Je, wajua kuwa Akili Unde (AI) inaweza kutumika kuwafanya watu kupuuza mchakato wa uchaguzi katika mataifa yao?

Je, wajua kuwa Akili Unde (AI) inaweza kutumika kuwafanya watu kupuuza mchakato wa uchaguzi katika mataifa yao?

JamiiCheck

JF-Expert Member
Joined
Nov 3, 2023
Posts
213
Reaction score
226
Mdau,

Je, wajua kuwa Akili Unde (AI) inaweza kutumika kuwafanya watu kupuuza mchakato wa uchaguzi katika mataifa yao?


Mwezi Januari 2024, maelfu ya wanachama wa chama cha Democratic nchini Marekani, katika jimbo la New Hampshire, walipokea simu ya roboti (robocall) yenye sauti inayofanana kabisa na ya Rais Joe Biden, ikiwashauri wasishiriki katika uchaguzi wa awali, bali wasubiri hadi uchaguzi mkuu wa Novemba.


Kwa wengi, ujumbe huo ulionekana rasmi na wa kuaminika — maana ulitolewa kwa sauti ya kiongozi wao mwenyewe.


Lakini baadaye iligundulika kuwa sauti hiyo haikuwa halisi. Ilikuwa ni sauti ya kughushi iliyotengenezwa kwa teknolojia ya AI, iliyolenga kuwarubuni wapiga kura wasijitokeze.

Kwa mujibu wa The cairo review wanaeleza kuwa
Sauti hiyo ilitengenezwa kwa kutumia AI (Akili Unde). Wahusika wa jaribio hili la kuingilia mchakato wa uchaguzi walikuwa:
  • Steven Kramer, mshauri wa kisiasa
  • Paul Carpenter, ambaye alilipwa dola 150 kutengeneza sauti feki
  • Kampuni ya mawasiliano ya simu iitwayo Lingo Telecom

Paul Carpenter alitumia ElevenLabs, jukwaa linalotoa huduma ya kunakili sauti papo hapo (voice cloning) kwa gharama ya chini hadi dola 5 kwa mwezi.

Aaron Jacobs, msemaji wa kundi la Write-In Biden, alisema katika taarifa kuwa:

“Huu ni upotoshaji wa taarifa kwa kutumia teknolojia ya deepfake uliolenga kumdhuru Joe Biden, kuzuia watu wasipige kura, na kuharibu demokrasia yetu.”

Source CNN, The Cairo Review
 
Back
Top Bottom