Je vita ya wakuu wa mikoa na wananchi, wakuu wa mikoa wataiweza?

Fasta fasta

JF-Expert Member
Feb 15, 2011
1,126
725
Ndugu watanzania mliopo hapa Jf ninadhani kitendo cha wakuu wa mikoa naJeshi la Polisi na Mahakama kudhulumu haki za watanzania ni kitendo cha kulaani mpaka kufa. Huu ubaguzi wa aliye nacho na asiekuwa nacho utaendelea mpaka lini? Mababu na mabibi zetu, na baba na mama zetu walivumilia sana kwa kunyimwa elimu, na sisi tuseme basi na wao CCM sasa watuvumilie.

Tunajitahidi kusomesha vijana wetu leo kufa na kupona ili wafanye nini, tujiulize,kama mashirika yamekufa na makampuni yote ya serikali na bado vijana wanahangaika kufungua maduka mikononi, kutembea na maduka mikononi serikali isiyokuwa na haya inakwenda kuwafetulia risasi, kuwapiga mabomu, na wasivyokuwa na utu, ubinadamu na akili zao zenye ndoto yakupenda madaraka wanawamwagia raia wenzao maji ambayo wanajua yanamadhara, yana sumu yakiingia mwilini. Sasa ni najiuliza vijana wetu wafanye nini ili wapate kipato kama watu wengine.

Hii serikali inajivunia nini kwa taifa letu leo hii ndugu zangu. Tunajua ya kuwa Tanzania tuna vitu vingi tu ambavyo serikali ingetilia maanani tungekuwa mbali kuliko hata Kenya. Nikitoa mfano tulikuwa na mashirika ya umma ambayo serikali isingekuwa legelege kuyaongoza haya matatizo tunayoyaona leo yasigekuwepo vijana wengi wangekuwa na ajira.

Leo hii hakuna hata shirika moja linalosifika hapa Tanzania, yote ni marehemu imebaki mifupa wamechukua ile minofu yote, halafu tukiuliza tunaambiwa tunavunja sheria. Pamoja na majonzi yote ya maisha magumu kwa watanzania, wakuu wa mikoa wanatutangazia ya kuwa ndio wamekabidhiwa nchi, kuliko hata yule aliyechaguliwa na wananchi, wakati haya mashirika yalifia mikononi mwao wakiwa wanaangalia,leo wanatuambia ni wakuu wa kamati ya maadili ya kupambana nawananchi wanapotafuta haki yao, ni kwa nini wasigepambana na serikaliya CCM kuuliza ajira za hawa vijana?

Tunaombakila mkoa uliokuwa na shirika waaze kudai ili na sisi tuweze kupataajira kama wao na akina Rejea walivyopata ajira humu JF.
 
Mi naona siasa zimewatawala badala ya ethics za administration.
Kwa mfano mikoa ya Arusha na Mbeya, MaRC wamekosea kuanza kwa ubabe.
Hii mikoa haitishiwi nyau bana, aende kule pwani kwa waswahili unamchimba mtu biti anagwaya, mikoa hii ni ya wagumu, unapiga mkwara wanakupa advertise namna watakavyo react na wewe saa ikifika.
Kandoro muulize mzaliwa Mwakipesile hiyo ngoma inachezwaje na Bwana Magessa Arusha si mchezo uliza wenzio waliopita kama mzee Shirima, we hata manispaa inatosha kukunyima ucingizi, badilikeni, ongozeni. Kwa ubabe hamtoboi!!!??
 
Mkuu,
Hapa tulipofikia kwa hizi siasa uchwara za CCM hatuwezi kuvumilia. Wao wanajua ya kuwa wametufikisha hapa lakini bado wanazububu kutoa amri ili watu wafungwe mdomo. Kama walikuwa wakuu wa kamati ya maadili waliruhusu vipi hizi mali za watanzania zikaendeshwa kizembe.

Bado niya yangu ipo palepale mikoa ishirikiane kudai haya mashirika waliyokuwa nayo. Nimefurahishwa sana na mbeya walivyokuwa wawazi bila kutafuna walivyotaka mkurugezi aridishe pesa zao za maji.
 
Back
Top Bottom