Je utumie program gani | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Je utumie program gani

Discussion in 'Tech, Gadgets & Science Forum' started by Yona F. Maro, Feb 13, 2009.

 1. Yona F. Maro

  Yona F. Maro R I P

  #1
  Feb 13, 2009
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 4,237
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Watu wengi makazini shuleni na sehemu zingine hawajui haswa wanatakiwa programu gani kwa ajili ya matumizi ya kawaida ya kazi zao za siku zote kutokana na ujuzi au utaalamu wake mfano mfamasia anatakiwa awe na programu yake maalumu kwa ajili ya masuala yake ya ufamasia , dakatari wa meno , fundi wa magari na kadhalika

  Katika mfululizo wa makala za Unatakiwa kutumia nini najaribu kupata programu mbali mbali kuzifanyia kazi na kuandika kidogo kuhusu programu hizo kwanza tutaanza na hizi chache ambazo zinajulikana na watu wengi na vile vile rahisi kuzipata kwa nchi za afrika ya mashariki .

  Kuna wale ambao kazi yao ni kuandika tu mambo mbali mbali unaweza kutumia programu za office kuanzia microsoft office 2003 mpaka 2007 ingawa sasa hivi kuna toleo jipya la office 2008 profesional hii haijaanza kusambazwa rasmi katika nchi za afrika ya mashariki hizo nilizotaja kuanzia 2003 mpaka 2007 ni rahisi kupatikana kwa mjini

  Ndani ya office 2007 profesional unapata vitu kama microsoft access hii ni kwa wale wa database , excell hii inahusu zaidi mambo ya hesabu inforpath , office onenote , publisher power point pamoja na microsoft project , project ina husu zaidi wahandisi utaona zaidi baadaye kama programu za microsoft zinakuwa garama sana kwako unaweza kujaribu open office hizo ni bure unahitaji muda wa kudownload tu .

  Sasa kama ni kazi za kuchapa unataka kulinda kazi zako unazoandika ufanye nini ? kuna programu kama Adobe Acrobat Proffesional 9 hili ndio toleo jipya ila zinazopatikana kwa wingi ni version 6 mpaka 7 , 8 ipo kuna watu wengine waliwahi kulalamika ina wasumbua kidogo mwaka jana sijaweza kujua hali ikoje mpaka sasa hivi kama usumbufu ni ule ule au la , naipenda 9 nimeitumia na kuona uzuri wake katika utendaji

  Una documents zako unataka kuiweka katika mfumo wa pdf hiyo itafanya hivyo au unataka kuweka protection zingine zozote zile hiyo itafanya vyote hivyo unavyotaka wewe pamoja na kuweza kugeuza pdf kwenda word na kadhalika pia kuna tovuti inayoitwa www.pdfonline. com katika tovuti hiyo unaweza kufanya yote hayo ukiwa online .

  Wakati mwingine umeshafanya kazi zako nyingi unataka kuzikusanya pamoja na kuhifadhi ufanye nini ? kuna programu inaitwa winrar , winzip programu hizi zinaweza kukusaidia kuzip files zako katika folder moja zijawahi kuona virus wanaoshambulia winrar ila wako wanaoshambulia winzip kwa urahisi au unaweza kuzihifadhi kwa kutumia programu nyingi inayoitwa folder lock .

  Kama unatengeneza kurasa na vitu vingine vya kiofisi zinazohusu kurasa , ni vizuri utumie Adobe PageMaker kwa sasa kuna hadi version 7.5 , kuna microsoft Publisher , Corel Draw 12 , Adobe Illustrator ni wewe tu na utaalamu wako au utundu wa kuweza kuelewa vitu zaidi

  Unaweza kupatiwa picha ukaambiwa upunguze hiki na kile , wengi wamezoea photoshop kwa sasa kuna hadi photoshop cs4 ambayo ni portable ukiwa na hii hauhitaji kuinstall inakuwa ndani ya flashdisk unaweza kuitumia moja kwa moja kama sio mtaalamu sana unaweza kutafuta paint shop kuanzia 9 na kuendelea au Corel paint

  Hizo kazi zote unazozifanya zinatakiwa kupangiwa muda na wakati mwingine unapenda kupendezesha desktop yako unayofanyia kazi si ndio ? kuna programu inaitwa webshots hiyo ina sehemu ya muda , inakuletea picha za sehemu mbali mbali duniani toka katika mtandao wao ingawa unaweza kuweka zako pia au unaweza kutumia google desktop moja ya uzuri wa programu hii ni kwamba ina saa , ina sehemu ya kuangalia hali ya hewa ya sehemu mbali mbali , ina sehemu ya note pad ( kama unafanya kazi zako au unafanya maongezi hauhitaji tena note pad ya karatasi google desktop itakusaidia bila shida )pamoja na kisehemu cha kukukuletea habari zinazoendelea duniani katika mfumo wa rss feed , kutoka vyombo vya habari mbali mbali duniani hata breaking news

  Ukiwa umekaa hapo hapo katika computer yako halafu unataka kutembelea maeneo mbali mbali duniani , unatakiwa utafute programu inayoitwa google earth , programu hii imeboreshwa zaidi katika nchi za ulaya na baadhi ya asia hata afrika lakini chache , ukitaka kujua hali ya hewa kilimanjaro na kujua kinachojiri kila baada ya muda fulani kwa picha za angani sio lazima uende kilimanjaro tena ukiwa na google earth unafanya yote hayo .

  Kwa leo tunaishia hapo tuungane siku nyingine katika muendelezo wa makala hii ahsante kwa kusoma mpaka hapa

  Kwa maswali au maelezo zaidi unaweza kuniandikia hollymaro@gmail. com Karibu
   
 2. Buswelu

  Buswelu JF-Expert Member

  #2
  Feb 14, 2009
  Joined: Aug 16, 2007
  Messages: 1,989
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  Nataka kuanza download Series kwenye internet...kama 24Hrs,Prison Break,....nitumie program gani?BIT Rocket nimeshidwa download.
   
 3. Yona F. Maro

  Yona F. Maro R I P

  #3
  Feb 14, 2009
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 4,237
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Ni bora uingie katika tovuti ya series hiyo utaweza kupata njia sahihi za kuweza kupata hizo series na vingine unavyotaka

  thanks
   
 4. Yona F. Maro

  Yona F. Maro R I P

  #4
  Feb 22, 2009
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 4,237
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  JE UTUMIE PROGRAMU GANI ?
  Karibu katika sehemu ya pili ya makala JE UTUMIE PROGRAMU GANI ? katika sehemu hii nitaendeleza program ambazo mtumiaji wa kawaida tu wa computer anatakiwa ajue ambazo zinaweza kurahisisha kazi zake zaidi – hapo mwanzo tuliona program za adobe na Microsoft zinavyoweza kurahisisha kazi za mtumiaji ahsante kwa wale ambao walitoa maoni yao .
  Kuna watu wengine mpaka leo bado wanabeba kamusi zao za oxford na wachapishaji wengine kwa ajili ya matumizi yao ya kiofisi hawajui kwamba kuna programu maalumu kwa ajili ya kutafsiri maneno na sentensi mbali mbali unaweza kutumia www.yale.edu/kiswahili ukiingia tovuti hiyo unaweza kutafsiri haswa kwa Kiswahili na kiingereza kuna www.google.com/languagetools tovuti hiyo unaweza kutafsiri sentensi nzima au hata kurasa nzima zamani ilikuwa haina lugha ya Kiswahili .
  Unaweza pia kutumia kamusi ambazo zinaongea pia jaribu Babylon kwa sasa kuna version 7.3 hiyo ni ya kisasa zaidi inakuwezesha kutafsiri neno kwenda lugha zaidi ya 30 duniani pamoja na kuongea yaani audio kama wewe ni mtundu zaidi unapenda kutengeneza sauti zako kuna program inaitwa textaloud hii inakuwezesha kusema au kuongea nano unalochapa ina sauti mbali mbali kuanzia za kike kiume na hata kutambua Sauti .
  Siku za karibuni kumetokea tovuti mpya inayoitwa Dicts unaweza kutumia tovuti hii kama kamusi pia lakini moja ya kitu kilichonivutia zaidi ni kwamba ina huduma ya kamusi pamoja na lugha kama unatafuta kitu inauwezo wa kukuonyesha kitu hicho unaweza kukipata wapi katika mtandao
  Kama ulisoma makala iliyopita haswa katika mambo ya pdf niligusia kuhusu pdf online unaweza kugeuza nyaraka kwenda pdf nakadhalika leo kuna tovuti inayoitwa pdfvia Send PDF Files with Ease | PDFvia.com katika tovuti hii unaweza kutuma file za pdf kwa watu wengine tofauti na pdfonline hii unaweza kushare nyaraka hizo ili wengine waweze kuziona popote walipoduniani badala ya kutumia kwa njia ya mtandao .
  Kwa wale watu walio nchi za magharibi haswa marekani watembelee TrapCall - Unmask Blocked Calls katika tovuti hiyo unaweza kuona private number zote zinazokupigia au ulizowahi kupigiwa lakini lazima ujiunge na huduma hiyo sikupenda kuweka link hiyo hapa wala kuielezea chochote ila imekuwa hivyo
  Baadhi ya watu wanapenda kuwasiliana kwa siri sana haswa kwa kutumia mitandao ukitembelea Email Privacy with StealthMessage.com inakuwezesha kuwasiliana na watu wako kwa njia ya siri sana bila mtu wa 3 kujua kinachoendelea kama mko katika mazingira ya domain katika maofisi
  Katika sehemu za afya kama hospitali na zahanati wahudumu na madaktari huwa wanapata taabu sana kwenda katika mitandao mbali mbali kutafuta misaada mbali mbali ukitembelea Welcome - Medpedia inaweza kuwa msaada mkubwa sana kwako kwa wale wataalamu wa biologia kuna program inayoitwa Biosolveit.
  Niliwahi kuona sehemu moja mtu akilalamika kazini kwao wamewazuia kutumia mtandao lakini anataka awe anasoma email zake wakati wowote anaotaka kuna program inaitwa gmail config hii ni mali ya gmail inakuwezesha kudownload email zako zote za gmail na kuzisoma bila kutembelea mtandao wa google , au unaweza kutafuta program inayoitwa invisible surf hii pia inaweza kutumia – programu zote hizo unatakiwa kuinstall maana yake lazima uwe na admin permissions ili uweze kutumiza hayo malengo na huo mtandao uwe blocked na program nyingine na uwe umeunganishwa kwa njia moja au nyingine
  Ukishamaliza kazi zako unapenda kupumzika sasa kuangalia luninga kwa njia ya mtandao si ndio tumbelea Sling - Browse Shows Alphabetically ina link ya televisheni na vipindi mbali mbali unavyoweza kuangalia au kama unataka tu kutazama video na kadhalika unaweza kutembelea YouTube - Broadcast Yourself.
  Je utapataje video unazotazama katika youtube ? fungua YouTube - Broadcast Yourself. katika search andika mfano Part Time Lover – Steve Wonder , hiyo itakuwezesha kuplay hiyo nyimbo kama unataka kuichukuwa kuihifadhi katika flashdsk au computer yako tembelea KeepVid: Download and save any video from Youtube, Dailymotion, Metacafe, iFilm and more! angalia katika address bar ya youtube utaona anuani ya nyimbo hiyo ambayo ni YouTube - Stevie Wonder - Part Time Lover chukuwa anuani hiyo fungua KeepVid: Download and save any video from Youtube, Dailymotion, Metacafe, iFilm and more! paste katika sehemu iliyoandikwa URL kisha click download utaona maelezo jinsi ya kudownload video hiyo
  Kwaheri kwa sasa tuonane katika makala ujayo ya JE UTUMIE PROGRAMU GANI

  Yona F Maro
  DUTY HAS NO SWEET HEARTS
  Dar es salaam
   
 5. Yona F. Maro

  Yona F. Maro R I P

  #5
  Feb 23, 2009
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 4,237
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  JE UTUMIE PROGRAMU GANI – 3
  Karibu katika sehemu ya tatu ya makala JE UTUMIE PROGRAMU GANI ? kumbuka tu haya ni maoni yangu mimi simwakilishi mtu wala kampuni yoyote unapoamua kutumia programu hizi zikileta matatizo yoyote mimi sintohusika kwa chochote .
  Mara nyingi kabla ya kuamua kutumia programu yoyote hakikisha matakwa yake yanaendana au kulingana na computer yako mfano unapoamua kutumia antivirus hakikisha computer hiyo haina tatizo lingine linaloweza kusababisha antivirus yako isifanye kazi
  Matatizo yanayotokana na antivirus kutokufanya kazi inavyotakiwa ni kwa mfano memory ndogo – unapokuwa na norton antivirus 2009 imeandikwa memory ya computer yako iwe angalau 256 mb , processor angalau Pentium 4 ya 1.8 haitosumbua ukiwa na chini ya hapo ujue unatafuta tabu kwa aliyekuulizia na wewe binafsi lazima itakuwa slow na kuibua mengine .
  Saa zingine computer hiyo inaweza kuwa na virus wengine pia au ina spyware au kuna programu ambazo hazifanyi kazi vizuri zinazohusiana katika utendaji wa antivirus mfano kama unatumia outlook au outlook express halafu ikawa inashida labda imecorrupt bila wewe kujua programu hii utendaji wake wa kazi unaingiliana na norton
  Maana yake norton haitofanya kazi ipasavyo haswa unapotaka kudownload emails zako haitoweza kuscan virus wataingia na kusababisha matatizo makubwa zaidi mwisho wa siku utasema norton si nzuri
  Au kama wewe ni mtu wa graphics kila programu unayotumia mfano adobe photoshop , corel , maya au paintshop imeandikwa uwe na memory si chini ya mb 512 processor angalau kuanzia ghz 2.0 uwe na nafasi kubwa katika harddrive yako kuweza kuhifadhi kazi zako na kadhalika usipofanya hivi lazima siku moja lawama zitaanza .
  Kitu kingine cha kutilia maanani zaidi kumbuka kununua au kuwa na programu ambazo ni halali sio bandia au kutoka kwenye source ya kuaminika ambayo unaweza kupwa support muda wowote unapotaka wewe kuhusu bidhaa uliyonunua – unaponunua programu hizi wenyewe wanakupa huduma ya support bure kabisa na hata tanzania kuna kampuni ni dealers wa baadhi ya bidhaa hizo kwahiyo unaonana nao tu .
  Mwisho kumbuka programu unaponunua na kuweka katika komputer yako inakuwa outdated unatakiwa kuiupdate kwahiyo chemeka katika mtandao ufanye update ya programu hiyo pamoja na komputer yako kila wakati unapopata muda .
  Wengi wanaogopa gharama za mtandao kama ni hivyo unaweza kutumia broadband ambazo nyingi ziko katika internetcafe au tembelea tovuti inaitwa Patch unaweza kudownload update mbali mbali manual na kwenda kuingiza katika computer yako na mwisho ni kutembelea tovuti ya bidhaa husika ujue kama kuna update yoyote imetoka au lah .
  Kama unatumia windows vista mfano hakikisha umeifanyia activation kupitia mtandao na microsoft kama ni windows xp nayo unafanya hivyo hivyo ili iweze kupata huduma za support kwa urahisi zaidi chochote kikitokea .
  Programu yoyote unapotaka kutumia lazima uwe katika account ambayo inakuruhusu kufanya hivyo maofisini ulizeni technical support wenu ndio watu wa karibu zaidi
  Ahsante kwa kusoma mpaka hapa

  Yona F Maro
  Duty has No SweetHearts
   
 6. Yona F. Maro

  Yona F. Maro R I P

  #6
  Mar 2, 2009
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 4,237
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  sehemu ya 4 ya makala hii imetoka tafadhali angalia attachment
   
 7. Tumsifu Samwel

  Tumsifu Samwel Verified User

  #7
  Mar 5, 2009
  Joined: Jul 30, 2007
  Messages: 1,406
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  nakuchauri utumie Bittorent ni nzuri sana ni ipo fast kuliko badhii ya p2p nyingine ,Unaweza kutumia link hii http://isohunt.com/torrents/?ihq=prison+break+season+4
  kudownload series yoyote unayo taka kudownload au movie.
   
 8. Yona F. Maro

  Yona F. Maro R I P

  #8
  Mar 8, 2009
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 4,237
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Karibu tena katika Mfululizo Wa makala nyingine ya JE NITUMIE PROGRAMU GANI ? katika sehemu hii kama ilivyo ile iliyopita siendelei na programu za kutumia bali nitaendeleza baadhi ya vitu tunavyokutana navyo katika matumizi ya programu mbali mbali ambavyo inabidi vieleweke kwa wengine ili wawe na uwelewa kisha kufanya maamuzi sahihi huko mbeleni .
  Kuanzia mwaka uliopita kumekuwa na ongezeko kubwa la matumizi ya kitu kinachoitwa PORTABLE APPLICATIONS au PORTABLE APP hizi ni programu za komputa zinazoweza kufanyakazi kutokea katika vifaa kama CD ROM , Flashdisk , flashcard au Floppy Disk . Hizi programu hizi kuweza kufanya kazi kutokana na matakwa yake bila hapo hazitoweza kufanya kazi .
  Pia unaweza kuikopy programu hiyo kuweka katika computer na kuitumia sio lazima iwe cdrom au flashdisk na aina nyingine za media
  Kuna watu wana computer nyumbani na makazini pamoja na shule lakini wanapata taabu sana katika au gharama nyingi sana wanapotaka kuinstall programu fulani fulani kama programu hizo zingekuwa portable utazibeba katika flashdisk tu au cd tu na kwenda kutumia moja kwa moja bila kuinstall katika computer yoyote ila lazima uwe na administrators access .
  Mfano kuna programu kama Adobe Photoshop CS4 programu hii ina ukubwa wa zaidi ya mb 350 inahitaji memory kubwa , muda kuingiza katika computer lakini ukipata portable application yake ambayo ni mb 60 katika flashdisk au cd unaweza kuitumia popote bila shida yoyote


  Ukitembelea katika mitandao mbali mbali utakutana na program kama ABIWORD hii inaweza kufanya kazi karibu zote za Microsoft word ina ukubwa wa mb 6 , openoffice ambayo ni mb 65 kama unatazama au kutumia sana pdf kuna Programu inaitwa SUMATRA pamoja na Fox Reader .
  ALL IN ONE mara nyingi hii inatumika sana katika Hardware kama Printers , Photocopy na vifaa vingine vinavyoweza kufanya kazi zaidi ya 2 na kuendelea katika printer wengi wamezoea 3 IN 1 yaani Scanner , Printer pamoja na FAX unakuwa na printer yenye uwezo wa kufanya vyote hivyo ila athari zake ni kwamba mfano scanner ikipata matatizo inawezekana printer yote ikawa ndio mwisho wake mara nyingi huwa hivyo na wataalamu wake wako wachache sana gharama zake kuziendesha ni kubwa kidogo je ungependa kupoteza scanner na printer kwa wakati mmoja ? FIKIRIA FANYA MAAMUZI SAHIHI
  Kwenye ulimwengu wa programu kuna ALL IN ONE hizi ni program ambazo zinakuwa na vitu vingine zaidi au vya ziada katika ufanyaji wa kazi ingawa nyingi zimekuwa ni kubwa na imekuwa karaka kwa watu wengine wale wanaokuwa wanataka kitu kimoja tu katika program husika ila kwa wengine ni shangwe kuu .
  Wengi tunaotumia Antivirus mfano tunapatwa na Spyware na vitu vingine vingi katika mitandao ambavyo vinahitaji program nyingine za ziada kuweza kuvishugulikia ukitumia programu katika Norton INTERNET SECURITY 2009 hii ni programu mfano wa ALL IN ONE ina vitu kama Privacy Protector ambayo inaweza kulinda privacy yako unapotembelea mtandao wowote ule na kama mtandao huo ni wa ajabu au haueleweki basi inakupa onyo kama site advisor tofauti yah ii unaweza kuweka password tovuti zote unazotembelea .
  Siku za karibuni kampuni nyingi sana zimekuwa na programu zao ambazo ni ALL IN ONE na sio programu za antivirus pekee yake
   
 9. Y

  Yassin JF-Expert Member

  #9
  Mar 10, 2009
  Joined: Jul 23, 2008
  Messages: 326
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Asante sana mkuu kes msaada wako zaidi!!
   
 10. Kuntakinte

  Kuntakinte JF-Expert Member

  #10
  Mar 10, 2009
  Joined: May 26, 2007
  Messages: 704
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Mkuu Shy, nashukuru sana maana vitu kama hivi ndio vinatakiwa ndani ya Jamii yetu (Darasa Huru) watu wengi wanajidai wanaelewa kwa ubabaishaji tuuu ila ukiangalia ukweli watupu hasa kwenye utumiaji wa program za kompyuta kwenye kazi za kila siku. Kwa jinsi ulivyoelezea nafikiri wengi wetu tumefunguka macho. Keep it up Bro asiye na macho haambiwi tazama
   
Loading...