Je, uongozi wa Roman Catholic ni 'ndumilakuwili' au huyu Papa tumepandikiziwa? Tutegemee nini?

Teslarati

JF-Expert Member
Nov 21, 2019
1,728
6,792
Uongozi wa Roman Catholic kwa miaka 15 iliopita umekua na changamoto sana hasa hasa kuhusu mambo ya ubakaji, rushwa na ushoga.

Miaka ilopita tulishuhudia Papa Benedict anajiondoa kwenye kile kiti, kitendo ambacho kilizua maswali mengi sana. Japo baadhi ya watu wanadai Papa Bemedict alikua anasukumwa na baraza lake kuidhinisha vitendo vya 'laana' ikiwemo ndoa za jinsia moja - ushoga. Hivyo ili kulinda agano lake kwa Mungu na mtangulizi wake (pope John Paul II) ikabidi aachie kiti kuliko kufanya maamuzi yanayoruhusu kuingiza laana kwenye kanisa.

Kwa hali inayoendelea kwa sasa kuna maswali mengi yanajitokeza.

kwa nini Roman Catholic wasiruhusu kubariki ndoa za wake wengi waje kuruhusu kubariki ushoga?

Kwa nn wasiruhusu na kubariki utumiaji wa njia za uzazi wa mpango waje waruhusu ushoga?

Kwa nn wasiwaruhusu makasisi kuoa waje waruhusu kubariki wanaume kuoana wao kwa wao?

Nimesoma huo waraka ulotolewa unadai haujaruhusu ndoa za jinsia moja ila umeruhusu 'kubariki' mahusiano ya jinsia moja. Kitendo cha kuruhusu kubariki haya mahusiano ya kishoga si ndio hukohuko kutoa go-ahead watu wafanyiane mambo ya sodoma na gomorra.

Je, sisi wazazi tutawaambia nn watoti wetu tunaowakataza kuangalia tamthilia za kifilipino na kizungu zinazoonesha ushoga lakini tunawaruhusu kwenda kanisani ambapo viongozi eake wameambiwa wabariki ushoga? Kwa maneno mengine Roman Catholic imeruhusu mashoga kwenda kanisani wameshikana kama couple za kawaida.

Tumaini pekee la kuokoa kanisa dhidi ya huu ufilauni ni hawa 'Conservative Cardinals' na hata wakiweza wamuondoe huyu Papa kwemye hicho kiti maana kwenye uongozi wake hakuna kikubwa alichofanya kwenye kanisa zaidi ya kuharibu miiko iliopo toka zama na zama.

Mtakatifu Yohanna Paulo wa pili, Utuombee. Amen
 
Ramon catholics ni capitalists Iman inatumika tu kama chombo cha kuwafikisha pale wanapo taka kufika.
Kuna muda kanisa huwa linaingiliwa na mapapa ambao actually ni 'projects' za kakikundi fln ka watu wanajiita wanaotaka kufanikisha New World Order.

Ninahisi huyu wa sasa ni project, ila nguvu iliolisimamisha kanisa kwa zaidi ya miaka 2000 itamuondoa na kurudisha kanisa kwenye miiko yake.
 
Huyu wa sasa ni pandikizi la wazee wa suti,thus ana mambo ya kijinga. Yule aliyekufa aliona hatia na anamkosea Mungu kuliingiza kanisa kwenye ushetani akatumia trik ya matatizo ya kiafaya akajiuzulu ili kuwakacha wajenzi huru. Huyu chenga inatakiwa kanisa limuondoe haraka.
 
wanaotaka kufanikisha New World Order.
Tuliwataahadharisha mkatubinulia midomo
20230604_005828.jpg
 
Huyu wa sasa ni pandikizi la wazee wa suti,thus ana mambo ya kijinga.
Yule aliyekufa aliona hatia na anamkosea Mungu kuliingiza kanisa kwenye ushetani akatumia trik ya matatizo ya kiafaya akajiuzulu ili kuwakacha wajenzi huru.
Huyu chenga inatakiwa kanisa limuondoe haraka.
huijui roma ww ndo umevamia roma yaan uijue roma kuliko baraza la maaskofu vatikan?? na waroma walivosystematic vile unadhan papa atakuwa kajitangazia tuu??
 
Wamenikata stimu sana hawa jamaa. Sijui nitawaambia nn watoto wangu. Paroko wangu aliwahi kusema 'neno ushoga hata halipaswi kuongelewa sababu ni laana tu hata kulitamka'
Niliacha siku nyingi kuamini hizi dini, nipo nipo tu yaani wala sizifatishi. Wewe tenda matendo mema fundisha watoto wako matendo mema. Mungu atajua mwenyewe aamue vipi
 
Back
Top Bottom