Je wafanyakazi wa serikali wapo chini ya Ccm?

ungonella wa ukweli

JF-Expert Member
Mar 27, 2012
4,210
555
Habarini wana jf. Kupitia maelezo mengi ya viongozi wa ccm na makada wao, huiaminisha jamii kuwa kwa vile ccm ni chama tawala,na ccm ndo inaunda serikali, basi wafanyakazi wa serikali wapo chini ya ccm. Je hili lipoje? Na kama sheria zetu zina mapungufu nini kifanyike?. My take: jambo hili lisipowekwa sawa linaweza pelekea vurugu kwenye taifa letu. Kwa sababu wafanyakazi hulipwa kwa kodi za wananchi wa vyama vyote na hata wasio na chama! Nawasilisha.
 
Sijui umetoroka mirembe au vipi embu rudia kulipitia swali lako halafu wahi hospital iliyopo karibu yako.CCM ndoo iliyomba kura kwa wananchi itengeneze Serikali na wakaaminiwa wakapewa mamlaka hiyo.Na wao ndo watakao ulizwa na wananchi.
 
wafanyakazi wa serikali ni wachache sana wenaoipenda ccm labda mafisadi lakini kama wanachama ccm inaojidai nao kama ni pamoja na wafanyakazi imepotea njia. wakibisha wapige kura za siri waone. ebu waseme wafanyakazi wangapi wanalipia kadi zao na wenye kadi zao? waache ku assume wafanye utafiti kwa kupiga kura za siri katika ukumbi utakao kusanya wafanyakazi wote waone matokeo. wafanyakazi vihio ndiyo wanabembeleza ccm
 
Asilimia zaidi ya 80 ya watumishi wa uma wanaichukia ccm. Katiba mbovu na njaa inachangia wao kutojionyesha wazi
 
wafanyakazi wa serikali wanafanya kazi kulingana na taratibu, kanuni, sheria na miongozo ya kazi ambayo ipo siku zote. CCM haiweki miongozo ya kazi bali ina sera fulani fulani ambazo wafanyakazi huijikuta wakizitekeleza. mfano ccm ikiamua kuwa wanafunzi wote wa darasa la saba waende sekondari walimu watakabiliwa na shida ya kujaa kwa madarasa, ukosefu wa vifaa, upungufu wa walimu n.k. Kwa hivo watumishi wanaweza kubeba mzigo au kupata nafuu fulani kulingana na sera zilizopo. wanaweza wakalalamika au wakafurahia mambo fulani fulani. hivo siasa inapaswa iwaachie wataalamu wapange na sio kujigamba eti wafanyakazi wako chini yao
 
Sijui umetoroka mirembe au vipi embu rudia kulipitia swali lako halafu wahi hospital iliyopo karibu yako.CCM ndoo iliyomba kura kwa wananchi itengeneze Serikali na wakaaminiwa wakapewa mamlaka hiyo.Na wao ndo watakao ulizwa na wananchi.
mkuu nadhani wewe uanze kwenda mirembe,kwani haujajibu swali,badala yake ni mipasho!
 
Back
Top Bottom