MsemajiUkweli
JF-Expert Member
- Jul 5, 2012
- 13,185
- 24,055
Kumbukumbu zinaonyesha Mheshimiwa Zitto Kabwe aliwahi kufanya mahojiano maalum hapa Jamiiforums ambayo yaliongozwa na Mwanadada AshaDii. Mahojiano hayo yalifanyika tahere 22 Novemba, 2012.
Zitto Kabwe aliongelea mambo mengi ya kisiasa lakini mojawapo ni matokeo ya vyama vya siasa baada ya Uchaguzi Mkuu 2015.
Moja ya swali aliloulizwa ni hili; Unalizungumziaje suala la kuwa na utitiri wa vyama vingi vya siasa vinavyokula pesa za walipa kodi halafu havina tija wala mchango wowote kijamii zaidi ya kutufilisi, je kuna umuhimu wa kuifanyia sheria mabadiliko ili kuwe na limitation mfano, vyama vitatu tu?
Majibu yake ni haya;
Tusiminye kabisa watu kuwa huru kuanzisha vyama vya siasa. Baada ya muda ni vyama vyenye uwezo wa kukonga nyoyo za wananchi ndio vitabakia. Wala hatuna haja ya kuweka sheria. Huko mbele ninaona Tanzania yenye vyama sio zaidi ya 4. Vyama vikubwa 2, CCM and CHADEMA. na CUF watakuwa a balancing party kama ilivyo LibDems UK au Greens and Liberals Ujerumani. Kwa hali ya sasa ya muungano ninaona kuwa CUF yaweza kuwa kama The Bloc Québécois ya kule Canada. Sioni NCCR ikidumu. Soini future ya UDP bila Cheyo na TLP bila Mrema.
Lakini pia kuna uwezekano mkubwa sana wa Kundi moja la CCM kuunda chama kingine cha siasa ambacho kinaweza kuwa na nguvu hata zaidi ya CHADEMA. Baada ya uchaguzi wa mwaka 2015 tutaona hivi new configurations. Tuache watu wawe huru kuunda vyama. Vyenye nguvu vitabakia.
Yaliyojiri kwenye huu utabiri wa Zitto:
NCCR-Mageuzi-Kimebaki na mbunge mmoja, kwa maana nyingine kinaelekea kaburini.
CUF-iko mbioni kumeguka na athari yake ni CUF kuwa imara upande mmoja pekee wa Muungano (Zanzibar) katika ajenda ya madaraka kamili kama kilivyo chama cha The Bloc Québécois huko Canada.
CHADEMA-Kwa sasa ni chama kikubwa baada ya CCM.
UDP na TLP zinapotea katika uwanja wa siasa nchini.
CCM kumeguka- CCM haikumeguka bali kuna kundi la heavy hitter lililotoka CCM na halikuunda chama bali lilikimbilia kwenye vyama vya upinzani. Sidhani kama ACT-Wazalendo ni kundi ambalo Zitto alikuwa anaongelea kwa sababu hata itikadi za ACT-Wazalendo ni social democracy kama ilivyo CCM kwa mbali.
Je, ACT-Wazalendo itaweza kuwa na nguvu zaidi ya CHADEMA?
Je, bado kuna uwezekano wa vyama kubaki vinne?