Je waafrika tulistahili utumwa?

Je waafrika tulistahili utumwa?

Kikusya

JF-Expert Member
Joined
Oct 2, 2011
Posts
277
Reaction score
389
Kitu gani tufanye kikubwa na chenye akili ili tuonekane na sisi ni binadamu wenye vipaji vikubwa na hatukustahili kuuzwa kama mbuzi enzi za utumwa?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu hayo mambo ya utumwa yameshapita, tupambane na hali zetu mkuu
 
Inasikitisha sana kuona Maprofesa wetu ambao tulitegemea watutoe kwa aibu hii, ndiyo kwanza wako kwenye siasa na kuacha vyuo vyetu bila wabobeaji ambao wangegundua chanjo za malaria, ukimwi na kipindupindu.
Fikiria magonjwa haya yangekuwa yanawa athiri wazungu kwa kiwango kikubwa!!!!! Tiba na chanjo vingepatikana muda mrefu.
Tatizo letu hatuoni kama ni tatizo. Matatizo yetu tunafikiri yatatatuliwa na mataifa mengine.

Kwa mfano viongozi wetu kukimbila kutibiwa nje miaka nenda miaka rudi. Je hili siyo tatizo? Mambo ni mengi yanakera sana lakini hatujatambua kama ni tatizo.
Fikiria ungekuwa wewe una design mashine ya kukatia mbao au mti , cha kwanza ungekipata toka kwa wenzako ni kukuita mvivu . Lakini wenzetu waliliona ni tatizo kukata mti kutumia shoka na leo ni sisi wenyewe wa kwanza kuagiza machine hizo, halafu tunakata miti mpaka basi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kabla ya kuja wazungu na waarabu, utumwa ulikuepo Africa.

Every man was born free. Hakuna anaestahili kua mtumwa!

Hayo mengine ya siasa nawaachia wengine!

- KANA -
 
Usishangae africa kuingia utumwani kwani hata marekani waliingia utumwani na walitawaliwa.
Nahisi hizo ni hatua au stage za world civilization. That's why we're here today!!!!!! God Bless Tanzania.
 
Back
Top Bottom