ilikuwa kwenye moto wa hatari sana.
ATLETICO SPORTS AVIACAO ya Angola ilikuwa ndio mpinzani wa Simba hawa Walikuwa wanaume wa ukweli.
Mechi ya Kwanza ilichezwa Dsm 17 October 1993 na hapa Simba ndio waliendeleza historia ya NYUMBANI HATOKI MTU kwa kumpiga kama amesimama 3 kwa mtungi hawa Atletico Sports Aviacao baada ya mechi walisema hawaamini matokeo haya kabisa kwani Simba imewashangaza sana hatakaa kusahau hawajawahi muda mrefu kufungwa popote TATU MZUKA KAVU na cha kuvutia zaidi Goli zote 3 kapiga Mwanaume mmoja EDWARD CHUMILA akaondoka na mpira wake.
Mechi ya marudiano ilifanyika Mjini Luanda Angola 31 October 1993 na timu zote kutoka 0 kwa 0 na kuipa Simba nafasi ya kwenda Fainal ya Kombe la CAF ni bonge ya historia ambayo haijakutwa wa kufikiwa mpaka sasa hivyo ni mwiko kufutika kwenye vichwa vya wana Simba.
KIKOSI CHA KAZI ZOTE HIZI 1993 KILIUNDWA NA HAWA
Kocha ni Abdala King Kibaden akisaidiwa na Ettene Eshente huyu alikuwa ni MuEthiopia.
Magolikipa walikuwa Mohamed Mwameja, Mackenzie Ramadhan na Often Martin alietokea timu ya Ushirika ya Moshi.
Wachezaji wa Ndani walikuwa Twaha Hamidu, Fikiri Magoso, Suleiman Pembe, Kasongo Athumani, Godwin Aswile, George Masatu na Deo Mkuki akitokea timu ya Pamba ya Mwanza.
Wengine walikuwa George Lucas, Ramadhan Lenny, Iddy Selemani, Hussein Marsha, Abuu Omari, Joachim Masumbuko na Dua bin Said Akitokea Small Simba ya Zanzibar.
Inaendelea kwa Damian Kimti, Nico Kiondo, Michael Paul, Thomas Kipese, Abdul Ramadhan Machine na hawa David Mihambo na Mbuyi Nyondani wakitokea Reli ya Morogoro.
Kikosi kilimalizika kwa hawa Malota Soma, Edward Chumila, Rashid Abdallah Magongo, Bakari Iddy, Razak Yusuph Careca toka Coastal Union, Feruzi Telu toka Milambo ya Tabora.
MTORI ULIANZA KULIWA TOKA ZAMANI KILICHOBADILIKA NI STYLE TOFAUTI TOFAUTI ZA MAPISHI