Je, utapeli unaoendelea kwenye yard za kuuzia magari, wamiliki wanashirikiana na matapeli? Polisi nao je?

affimation

Member
Jan 25, 2019
48
104
Kwanza sipo hapa kuharibu biashara za watu au kuhoji utendaji wa Jeshi la Polisi, ila nazungumza lipo.

Kumekuwa na utapeli mkubwa unaoendelea kwenye Yard za kuuzia magari, na huu umekua ukiendelea miaka na miaka, na bila wahusika kushugulikiwa.

Swali, je hawa matapeli wanashirikiana na wamiliki wa yard, na vipi kuhusu Jeshi la Polisi, kwasababu kuna kesi zipo miaka na miaka bila wahusika kukamatwa.

Yard zinazoongozwa kwa watu kutapeliwa ni hizi za Kinondoni na hizi za kutoka Morocco kuja Victoria, chunga sana hapo.

Kinachoendelea ni hiki: Mfano umekua ukipita kuangalia gari kwenye yard, matapeli wameshakuona muda mchache wameshajua wewe unatafuta gari gani, wataanza kukufuatilia. Pili, mfano umetangaza sehemu yoyote unatafuta gari, ukaacha contact basi jua na hapo matapeli watakutafuta. Tatu, sijui wananusaje, ukishaanza kutafuta gari, kuwa makini wanaweza kukunusa.

Kinachoendelea ni hiki, mfano umetangaza unatafuta Noah labda ya Milioni 10 basi utapigiwa simu nyingi, na mojawapo inaweza iwe ya matapeli. Sasa tapeli anakuambia Noah yard au kuagiza ni Milioni 14 ili kuna za bondi ambazo zipo kwa Milioni 9, unarushiwa na picha nyingi za Noah amabzo zipo kwenye zile yard.

Sasa tamaa inaanzia hapo kuagiza ni 14m kwa mtu, labda namba C ni Milioni 8, ngoja nikazichek hizi za bondi za Milioni 9 ukishakuwa na wazo kama hilo umeshaanza kuingia mkenge.

Ukishawatafuta watakupeleka kwenye zile yard kama ile picha yadi ipo pale Kinondoni watakupeleka pale, hizi za pale Victoria kuwa makini sana.

Ukishakutana nao pale utakagua gari vizuri kabisa, na kupewa funguo na kuwasha kabisa kitu iko mang'anyu. Basi utaongea nao pale wakupunguzie pamoja na usajili basi utakubaliana nao. Kosa linakuja pale unapotaka kuamini kuwa ni zaidi ya bondi mtu akitakiwa kulipa iwe bandarini au popote.

Watakuambia upewe akaunti namba ya kulipia usajili uanze, ukienda kulipia bank amini umeshaumia. Au wanajifanya wana mwanasheria wao feki mkaandikishane, hapo pia ukiwapa cash uneshaumia.

Kwanini nimewaweka wamiliki wa yard humu, wanajua huu utapeli upo. Je, kwanini wanaruhusu mtu kuja kukagua na kumpa mpaka funguo, bila kumwambia aingie ofisini (japo hapo si lazima) ila kwasababu ya utapeli ni viziri aingie ofisini.

Kwanini nimewaweka Jeshi la Polisi humu, huu utapeli wameshajua upo na unaendelea!

Ukweli ni kwamba hatua hakuna wanazozichukua. Pili, mtu akishatapeliwa utafuatilia wee polisi mpaka utachoka.

Sasa mfano polisi mmeenda mpaka benki mkaonyeshwa CCTV ya yule tapeli, na mkafuatilia mpaka mkapata na leseni ya udereva ya mhusika, na bado hamna kitu, mkapata taarifa za matapeli na sehemu wanazokaa mnamwambia alietapeliwa aweke mafuta! Ukweli ni kwamba Jeshi la Polisi linajua huu utapeli, ila sijui nini kinaendelea.

Kama unataka ushahidi nenda Osterbay Polisi utakutana na hizi kesi nyingi. Nina visa vingi ila kuna jamaa anafuatilia kuanzia mwaka juzi, kuna wengine miaka na miaka zipo.

Kilichonikumbusha huu utapeli ni kwamba, kuna jamaa alinitumia pesa toka mkoani nimtafutie Noah old model used kwa 11M, basi nikawa namtafutia, siku ya kwanza akafikia hotelini tukakosa gari, siku yapili tukakosa, bado tuko tunatafuta Noah na madalali, loo jamaa sijui matapeli walinusa vipi.

Wakamwendea yule mteja sisi hatujui, wakamwambia kuna za bondi zipo kwa 9M jamaa kusikia hivyo akasema sisi tunamyeshusha akaenda kuona gari yadi za kule Victoria, akakutana na jamaa kama Mpemba pale, akaonyeshwa gari kitu chasses na usajili 9M huku mimi nina Milioni 11 yake kwenye account, akanichek na kuniambia amepata gari, tukutane bank Mlimani, basi tukakutana pale, mimi nipo na jamaa yangu ambaye tulikuwa tunamtafutia, yeye yupo na wale matapeli kwenye gari akashuka na document feki za ile Noah, pamoja na account namba.

Amesema amepata Noah chases ya 9M tukasema wapi na wapi, means walengaji wote town hawajaiona?

Tulibishana pale akasema pesa ni zake tumpe, kusoma zile documents chases haziendani na Noah! nikamwambia twende tukaone gari, wale matapeli wanasema mnamchelewesha tu mwenzenu, jamaa nae akasema sisi siyo, nikamwambia pesa ipo kwenye account yangu, sitoi hiyo pesa hata uniue ila lazima nione kwanza gari, nitalipia bajaji twende tukaione. Tukaita bajaji wale madalali wakasema nyie tunawafuata nyuma, sisi kwasababu tulivurugana tukapanda wote kwenye bajaji, wao wakawa anakuja nyuma, basi kwenye bajaji hakuna kuongea.

Kufika kwenye yard bado ile Noa ipo, kusubiri wale jamaa hawajatokea mpaka leo. Pale tukamkuta Singasinga mwingine hapo tunaanza kukagua ile gari, anatuuliza vipi, tukamwambia tulitaka kulipia hii gari, akasema niliwanona mnaangalia, Noah ni 14M, tukamwambia tulishakagua tumepewa account tukalipe, akatuuliza duh mlishalipa tukamwambia bado akasema mshukuruni Mungu, wale ni matapeli!

Jamaa mwenye pesa aliangua kilio palepale akasema nimedunduliza sijui ningesemaje, mimi natangulia home mkoani mtaniletea gari!

KUNA MENGI YA KUJIFUNZA, ILA UKIENDA KUONYEHSWA GARI YARD, IWE NA MTU YOYOTE HATA NDUGU YAKO, HAKIKISHA UMEINGIA OFISINI, NA KAMA NI MALIPO LIPA KWA JINA LA KAMPUNI YA ILE YARD NA SIO MTU BINAFSI.
 
Matapeli ya hivyo hayatakiwi kua yanapelekwa police,ni wasiojulikana wanapiga operation za kimya tu kama kuyagonga na gari,kuyafunga jiwe kuyadumbukiza baharini,etc
 
Jamaa mwenye pesa aliangua kilio pale pale! akasema nimedunduliza sijui ningesemaje, mm natangulia home mkoani mtaniletea gari!

kwa hiyo baada ya kunusurika kutapeliwa 11M na kulia machozi, bado akakuachia hela akasema "mimi natangulia home mkoani mtaniletea gari"!

stori nyingine ni za kutufanya Watanzania wajingaaaaa!
 
Yard nyingi wanadanganya mwaka gari imetengenezwa maana wanajua watu hufuta mwaka.
Yard zote huchezea speedometer kushusha mileage.
Yangi nyingine hubadili vifaa
Yard nyingi huongeza bei halisi ya gari kwa zaidi ya milioni 1
 
Kwanza sipo hapa kuharibu biashara za watu au kuhoji utendaji wa Jeshi la Polisi, ila nazungumza lipo

Kumekuwa na utapeli mkubwa unaoendelea kwenye Yard za kuuzia magari, na huu umekia ukiendelea miaka na miaka, na bila wahusika kushugulikiwa

Swali je hawa matapeli wanashirikiana na wamiliki wa yard, na vipi kuhusu Jeshi la Polisi, kwasababu kuna kesi zipo miaka na miaka bila wahusika kukamatwa

Yard zinazoongozwa kwa watu kutapeliwa ni hizi za Kinondoni na hizi za kutoka Morocco kuja Victoria, chunga sana hapo

Kinachoendelea ni hiki; Mfano umekua ukipita kuangalia gari, kwenye yard matapeli wameshakuona muda mchache wameshajua wewe unatafuta gari gani, wataanza kukufwatilia, Pili mfano umetangaza sehemu yoyote unatafuta gari, ukaacha contact basi jua na hapo matapeli watakutafuta, Tatu sijui wananusaje, ukishaanza kutafuta gari, kuwa makini wanaweza kukunusa

Kinachoendelea ni hiki, Mfano umetangaza unatafuta Noah labda ya Milioni 10 basi utapigiwa simu nyingi, na moja wapo inaweza iwe ya matapeli, Sasa tapeli anakuambia Noah Yard au kuagiza ni Milioni 14 ili kuna za bondi ambazo zipo kwa Milioni 9 unarushiwa na picha nyingi za Noah amabzo zipo kwenye zile Yard

Sasa tamaa inaanzia hapo kuagiza ni 14m kwa mtu labda no C ni 8M ngoja nikazichek hizi za bondi za Milioni 9 ukishakua na wazo kama hilo umeshaanza kuingia mkenge

Ukishawatafuta watakupeleka kwenye zile Yard kama ile picha yadi ipo pale Kinondoni watakupeleka pale, Hizi za pale Victoria kua makini sana

Ukishakutana nao pale utakagua gari vizuri kabisa, na kupewa funguo na kuwasha kabisa kitu iko manganyu. Basi utaongea nao pale wakupunguzie pamoja na usajili basi utakubaliana nao. Kosa linakuja pale unapotaka kuamini kuwa ni zaidi ya bondi mtu akitakiwa kulipa iwe bandarini au popote.

Watakuambia upewe akaunti namba ya kulipia usajili uanze, ukienda kulipia bank amini umeshaumia. Au wanajifanya wana mwanasheria wao feki mkaandikishane, hapo pia ukiwapa cash uneshaumia

Kwanini nimewaweka wamiliki wa yard humu, Wanajua huu utapeli upo je kwanini wanaruhusu mtu kuja kukagua na kumpa mpaka funguo, bila kumwambia aingie ofisini(japo hapo si lazima) ila kwasababu ya utapeli ni viziri aingie ofisini

Kwanini nimewaweka Jeshi la Polisi humu

Huu utapeli wameshajua upo na unaendelea! ukweli ni kwamba hatua hakuna wanazozichukua. Pili Mtu akishatapeliwa utafwatilia wee polisi mpaka utachoka

Sasa mfano polisi mmeenda mpaka benki, mkaonyeshwa cctv ya yule tapeli, na mkafwatilia mpaka mkapata na Leseni ya udereva ya mhusika, na bado hamna kitu, mkapata taarifa za matapeli na sehemu wanazokaa mnamwambia alietapeliwa aweke mafuta! ukweli ni kwamba jeshi la polisi linajua huu utapeli, ila sijui nini kinaendelea

Kama unataka ushahidi nenda Osterbay polisi utakutana na hizi kesi nyingi! nina visa vingi ila kuna jamaa anafwatilia kuanzia mwaka juzi! kuna wengine miaka na miaka zipo.

Kilichonikumbusha huu utapeli ni kwamba, kuna jamaa alinitumia pesa toka mkoani nimtafutie Noah old model used kwa 11M, basi nikawa namtafutia, siku ya kwanza akafikia hotelini tukakosa gari, siku yapili tukakosa, bado tuko tunatafuta noah na madalali, loo jamaa sijui matapeli walinusa vipi

Wakamwendea yule mteja sisi hatujui, wakamwambia kuna za bondi zipo kwa 9M jamaa kusikia hivyo akasema sisi tunamyeshusha akaenda kuona gari yadi za kule victoria, akakutana na jamaa kama mpemba pale, akaonyeshwa gari kitu chasses na usajili 9M huku mimi nina Milioni 11 yake kwenye account, akanichek na kuniambia amepata gari, tukutane bank mlimani, basi tukakutana pale, mimi nipo na jamaa yangu ambaye tulikua tunamtafutia, yeye yupo na wale matapeli kwenye gari akashuka na document feki za ile noah, pamoja na account no

Amesema amepata noah chases ya 9M tukasema wapi na wapi, means walengaji wote town hawajaiona?
Tulibishana pale akasema pesa ni zake tumpe, Kusoma zile documents chases haziendani na Noah! nikamwambia twende tukaone gari, wale matapeli wanasema mnamchelewesaha tu mwenzenu, jamaa nae akasema sisi sio, nikamwambia pesa ipo kwenye account yangu, sitoi hiyo pesa hata uniue ila lazima nione kwanza gari, nitalipia bajaji twende tukaione, ukaita bajaji wale madalali wakasema nyie tunawafwata nyuma, sisi kwasababu tulivurugana tukapanda wote kwenye bajaji, wao wakawa anakuja nyuma, basi kwenye bajaji hakuna kuongea

Kufika kwenye Yard bado ile noa ipo, kusubiri wale jamaa hawajatokea mpaka leo, pale tukamkuta singa singa mwingine hapo tunaanza kukagua ile gari, anatuuliza vipi, Tukamwambia tulitaka kulipia hii gari, akasema niliwanona mnaangalia, noa ni 14M, tukamwambia tulishakagua tumepewa account tukalipe, akatuuliza duh mlishalipa tukamwambia bado akasema mshukuruni Mungu, wale ni matapeli!

Jamaa mwenye pesa aliangua kilio pale pale! akasema nimedunduliza sijui ningesemaje, mm natangulia home mkoani mtaniletea gari!

KUNA MENGI YA KUJIFUNZA, ILA UKIENDA KUONYEHSWA GARI YARD, IWE NA MTU YOYOTE HATA NDUGU YAKO, HAKIKISHA UMEINGIA OFISINI, NA KAMA NI MALIPO LIPA KWA JINA LA KAMPUNI YA ILE YARD NA SIO MTU BINAFSI.
Tapeli humweka mtu katika mizani na kuona huyu wangu au sio wangu.
cha kushangaza watu kwenye hela nyingi sio wajanja ni wakulima, wauza mazao na ng'ombe hawa kuwapiga ni dakika sababu anapandisha grade take wamwone kwa kununua gari sababu nyumba tayari anayo.
 
Tatizo la Watanzania wengi ni kupenda vitu vizuri kwa bei ndogo ndio maana tunatapeliwa. Unajua kabisa gari fulani inauzwa Tsh kadhaa inakuwaje unakubali kwa bei ndogo?

Kwenye yard imeandikwa kabisa biashara zote zinafanywa ofisini tu.
Sijui we we unatoka wapi una akili ya watanzania 115

Asante sana.
 
Kuna mafunzo meng kwenye hii stori asante mkuu kwa kushare huu ujumbe

Back
Top Bottom