Je, ushawahi kuchukiwa na mama mjamzito?

Je, ushawahi kuchukiwa na mama mjamzito?

Kadhakan

Senior Member
Joined
Jul 20, 2026
Posts
115
Reaction score
174
Zuchu ameweka wazi kuwa katika kipindi cha ujauzito wake alikuwa hampendi mume wake Diamond Platnumz kiasi kwamba hata akiwa amelala anatamani hata ampige kibao.

Kupitia ukurasa wake wa Snapchat amepost video hii na kuandika "I hated him nilikua simpendi hapo kama nimtie kofi"

Soma pia: Zuchu na Diamond wanatarajia kupata mtoto wa kike

Vipi umeshawahi kupitia hali hii? Kuchukiwa na mjamzito na ilikuwaje?

Source: Simulizinasauti
 
Kuna wakati unatamani hata usilale kitanda kimoja, maana geuko lake tu unahisi anatafuta ugomvi. Hormones are crazy, cha msingi ni kukwepa makofi tu hadi miezi tisa iishe!
 
Wanafanya makusudi wanakuwa na visirani vyao vya muda mrefu tu ,mimba kama kizingizio tu.
Mke wangu alinipiga mwiko wa kichwa bila sababu nikamrudishia kibao matata sana tangu siku hiyo mimba zake zote hajawahi kuniletea visirani
Kabisa chief
 
Hata kwa kunidanganya sawa, ili mradi uongo uwe na logic.
Kuna mambo ni kawaida 99% kuletwa na ujauzito mfano; usingizi kupita kiasi, kupenda au kuchukia vyakula fulani.

Imezoeleka kuongelewa kwamba ujauzito huleta tabia ambazo mwanamke hakua nazo kabla sasa hapo ndo wanawake wengi huwa tunatumia kigezo hiki kuhalalisha baadhi ya tabia tulizokua tunajizuia kuzifanya mwanzo.
Mfano; Ugomvi, uchafu
 
Sawa nimekuelewa, mfano wewe kabla ya ujauzito ulikuwa unaipenda labda perfume yangu fulani lakini baada ya kuwa mjamzito ghafla unachange yani nikiwa karibu yako ile harufu inakuwa mbaya sana kwako kiasi kwamba hautaki nikukaribie.

Situation za aina hii huwa mnasingizia kweli Ephen?
 
Inategemea! Ila kwa mfano huo wa perfume asilimia kubwa hasingizii
 
Wanafanya makusudi wanakuwa na visirani vyao vya muda mrefu tu ,mimba kama kizingizio tu.
Mke wangu alinipiga mwiko wa kichwa bila sababu nikamrudishia kibao matata sana tangu siku hiyo mimba zake zote hajawahi kuniletea visirani
Na hayo wanafanya wale wenye maisha safi hawa wengine pangu pakavu au mimba kapatia nyumbani hawana hizo mambo
 
Ila MJAMZITO akikupenda sasa,utaomba ajifungue mapema.
 
Niliwahi pendwa na mjamzito from no where tu hata sikuwa na mazoea nae. Jamani alinisumbua yule mama sina hamu🙆‍♂️🙆‍♂️
 
Eeh hapa Zuchu amesema ukweli wa mwanzo kabisa, mjamzito hormones ni kitu cha ajabu sana. Mke wangu alikuwa ananipiga makofi tu na kunitaka nisilale kitanda kimoja, geuko lake tu nilihisi anataka ugomvi kila siku. Nilikula kimya tu hadi miezi iishe, sasa ndio anarudi kuwa mwanadamu tena. Hata Diamond anajua hii kitu, yeye amepitia na wasichana wengi hivyo anaelewa.
 
Back
Top Bottom